Tozo mpya 17, mwendelezo wa maumivu kwa Mtanzania

Tozo mpya 17, mwendelezo wa maumivu kwa Mtanzania

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
54BB4A96-DA8B-47D6-8430-8D51A8294DBE.jpeg
 
Nitarudi ngoja nihudumie wagonjwa kwanza

Nimerudi sasa saa 2 asubuhi USSR

Nadhani wakati tunapata haya maumivu kwa hizi kodi ni vizuri tujiulize maumivu yetu yanasababishwa na nini haswa!?
1 Kwa sababu tunaonewa na kuchukiwa sana na serikali yetu?
2 Ni sababu hatuko tayari kwa mabadiliko kwa kile tulichozoea?
3 Au sisi ndio nchi ya pekee duniani kulipa hizi kodi? Na kama kwingine zipo wanalipa kiasi gani?

Cc BAK Deceiver SN.BARRY
 
"Upinzani umetuchelewa sana."

Sasa ndio mtajua faida ya uponzani dhidi ya wagonga meza...

Maumivu zaidi ni kwa walisaidia wizi wa kura 2020, Hadi maji utaita mma

Mkuu acha uongo,wana ccm wakitaka kupata huduma zote zinazohusiana na mambo ya tozo wanaonyesha tu kadi ya chama afu wanapewa discount.Kwa hio tozo haziwahusu kabisa mkuu.
 
2025 CCM imekwisha, waTanzania watapongezwa kwa kupata kiongozi mpya asiyetokana na CCM. Je ni sababu gani zitawafanya waTanzania kuchukua hatua hiyo:
  • Uchovu wa ndani ya CCM kufanya siasa kutokana na kutenda maovu, ugandamizi, kukamua wananchi kodi kupita kiasi huku viongozi wao wakijiongezea mishahara minono, magari ya kifahari ya kuwahudumia, majumba na marupurupu mengi. Mfano wa kuchoka ni gazeti la UHURU kuonesha kuchoka kutetea serikali ya CCM huku mhariri wake mkuu wa gazeti ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM MNEC. Kifupi CCM imeshindwa kufanya ushawishi kitu ambacho ndiyo msingi wa chama chochote cha siasa
  • Kila mtanzania akiangalia matendo ya CCM wanaona ni kama "eneo la jinai" yaani Crime scene mfano tozo za miamala, miradi ghofu ndege za Air Tanzania , SGR reli mpya, Stiegler's gorge, kesi za kubambikia, wafungwa wa kisiasa, matumizi mabaya ya vyombo vya usalama n.k
  • Makada na wanachama wa CCM waliopo serikalini wenye mamlaka yaani mawaziri, wakuu wa mikoa, RAS, maDC, DAS, DED wamekuwa watesi kwa waTanzania na siyo watumishi.
  • Wananchi kutambua kuwa hawana wawakilishi wao waliowachagua kupitia uchafuzi wa uchaguzi 2020 wa wabunge, madiwani, wenyeviti wa Mitaa na Vijiji. Hivyo kifupi hawana viongozi waliowachagua wao.
Kinachofuata ni kuwa 2025 wananchi wote bila kujali vyama vyao au itikadi hawatakichagua chama-ruhani cha CCM kwa kuwa CCM hakina tena vinasaba / DNA ya sifa za kuwa chama cha kisiasa.
 
Back
Top Bottom