Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Umedadavuwa vyema ukipata muda itapendeza ukituandalia makala ya Korea peninsula hasa ukiweza kuireview series ya Iris, hii series inaakisi mgogoro mzima wa Korea peninsula na unseen power na power within.Hahahah! Movie za james bond zina details nyingi sana pamoja na 'chumvi'..
MI6 na MI5 bado sijawahi kusikia kuweka hadharani mafaili ya siri nzito kuhusu shughulo zao ingawa siku za karibuni nimeona wameanza kuweka utaratibu wa kuwa na Kumbukumbu za Usalama wa Taifa (National Security Archives) lakini kadiri nilivyoangalia sijaona yale mambo mazito mazito yanayotia hamasa watu kufuatilia.
Nadhani hii pia inachangiwa na raia wa Uingereza kutokupenda "kudeka" sana kwa serikali yao. Unajua kingine kinachowaponza CIA na serikali ya marekank ni vile raia wake wanapenda sana "kudeka" ile kujifanya wanasimamia haki zao hata kama wanahatarisha siri za nchi. Ndio sababu hata ya kutungwa kwa "Freedom of Information Acy" ili kumaliza malalamiko ya wamarekanj kuhusu "haki" yao ya kujua "mwenendo" wa nchi yao..
Ila huko mbele tutegemee kuanza kuvuja au kuwekwa hadharani kisheria mafaili yahusuyo shughuli za MI6 na MI5.
Ukiwatazama watu kama Baek san jinsi wanavyoweza kuigiza kiumahiri sasa vipi wakiwa kikazi kwenye reality?
Hili ni ombi maalum naomba uiliview IRIS na ukizingatia mtoa ombi ndio Ankal wa Nifah basi hili ni moja ya sharti katika mahari ya huyu Ankal wangu Nifah.