Tottenham Hotspurs Thread

Hahaa,, kwenye vikombe hapo... Sijui tufanyeje, lkn navyoona timu y mourinho naishiwaga nguvu kabisa! Uliona sanchez alivyokua anamkaba gundogan..[emoji2960]
Kama kweli mourinho anataka vikombe hvyo,, aanze kubadili game approach sasa, na kujua kwenye defence anaenda na wapi ambao nao tunatak tuone, consistency zao kwa hizi game zilozopo.

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
Nachoelewa Mafanikio ya kocha ni vikombe alivyovipata katika timu husika.
Uyu mwamba katika msimu wake wa kwanza united aliwapa vikombe vitatu Europa,,,Carabao cup na ile ngap ya jamii. Akiwa real madrid nako aliwapa vikombe vitatu kikiwemo LaLiga Santander title kwa pointi 100 na magoli 121.
KWA iyo uyu jamaa kote alikopita hakuna ambapo hajafanikiwa Mana kuna makocha timu zao zinapiga pasi 900 katika mechi ola kwenye kabati hakuna kombe hata moja.
Hakuna mpira mzuri husiokuwa na kombe.
 
Nilipenda sana namna D Sanchez alivyojaribu kumkaba Gundogan. Alizidiwa uwezo ila alionesha determination ya hali ya juu sana. Hicho ni kitu nakipenda kutoka kwa Jose; kumfanya mchezaji anayejitambua kucheza to the fullest bila kujalisha level ya kiwango chake. Mchezaji anajituma kama yuko vitani vile.

Ila namshauri Levy ampe Mourinho anachotaka dirisha lijalo. Aache mambo ya kutafuta cheap bargains kwenye zama hizi za soka. Kwa defense hii ya Spurs naamini angekuwa kocha mwingine hasa hao wanaocheza attacking football, timu ingekuwa inasubiri kuona ratiba ya mechi zake za Championship msimu ujao.

Imagine mechi kama ile ya City tungekuwa na kocha kama Bielsa wa Leeds ambaye angetaka kushambulia tu. Ndiyo zile mechi City anashindaga goli 9.
 
Kiukweli sikufurahia Mou kuja kuifundisha Spurs, Mourinho ni winner by nature, ukimletea wachezaji anaowataka andaa kabati la kujaza vikombe.
Levy ana deals ngumu na za ubahili, timu haina uwezo wa kupigania mchezaji yoyote mkubwa. Hivyo hii timu kushinda kombe ni kocha atumie akili zote kichwani ndio atoboe, kutokana na hilo mafanikio yake ni amsha amsha tu uwanjani ili ifaulu UEFA, hakuna cha zaidi.
Mpaka sasa unasikia club kama Chelsea, Man au Liver tayari wanafuatilia kwa ukaribu wachezaji wa msimu ujao( tena zile big guns kwa Ulaya.
Levy kanunua wachezaji wa mafungu na wengine kwa mkopo(tena wakiwa wameflop kwenye timu zao) kakaa kakunja nne anataka kunyanyua kwapa kwa kuchukua makombe. Hii biashara huenda isilipe.
 
#COYS

Leo tumewapiga hawa wakulima Wolfsberger FC.

FT: 1 - 4

Kizuri ni kuwa Bale, Dele Alli, Lamela, Moura, Winks, Vinicious na flops wengine wameosha nyota leo kwa magoli na assists.

Pia tuliua mchezo kipindi cha kwanza hivyo kutoa nafasi kwa Sonny kupumzishwa. Ikumbukwe kwamba Sonny alikimbia km zaidi ya 28 kwa kila mechi, dhidi ya Everton na dhidi ya City. Hivyo ilikuwa muhimu leo acheze dk chache tu. Mwenzake Kane kapumzika mapema mara tu baada ya game ya City. Kapewa off duty siku hizi mbili tatu.

Kibaya ni kwamba bila wachezaji wetu kufungisha mechi haijaisha. Sissoko kamwangusha mtu kwenye box wakapata goli.

Siyo mbaya. Next stop Jumapili vs Burnley. Mechi yetu ya marudiano Europa itakuwa Jumatano badala ya Alhamisi. Sijui kwa nini.

#COYS
 
Jumapili ni Tottenham vs Westham, Burnley ndio game ya ligi itafuta baada ya hiyo ya Jumapili. Kwa game hizi naamini Mou atapata matokeo.
 



Bale is getting back people. Kwa hii display ya game iliyopita huenda leo akaanza. Ni aibu kuwa na tatizo la RW wakati tunaye Bale kikosini. Aoneshe ukomavu wake kwa kushusha performance nzuri match in match out.

My prediction vs West Ham; 4 2 3 1

Hugo, Doherty, Davies, Dier, Toby, Hojbjerg, Sissoko, Son, Ndombele, Bale, Kane.
 
Watetezi wa Mourinho mko wapi tajiri anajiandaa kumtimua huyo kinyago wenu na kumchukua Brendon Rodgers wa Leicester City
 
Levy kasema anasubili msimu uishe afanye maamuzi ya kumtimua au hapana.Leo tena West Ham wamejinyolea mwendawazimu
 
Mtafutieni Mou timu ya kufundisha spurs anachukua kocha mwingine la sivyo anarudi kucheza na dog wake home
 
Mtafutieni Mou timu ya kufundisha spurs anachukua kocha mwingine la sivyo anarudi kucheza na dog wake home
yaani nawaambia kila leo na sitaacha kuwaambia kwa mpira wa kisasa Mou kaishiwa hana tena jipya makocha wengi wameshamjulia yani akijilinda anapigwa,akifunguka anapigwa hajui hata afanyeje.bado yule mwenzake wa LA LIGA kashaanza kudondosha point akikutwa na kupitwa wala sitashangaa maana wote wana mipira ya hovyohovyo tu.......NB. furaha yangu ni kuona Mourinho anafungwa kila leo.
 
Ivi mpira wa kisasa upoje tuelewashane kwanza hapo?
Afu timu ngapi zinacheza mpira wa kisasa zitaje?
 
Furaha yako itakamilika mwishoni mwa msimu. Pale Mourinho atakapokuwa na kikombe (Europa/EFL). Wewe utakuwa na modern football aka attacking football but trophyless.
 
Watani mna hali ngumu kiukweli. Kinachoniuma ni kwamba sioni timu ikijiandaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…