Utatunguliwa yafuatayo:-
1. Custom Processing Fee = 0.6%
2. Railway Dev Levy = 1.5%, na
3. VAT = 18%.
Sasa assume simununua kwa TZS 500,000
0.6% ya TZS 500K = TZS 3000...... i
1.5% ya TZS 500K = TZS 7500..... ii
Now, thamani ya simu itayotakiwa kukatwa kodi ni 3000 + 7500 + 500,000 = 510,500
VAT 18% ya 510,500 = TZS 91,890 -- Hiyo ndo utawaachia TRA!
Itoshe tu kwamba, ukiagiza bidhaa kwa bei ya kukurupuka, halafu ukaingia kwenye mikono ya TRA, unaweza kujikuta unalipia bidhaa husika kwa pesa ya juu zaidi kuliko kama ungenunua TZ!