Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

Hawa wapuuzi tu....wajifungie wapururane humo ndani hatutoi maoni wasubiri cha moto
 
"Hizi gharama mpya za mitandao ni dalili kuwa hatujuani hali zetu. Hayo makato sio mzigo kwa wenye uwezo bali kwa "wanyonge" ni mzigo mzito. Hakika matajiri na mali zao na maskini na watoto wao."- Dr. Stephen Munga

Tatizo sio kutolipa kodi tatizo kodi haziangalii hali za watu as if wote tunalipwa 12m kama wabunge.

Kodi zije kulingana na kipato cha mtu na huo unyonyaji kisa wao wana vipato vikubwa. Kwa wasifikiri kupunguza matumizi ya serikali kwanza?
Hakuna mwenye wazo la kupunguza gharama za matumizi ya serikali. Angalia misafara ya ma-V8 kati Dar na Dodoma, angalia misafara ya wakuu wa mikoa, RC mmoja aliehamishiwa Mwanza akiwa Tabora barabara zilikuwa zikifungwa kuepusha spite na msafara wa magari yake. Mkuu nae ni mwendo wa kupata kwenda kutuletea corona .
 
Unawekaje tozo ya shilingi 7,250/= kwenye mwamala wa elf 50......kimsingi kwa pesa ndogo kama hiyo jumla ya tozo haitakiwi kuzidi 700.....

Hii inaashiria serikali imekaukiwa vyanzo vya mapato kuendesha bajeti yake ambayo imelemewa na mzigo wa kulipa mishahara na posho nene nene kwa wateuliwa hasa ma-DC na ma-RC na kugharamia mashangingi yao, bila kusahau kutumia bajeti kubwa kuwalipa wagonga meza ambao hawajachaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi huru, hivyo kukosa tija yoyote kwenye kuwakilisha wananchi.

Yaani serikali inafanya matumizi ya anasa kuwazidi hata matajiri. Hivi kuna manufaa gani kumpa DC au RC vii eite, kwani wana value gani kiasi kwamba hawastahili kutumia landrover, land cruiser hardtop au hata corolla ambazo hata wafanyabiashara wanaweza kuwachangia mafuta wanapokuwa na ziara za kwenda kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo...

Badala ya kuwalipa wataalamu na kuwabana walete majibu ya changamoto za wananchi mnatumia pesa nyingi zaidi kuwalipa wateule, wanasiasa na viongozi na kugharamia magari yao ya anasa.....hivi mbali na awamu ya Nyerere nchi hii imewahi kuwa na viongozi serious tena? au ni mwendo wa kuchumia matumbo yao tu.....
Na V8 haizimwi ili AC ifanye kazi mteule asipate tabu.
 
Binafsi naunga na ninakubaliana na tozo mpya za miamala ya simu,Ni wajibu wangu Kama mtanzania kushiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yangu kwa kulipa Kodi halali zote zinazotozwa na serikali yangu.

Watanzania wenzangu tuiunge mkono serikali ya awamu ya sita kwa kulipa Kodi ili iweze kutuletea maendeleo chanya.

Hakuna nchi yoyote duniani imewahi kupata maendeleo bila ya Kodi,hata ughaibuni wanalipa Kodi.
Leo umenikumbush usemi wa kwenye msafara wa mamba na kenge wamo. Japo leo nashangaa kumwona mamba kwenye msafara wa kenge.
 
Safi tu,tujenge nchi yetu kupitia kodi zetu,hakuna njia tunayoweza kuinua uchumi wetu bila kujifunga mikanda,na mikanda yenyewe ndio hizi tozo,cha msingi maendeleo yaonekane kupitia kukamuliwa kodi hizi
Tatizo ni matumizi ya hizo kodi
Ghafla utasikia uwanja wa ndege unajengwa kijijini kwao pemba
 
CCM ni Chama dhalimu, hamuwezi kuwatwika mzigo mkubwa namna hii watu wa chini.
Pandisheni ushuru was sigara na pombe, Malaya walipe Kodi yaani kila starehe simika massive tax lakini sio kwenye vitu sensitive Kama mawasiliano
Sasa wao kwenye pombe ndiyo wanapunguza kabisa, Maana wanatengeneza wanywaji wengi,na wanapunguza watumiaji wa mobile Money
 
Waliweka VAT kwenye miamala tukavumilia,

Wameanzisha hizi tozo, naona wanatuchora tu. Eti maoni ili iwe nini?

Hapa kuna bilioni kadhaa zinatafutwa. Zikifika tukiwa wakaki wanaondoa hizi habari zao.
Na hizo bilioni zinazo tafutwa si kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, ni kwa manufaa ya wakubwa.
 
Hili jambo huenda wataalamu wa Wizara ya Fedha hawakupewa takwimu sahihi ya idadi ya miamala kwa siku toka kampuni za simu. Hivyo wakati wanaandaa charges ili kuweza kufikia makisio ya matarajio ya makusanyo ya tsh. 1.254tr (hiki ni kiasi tunategemea kukusanya kwenye tozo la miamala kwa mwaka) wakapigia idadi kwa miamala michache na ndio maana tozo ikawa kubwa.

Maoni yangu warudi kupata taarifa sahihi ya miamala ya makampuni iliyokuwa inafanywa kwa kampuni zote kwa siku. Maana kama miamala kwa siku ikifika miamala 2.7m wangeweza kucharge tsh 1254 kwa kila muamala na kuweza kufikia lengo la makusanyo 1.254tr( tsh 1254 kwa kila muamala x miamala 2.7m kwa siku x siku 365) hesabu hii ingetimiza lengo.
Na endapo idadi ya miamala iliyokuwa inafanywa itazidi 2.7m basi tozo inaweza kupungua hata kufikia tsh 500 kwa siku.

Tuwe Wakweli kwenye hili kuna mtu (Government)hakufanya homework yake vizuri. Au alikubali kutumia data alizopewa bila kuzitest kama zina ukweli.
Nilimuuliza wakala mmoja huku mtaani akaniambia hata wangeweka tsh 200 lengo lingetimia na yeye anafanya sehemu ambayo haijachamka kwa siku anafanya miamala 90 kwa siku. Bado wale anawawekea pesa wanafanya miamala ya kutuma kutoka hiyo miamala 90 inaweza kuzalisha miamala mingine 90 kwa wale wakioweka kuwatumia ndugu na jamaa na kuendelea
 
Na V8 haizimwi ili AC ifanye kazi mteule asipate tabu.
Vii eite lipo silencer mheshimiwa abaki kuwa comfortable, mkuu ni nini kifanyike serikali iachane na matumizi ya anasa ili pesa nyingi iende kwenye miradi na kuwalipa watumishi na wataalamu mishahara ya kuridhisha.......wafanyabiashara wanaoweza kumiliki na kuendesha vii eite ni wachache, lakini serikali inakusanya kodi kwa raia na wafanyabiashara kwenda kununua vii eite za watawala ambazo hata hao walipa kodi hawana. Matumizi ya serikali yanatakiwa yawe basic ili pesa nyingi iende kufanya mambo ambayo ni ya maslahi kwa walipa kodi, maji, elimu, afya, barabara, umeme, kilimo, mifugo, uvuvi, reli nk. Unapotumia asilimia 80 ya bajeti kuendesha serikali inayofanya anasa na kubakiza asilimia 20 ndo iende kwenye maendeleo hapa ndo uzumbukuku ulipo!
 
Na haya mambo ya kuitana waheshimiwa ndo yameleta balaa yote hii, serikali inahalalisha matumizi ya anasa kulinda hadhi ya cheo cha uheshimiwa. Mbona nchi zilizoendelea ni nadra sana kiongozi hata rais kuitwa mheshimiwa, wanawa address tu kwa majina yao hata kama ni profesa huwezi kusikia anaitwa Hon. Dr. Joe Biden, Hon. Dr. Barrack Obama, Hon. Prof. Bill Clinton. Hivi kwa nini tusijenge jamii ya usawa isiyo na kutukuza cheo au usomi wa mtu......
 
View attachment 1856216

Wadau, tutiririke hapa au mnaonaje?

Unaweza kusoma maoni ya wengine kupitia hii TAG on JF: tozo za miamala

Huu ujinga wa nini Waziri fedhuli na jeuri kabsa, mnapima upepo muone shemu ya kukazia, akili pumba kabsa kipindi cha Corona watu wanafanya utalamu kijinga sana, badala ya kutupa waiver nyie mnaibia raia. Badala ya relief fund mnaanzisha solidality fund? Mjivuni pumba kabsa Rais wenu anasema ana stemulate economy, sasa hivi majimbo yamepata 1.5bilion za Tarura, hivi hio akili matope, huku unaibia raia huku unakula kimdebwedo. Hii serikali akili za kiutopolo tu, wakati wa mdororo wa uchumi nyie ndio mnaiba. Huo ni uchimvi na ubofoaji.
 
Walitakiwa waje kabla sheria haijaanza. Kuja kuuliza maoni wakati watu wameshaumia ni unafiki
 
Dawa yenu inachemka subirieni dose October 2025
 
Vii eite lipo silencer mheshimiwa abaki kuwa comfortable, mkuu ni nini kifanyike serikali iachane na matumizi ya anasa ili pesa nyingi iende kwenye miradi na kuwalipa watumishi na wataalamu mishahara ya kuridhisha.......wafanyabiashara wanaoweza kumiliki na kuendesha vii eite ni wachache, lakini serikali inakusanya kodi kwa raia na wafanyabiashara kwenda kununua vii eite za watawala ambazo hata hao walipa kodi hawana. Matumizi ya serikali yanatakiwa yawe basic ili pesa nyingi iende kufanya mambo ambayo ni ya maslahi kwa walipa kodi, maji, elimu, afya, barabara, umeme, kilimo, mifugo, uvuvi, reli nk. Unapotumia asilimia 80 ya bajeti kuendesha serikali inayofanya anasa na kubakiza asilimia 20 ndo iende kwenye maendeleo hapa ndo uzumbukuku ulipo!
Njia sahihi kuyafikia maendeleo ni kuwa na bunge lenye meno, nalo huwezi lipata bila kuwa na katiba imara. Makusanyo ya kodi ni makubwa, japo yanaweza ongezeko vyanzo vingi vya mapato vikioanishwa. Tatizo lipo kwenye matumizi, ambapo wizi ni mkubwa, matumizi nje ya budget ni makubwa na hakuna mfumo wa udhibiti wa matumizi hayo.
 
Unawekaje tozo ya shilingi 7,250/= kwenye mwamala wa elf 50......kimsingi kwa pesa ndogo kama hiyo jumla ya tozo haitakiwi kuzidi 700.....

Hii inaashiria serikali imekaukiwa vyanzo vya mapato kuendesha bajeti yake ambayo imelemewa na mzigo wa kulipa mishahara na posho nene nene kwa wateuliwa hasa ma-DC na ma-RC na kugharamia mashangingi yao, bila kusahau kutumia bajeti kubwa kuwalipa wagonga meza ambao hawajachaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi huru, hivyo kukosa tija yoyote kwenye kuwakilisha wananchi.

Yaani serikali inafanya matumizi ya anasa kuwazidi hata matajiri. Hivi kuna manufaa gani kumpa DC au RC vii eite, kwani wana value gani kiasi kwamba hawastahili kutumia landrover, land cruiser hardtop au hata corolla ambazo hata wafanyabiashara wanaweza kuwachangia mafuta wanapokuwa na ziara za kwenda kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo...

Badala ya kuwalipa wataalamu na kuwabana walete majibu ya changamoto za wananchi mnatumia pesa nyingi zaidi kuwalipa wateule, wanasiasa na viongozi na kugharamia magari yao ya anasa.....hivi mbali na awamu ya Nyerere nchi hii imewahi kuwa na viongozi serious tena? au ni mwendo wa kuchumia matumbo yao tu.....
Viongozi wetu ni wavivu wa kufikiri na sio wabunifu kabisa,kifupi ni mazombi.
 
Back
Top Bottom