Tottenham Hotspurs Thread

Tottenham Hotspurs Thread

Hawa kulikuwa na uwezekano wa kuwapiga mkono

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Game kama hizi ndiyo inapaswa kufanya mauaji. Mpinzani hana ulinzi kabisa. Siyo mbaya. Sasa tumeingia kundi la pointi 29. Hii ligi ni [emoji91][emoji91][emoji91]. Kabla ya mchezo huu, timu 6 zilikuwa zimefungana pointi (26) zikikalia nafasi ya 5 mpaka 10.

City ni wa nane ila akishinda game za mkononi anakuwa wa 3!

Ligi bora zaidi duniani.
 
Bado imejengwa kuwazunguka Kane na Son. Mourinho ana kazi ya kuijenga upya isiwe timu ya wachezaji wawili tu.
Bale alitarajiwa awe back up nzuri ya hawa, ila sioni dalili. Timu inahitaji kuimarisha beki za kati na mshambuliaji aliye na uwezo wa kutupia.
 
Bale alitarajiwa awe back up nzuri ya hawa, ila sioni dalili. Timu inahitaji kuimarisha beki za kati na mshambuliaji aliye na uwezo wa kutupia.
Bale kwa kweli anazingua maana hata game ndogo anazoanzishwa hana sharpness kabisa. Kwa jinsi kocha alivyoongea jana kuhusu usajili ametengeneza "utata" ikiwa tutasajiri au la.

Kikwazo chetu kikubwa kwenye usajili ni uwiano baina ya wachezaji wa ndani na wa kigeni. Ili tupate mchezaji wa kigeni ni lazima tuuze kwanza. Mfano; Ili tununue beki ya kati inabidi kuuza kwanza D Sanchez au Dier. Dier sio home grown player. Alikulia Wales/Scotland.
 
Niaje watu wangu wa Spurs a.k.a Mourinho people!

Ni hivi, leo tunacheza na Brentford na kama kawa Mourinho anaheshimu kila kikombe kwa hiyo kashusha full squad. Hivyo tutarajie kuona "full dozz".

Screenshot_20210105-220911.jpg
 
Mushinde leo tukutane final, ili isionekane MUFC kamchukulia (kombe) kibonde.
Kwa jinsi City walivyocheza game ya juzi na Chelsea, nimeanza kuwa na hofu wanaweza kuwatoa. Mkumbuke kuwa hamna kocha pale hivyo mechi zinazoamuliwa kwa mbinu kama hizi za knockout mnakutana na majanga.

Nataka mpite ili Jose awape bakora zingine.
 
Waandishi wengi wa habari kwa kutompenda Jose hujikuta wanaishia kuonekana wajinga zaidi.

Mwandishi anauliza kuwa timu kubwa hazichukulii michuano hiyo seriaz hivyo nini mtazamo wa Spurs!

Mourinho anamjibu kuwa hakumbuki lini timu nje ya top six kama akina Swansea ilichukua kikombe hicho! Kwa mwendo huo hawawezi kumpenda maana anawafanya waonekane vituko.

Kombe ambalo Pep kalibeba mara mbili au tatu, Chelsea, United, unasema timu kubwa hazilitilii maanani! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jose for you.
 
#COYS

Jumapili saa 20:00 tunacheza mechi yetu ya kwanza ya FA na Marine FC. Zifuatazo ni dondoo kadhaa kuhusu haka katimu.

Ni mchezo wa ndoto kwao. Spurs ndiyo timu kubwa zaidi wamewahi kucheza nayo katika miaka zaidi ya 120 ya historia yao.

Timu iko ngazi ya 8 ya mfumo wa ligi ya Uingereza (eighth tier). Hivyo ni non league team.

Kikosi chao kina wachezaji 19 tu ambao ni wafanyakazi kwenye taasisi zingine! Walimu, madaktari, mafundi, nk!

Kwenye siku ya mechi wanaweza kuhudumia (kulipa) wachezaji 16 tu.

Mishahara ya wachezaji wao ni kati ya £100 na £300 kwa wiki.

Kocha wao imembidi kuomba ruhusa ya wiki moja huko kazini kwake ili aweze kuandaa kikosi na mchezo wetu!

Kiwanja chao cha mazoezi kimejaa theruji hivyo wamesaidiwa na jirani zao Everton na Liverpool kwa kuruhusu watumie viwanja vyao vya mazoezi.

Hawana uwezo wa kupata michezo iliyopita ya Spurs kwa ajili ya kuipitia hivyo Liverpool wamewasaidia katika hilo.

Wachezaji wa Spurs watalazimika kubadilishia nguo kwenye baa iliyoko jirani na "kiwanja" chao kutokana na restrictions za Covid 19. Hivyo Spurs watavuka barabara kuingia kiwanjani kutokea "dressing room"!

Kuna tofauti ya nafasi 161 kutoka walipo Spurs (namba 4 kwenye msimamo) mpaka walipo hawa Marine FC. Hili ndili pengo kubwa zaidi la kingazi baina ya timu zinazokutana kwenye historia ya michuano hii.

Wachezaji na wadau wa timu hii wanatamani sana kucheza na kikosi cha kwanza cha Spurs kwani kwao ni ndoto iliyotimia kucheza na timu kubwa.
 
Haya matimu makubwa yamekuwa ya kiboya Sana.
Hao watoto walitakiwa wale hata 20-0
Umeona eee. Hako katimu ilipaswa kukaoshea kabisa. Hakawezi kukaa na mpira dakika nzima. Wakongwe akina Moura, Dele Alli, walikuwa wanagongeana visigino tu badala ya kufunga magoli wasafishe nyota zao zilizofifia.
 
Back
Top Bottom