Toyota IST imeniangusha sana

Toyota IST imeniangusha sana

Duh HP 1100 mzee baba hiyo gari itakua na speed ngapi mkuu
ile EVO 6 iko moded stage 3 moto wake sio wa mchezo,hio GT-R ikiwa stock(480hp-545hp) inaachiwa manyoya tu.

Kuna EVO 6 niliiona kwa madiba ina HP 1100 nadhani moto wake hapo unauelewa mzee baba.
 
Wiki iliyopita niliamsha IST yangu kwenda Kahama, safari ilikuwa tamu, japo nimeumia sana kuona napitwa njiani kama vile nimesimama, japokuwa nilikuwa nakanyaga mafuta mpaka mwisho!

Nimeumia sana! Siitumii tena nimeapa
Binafsi naangalia power ya gari na reliability. Ndio maana land cruisers hasa za hard tops au mayai lakini models za zamani, ni gari nzuri sana. Ijapokuwa fuel consumption iko juu, gari kuku-let down gharama za maintenance nk. ni mara chache sana sana. Na zinadumu miaka mingi sana bila kuhitaji overhaul kubwa. Na inaenda popote na kokote bila kuharibika. Na ina nguvu hata ya kuvuka mto au kupita barabara ya tope kali au majabali bila shida. IST hata safari ya mikoani unaiumiza tu. Hio ni gari ya kupiga round za ndani ya mji tu tena kwenye lami nzuri.
 
Ligi ya nini kaka ?!. Kwanza mafuta umetumia nusu ya wao
Msiangalie sana ku-save mafuta. Gharama mnazotumia kufanyia hayo magari maintenance inazidi kabisa gharama za mafuta mtu mwenye land cruiser. Manake at the end of the day, mtu mwenye land cruiser gari inadumu miaka na miaka, yako imeshaisha. Umemalizwa garage, yeye hajaumia maintenance. Gari yake inakanyaga popote kokote muda wowote, yako haiwezi. Msiangalie sana mafuta, angalieni reliability ya gari. Hapo ndio mnakosea
 
Wiki iliyopita niliamsha IST yangu kwenda Kahama, safari ilikuwa tamu, japo nimeumia sana kuona napitwa njiani kama vile nimesimama, japokuwa nilikuwa nakanyaga mafuta mpaka mwisho!

Nimeumia sana! Siitumii tena nimeapa
Wenzako huto tugari tukiwachelewesha wanavipakata kwapani ndukii
 
Mbona inawezekana tu. Hapo sio suala la model ya gari, ni suala la engine. Ukiweka more powerful engine kwa gari ndogo, ni sawa na jitu lenye nguvu kama Samson wa biblia anasukuma katoroli kadogo. Kumbuka power ya gari sio mwonekano wa nje. Bali ni engine.
Kuweka powerful engine unamaanisha nini?
 
Kuweka powerful engine unamaanisha nini?
Gari inapotoka kiwandani, inakuwa na engine ya kiwandani. Lakini engine nyingine inaweza kuwekwa katika gari hiyo on the streets. Cha muhimu ni engine itoshe katika engine compartment, and in many cases compartments can handlr bigger engines. Kwa hio gari yenye 2000cc (4 cylinders) inaweza kuwekewa engine ya 3000cc (6 cylinders) au zaidi. In that case, itakuwa na power zaidi.
 
Back
Top Bottom