Top five ya wasanii wakali wa Hip Hop Tanzania

Binti malkia je utanipa denda hata kama ujapiga mswaki!
Binti malkia mie nakuzimia
 
Roma gan yule yule aliyeimba k yaan mpaka pale kati ni k au mwingine mbona sijakuelewa
Huyo huyo. Kayumba kwenye msimamo. Unajua nini? Kwa sasa baadhi ya wasanii imebidi waige aina flani za mziki ambazo zinashika soko kwa sasa. Muziki kama wa msaga sumu na singeli ndio miziki inayobamba vijana kwa sasa.

Anafukuzia soko mkuu.
 
Sugu ni mwiz wa kaz za wasanii aliiba ngoma ya mr blue inaitwa freedom huyo anazingua mtoe
Make It Rain ya Fat Joe, Byser alipata ruhusa kwa Fat Joe?

Alafu una ulimsikia Master J kuhusu hiyo ngoma?
 
Hip Hop ni nini?
 
Hip hop ni aina ya muziki unaoelezea aina ya usanii na utamaduni uliyotokana na jamii ya Wamarekani Weusi na Walatino kunako miaka ya 1970 mjini New York City , hasa katika
kitongoji cha Bronx.
DJ Afrika Bambaataa alieleza kwa
muhtasari wa nguzo nne za utamaduni wa Hip hop: U-MC , U-DJ, breaking na
uandikaji wa graffiti.
Elementi nyingine ni pamoja na
beatboxing .
Uenezi
Kwa vile imeibukia kutoka mjini South Bronx , utamaduni wa Hip hop umeenea
dunia nzima.
Muziki wa hip hop awali ulianzishwa na Ma-DJ waliokuwa wanatengeneza midundo kwa kutumia mtindo wa kurudirudia na kusimama (hasa katika visehemu vidogo vya muziki wa kusisitiza mwelekeo wa kigongoma) b turntable mbili, hasa hujulikana kama kusampo muziki.
Hii baadaye ikaja kusindikizwa na "rap", mtindo wa wizani unaotoa maneno au mashairi yaliyo kwenye vipimo vya mstari ulalo wa nota 16 katika fremu ya muda, ikiwa sambamba na beatboxing, maujanja ya sauti hutumika hasa katika kugezea mfumo wa midundo na elementi za muziki mbalimbali na mautundu na vionjo kadhaa kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.
Muundo kamili wa kudansi na staili kadha wa kadha za mavazi zimezua mashabiki miongoni mwao katika muziki mpya. Elementi hizi zimeonesha mabadiliko ya na maendeleo kadha wa kadha katika historia ya utamaduni huu. Baadhi ya miziki ya hip-Hop hutoa maelezo ya kisiasa.
Mahusiano baina ya graffiti na utamaduni wa hip hop unatokana mionekano mipya tofauti iliyoongeza ufafanuzi wa kina na uenezi tofauti wa kivitendo ambapo kwingine walichukulia elementi ya hip hop kama sehemu ya sanaa, kukiwa na mpitilizo mkubwa baina ya hao wanaondika graffiti na hao wanaotenda elementi zingine za hip hop kivyao. Leo hii, graffiti imebakiwa kuwa sehemu ya hip hop, wakati kwa upande wa sanaa imechukua eneo kubwa katika masuala ya picha na michoro katika maeneosho mbalimbali duniani kote.
 
Afu nilikua nimesahau pro jay anaimba hip hop singeli siyo hip hop yenyewe
Zali la mentali,Ndio Mzee,Jina Langu,Bongo Dar es salaam,Chemsha Bongo,Niamini,Nang'atuka,Nikusaidieje,Promota anabeep zote zilikuwa Hip Hop Singeli?!

Au wakati ule ulikuwa bado ujafika mjini?!

Kwa kukusaidia hakuna msanii wa Hip hop mwenye hit songs(nyimbo za taifa) nyingi bongo kama Profesa Jay au unaowakubali wewe wote waliamua ku-rap kisa Profesa Jay ni Role Model wao.
 
Huyo huyo. Kayumba kwenye msimamo. Unajua nini? Kwa sasa baadhi ya wasanii imebidi waige aina flani za mziki ambazo zinashika soko kwa sasa. Muziki kama wa msaga sumu na singeli ndio miziki inayobamba vijana kwa sasa.

Anafukuzia soko mkuu.
We nimetoa list ya wana hip hop sio ya wasanini wanao tamba au wasanii wa singeli wasanii wanaotamba wapo weng lakin sio wa hip hop hapa tuna jadili wana hip hop sio wanaotamba nazan had kufikia hapo utakua umenielewa
 
Punguza mahaba kwa profesa we mzalamo kuna watu wameanza hip hop kitambo kabula hata ya huyo profesa wako
 
Punguza mahaba kwa profesa we mzalamo kuna watu wameanza hip hop kitambo kabula hata ya huyo profesa wako
Sasa hapa mimi namzungumzia Profesa Jay wewe wazungumzie hao watu wengine walioanza kabla ya Profesa Jay.

Vipi kuna tatizo kwenye hilo?!
 
Acha zako arusha hakuna wasanii wa hip hop
Arusha kuna wavuta bange tu wanaojificha nyuma ya kivuli cha Hip Hop.

Mtu anakwambia Jcb Mara Chindo Man watu ambao hawana Hit Song hata moja ya kueleweka.
 
Kwa hiyo unataka kusema Kwenye hip hop hakuna mapenzi?!

Stamina Ana Wimbo unaitwa bora nikuoe humo mapenzi tupu.

Roma Ana Wimbo unaitwa mtoto wa kigogo na nyingine
maumivu humo mapenzi tupu.

Ney wa mitego ana nyimbo kama mapenzi kamari na akadumba humo mapenzi tupu.

Eti unamuweka madee Kwenye kundi la Hip hop alafu Mtu kama Fid,Jay na Mbishi unawatoa aiseee we jamaa wa ajabu mno.

wakina Jay z,Snopy Doggy,50 Cent,Tupac,BIG,Nas,T.I wote wana ngoma za mapenzi sasa hao nao sijui utasema hawafanyi hip hop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…