Toyota Premio inakimbia kuliko X- Trail new Model

Toyota Premio inakimbia kuliko X- Trail new Model

Jamaa yangu huyu alikuwa na Nissain Xtrail ile new model. Akanunua na Toyota Premio kwa ajili ya Mkewe. Anasema kwa Uzoefu wake baada ga kuzitumia zote kwa safari ndefu amegundua Toyotw Premio (model ya kati ) inakimbia zaidi kuliko Nissan Xtrail.

Nlijiuliza IS IT POSSIBLE? on what basis? Akasisitiza Premio imetulia zaidi pia kuliko Xtrail ukiwa mwendo mkali barabarani.

Je, kama ni kweli nini kinaweza kuwa sababu?
Njoo nkuuzie XTRAIL YANGU inakimbia kuliko zote hizo njoo ukague
IMG_20210310_115202_669.jpg
 
Umemuelewa mto mada ameongelea premio ya kipindi gani lakini? au unaleta ujuaji usio na maana, hicho unachokiongelea hakina maana hata kidogo na akikidhi criteria ya mtoa mada ameshasema premio hizi model za kati. Wewe hiyo ya 2017 umeowaona nao vijana gani wanazurula nazo hapa mjini? Sioni hata unachobisha na uwezi kunifundisha mie Engine Systems na zinavyofanya kazi kwa taarifa yako, ukitaka tujadili hili fungua uzi wako wa Engine Varieties na tutachangia na kukubomoa huko huko.
Nadhani hili wazo la uzi special kwa ajili ya engines ni wazo zuri mnoo tutajifunza mengi saana.. im interested. Fanya kuufungua Biohazard
 
9 and 3 ndio position salama
Uki assume steering wheel ni saa basi mikono iwe katika namba 3 na 9 hasa ukiwa highway. ILA kama uko mtaani kwenu unaweza hata usishike steering.
Nakubali kwa 100% mkuu,hata 10 2 position naona nayo ishakataliwa na wataalam.

Hio comment yako nimecheka sana maana najua huyo blaza hua anapenda kuonekana unique kwny vitu vyote so hawezi kubali kama anakosea kwny hilo,hahah.
 
Kijijini kwetu kama vile wanapishindana kila mtu ana premio.vitoto vidogo vina premio hadi kero hawajui huku mjini premio ni baby walker tu kama baby walker nyingine.

Nb gari zuri mjini muulize mtu ambae hana hata pikipiki.😀
 
Back
Top Bottom