Tour Guide Feki, Leseni Feki – Mfumo Mnaulinda Weh, Lakini Sisi Tutaumbua Mpaka Mwisho

Tour Guide Feki, Leseni Feki – Mfumo Mnaulinda Weh, Lakini Sisi Tutaumbua Mpaka Mwisho

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Jamani hebu tuwe real kidogo... tusiwe wanafiki walahi! Hii sekta ya utalii na utamaduni imeingiliwa na watu wa ajabu ajabu, yaani watu wa mtaani wanavua magwanda ya boda boda, kesho unamkuta anakwambia “Hey I’m your professional guide, welcome to Tanzania” – kumbe jamaa hata hajui tofauti ya antelope na zebra! Brooo!

Watu wanafoji leseni kwa hela ndogo ndogo, wanapiga deal chafu huko kwenye mamlaka husika, wanatoka na karatasi za kugushi halafu system inawalinda kama mapapa. Yes, I said it – SYSTEM yenu ni kama mama anaeweka kofia ya mwanae jua lisimuunguze – hamchunguzi, hamwajibishi, mnabeba wezi wa taaluma kana kwamba ni mashujaa wa taifa!

Na worse enough, hawa feki wakifika gate za hifadhi, wanapita bila wasiwasi, wanapewa green light kama FBI walivyo na clearance ya top secret mission! Lakini sisi wa mtaani wenye degree, wenye knowledge, wenye exposure – tumebaki kuokota makopo tu.

Let’s cut the bullshit – hii ni CRIME. Ni kosa kisheria kabisa, Sheria ya Leseni za Kazi ya Utalii (Tourism Act No. 29 of 2008, Part V – Licensing of Tourist Services) inasema wazi kwamba mtu haruhusiwi kutoa huduma yoyote ya utalii bila kuwa na sifa na leseni halali. Ukiwa na leseni feki, una commit felony, hiyo ni fraud, hiyo ni impersonation, hiyo ni deception – hiyo ni dhambi kwa nchi!

Na msiifikirie hii ni kama kuingia club bila ID – hapana bro! Hapa tunaongelea taifa, tunaongelea wageni, tunaongelea image ya nchi yetu. Imagine mgeni anatoka Germany, anaweka pesa yake, anakutana na tour guide wa kihuni mwenye English ya kuungaunga na geography ya kitoto. Ata-recommend Tanzania tena? Atawekeza tena? Hell no!

Kwa hiyo nyie ma-top boss wa mamlaka husika – this is not beef, it’s a wake up call. Acheni ku-cover mafisadi wa taaluma. Vijana wa mtaani wameelimika hadi chuo kikuu, wanazijua ethics, safety, culture, na professional tour standards – lakini mnawafungia nje kama vile ni washamba.

Real recognize real – na hawa mnaowapa leseni kwa chai ya elfu hamsini hawana kitu. Ni matapeli wa ndoto za taifa. Mkiendelea kuwasikiliza hao, basi sekta yenu itakuwa ni ya 'Fake it till you break it'. Tunahitaji system ya kweli, siyo ya kupendeleana wala kujuana, tunahitaji utu, uwazi, na uadilifu. Period.

#ReclaimTourism #LeseniFekiNiUhujumu #SupportQualifiedGuides #MfumoFekiNauliz
aUnaishiaWapi?
 
Back
Top Bottom