Unawekaje tozo ya shilingi 7,250/= kwenye mwamala wa elf 50......kimsingi kwa pesa ndogo kama hiyo jumla ya tozo haitakiwi kuzidi 700.....
Hii inaashiria serikali imekaukiwa vyanzo vya mapato kuendesha bajeti yake ambayo imelemewa na mzigo wa kulipa mishahara na posho nene nene kwa wateuliwa hasa ma-DC na ma-RC na kugharamia mashangingi yao, bila kusahau kutumia bajeti kubwa kuwalipa wagonga meza ambao hawajachaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi huru, hivyo kukosa tija yoyote kwenye kuwakilisha wananchi.
Yaani serikali inafanya matumizi ya anasa kuwazidi hata matajiri. Hivi kuna manufaa gani kumpa DC au RC vii eite, kwani wana value gani kiasi kwamba hawastahili kutumia landrover, land cruiser hardtop au hata corolla ambazo hata wafanyabiashara wanaweza kuwachangia mafuta wanapokuwa na ziara za kwenda kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo...
Badala ya kuwalipa wataalamu na kuwabana walete majibu ya changamoto za wananchi mnatumia pesa nyingi zaidi kuwalipa wateule, wanasiasa na viongozi na kugharamia magari yao ya anasa.....hivi mbali na awamu ya Nyerere nchi hii imewahi kuwa na viongozi serious tena? au ni mwendo wa kuchumia matumbo yao tu.....