Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

CCM ni Chama dhalimu, hamuwezi kuwatwika mzigo mkubwa namna hii watu wa chini.
Pandisheni ushuru was sigara na pombe, Malaya walipe Kodi yaani kila starehe simika massive tax lakini sio kwenye vitu sensitive Kama mawasiliano
 
Kuhusu tozo za miamala ya simu mie bado nipo pamoja na mh. Raisi kwan amelazimika kutoka na hali halis aliyoikuta ya mtanguliz wake.

Tuvumilieni na tumpe matumaini na tumkosoe kwa staha kwakuwa yeye Ni binadam hataacha mapungufu ila sio matusi Kama wafavyo wahuni.

Haya mnayoyaona Sasa Ni matokeo ya mwendazake na lilikuwa Jambo la muda tu lazima yangetokea na nahis yangepita hapa.

Mama amekaa muda mchache ila ameleta matumaini makubwa kwa wananchi,tusimbeze badala yake tunpe muda tu hali itaimarika.
Nilimwelewa mama mwanzoni, aliupiga mwingi on target. Lakini sasa anaupiga mwingi off target.

Lazima tufungwe
 
Really !!!???, Kweli wanauliza Maoni ? Kwani wao Wanaonaje ?

Matusi yanaruhusiwa ?

TCRA ni Part of the Problem Bure Kabisa (Swali kwao, wao wanakula ngapi kutoka Tozo)?
 
Hii sawa sawa KESI ya nyani unampelekea NGEDERE
 
Safi tu,tujenge nchi yetu kupitia kodi zetu,hakuna njia tunayoweza kuinua uchumi wetu bila kujifunga mikanda,na mikanda yenyewe ndio hizi tozo,cha msingi maendeleo yaonekane kupitia kukamuliwa kodi hizi
 
Logic ni kuwa:

1. Wakati uchumi dunia nzima umeshuka sababu ya ugonjwa wa corona, baadhi ya nchi za wenzetu zimefikia hatua ya kuwapa watu wao pesa, au kuwapunguzia kodi, kwetu sisi haiwezekani ikawa ni busara kutwaa pesa zaidi za wananchi kipindi hiki ambacho uchumi ni mgumu zaidi

2. Kuna kodi nyingi sana zipo tayari kwenye miamala ya kwenye mitandao, kuna VAT tayari iko pale, kuna kodi ya kuchaji laini kila ukiweka hela, kuna kodi ya kutuma kuna kodi ya kutoa- Hizi ni Multiple taxations kwenye huduma ambazo basically ni kwa huduma zinazoshabihiana, hupaswi kuendelea kuongeza makato katika makato ambayo tayari yapo, kufanya hivyo ni too much

3. Kuongeza makato kwenye huduma ambayo ni ya msingi kwa wananchi ni kutaka wananchi warudi katika ugumu wa maisha wa zamani wakati tayari kuna unafuu wa maisha waliokwisha upata kwenye kufanya shughuli zao za kiuchumi. Maendeleo siyo tu kujenga mabarabara na mashule tu, Maendeleo ni pamoja na wepesi wa kurahisisha maisha ya wananchi. Sasa hata hilo serikali inataka kuitwaa?

4. Hatua ya kuongeza hizi kodi itaua ajira za watu kibao kwa sababu wananchi watapunguza kutumia huduma hizi za miamala kutumia kampuni za simu, wale mawakala wataanza kukosa pesa

5. Haya makato yanazidi kuyatajirisha makampuni ya Simu kwa pesa za burebure kutoka kwa wananchi,maana pale serikali inapoongeza makato haya ili ipate hela nyingi, basi na makampuni hayo nayo pia yanatumia opportunity hiyo nayo kuongeza pesa yanayochukua kwenye miamala hiyo. Yaani Just imagine sasa hivi makampuni ya simu yanakaribia kuchukua pasu kwa pasu na serikali katika kile yanachomkamua mwananchi. Sasa kwa nini sisi wananchi tuwe ng'ombe wa kukamua kuzidi kutajirisha haya makampuni

6. Haya makato kiufupi yataua uchumi mdogomdogo uliokuwa uliokuwa umejiambatanisha na huduma hizi za miamala kupitia simu. Sasa kodi yenye kuua uchumi mdogo kwa ajili eti ya kujenga uchumi mkubwa ni kodi ya ajabu kwa sababu uchumi mdogomdogo ndiyo unagusa wananchi wengi ambao wanategemea kutafuta hela ya kula on a daily basis

7. Serikali iione hizi huduma kama aid to trade kusaidia wananchi na siyo source ya kutegemea kwa ajili ya kodi
 
Logic ni kuwa:

1. Wakati uchumi dunia nzima umeshuka sababu ya ugonjwa wa corona, baadhi ya nchi za wenzetu zimefikia hatua ya kuwapa watu wao pesa, au kuwapunguzia kodi, kwetu sisi haiwezekani ikawa ni busara kutwaa pesa zaidi za wananchi kipindi hiki ambacho uchumi ni mgumu zaidi

2. Kuna kodi nyingi sana zipo tayari kwenye miamala ya kwenye mitandao, kuna VAT tayari iko pale, kuna kodi ya kuchaji laini kila ukiweka hela, kuna kodi ya kutuma kuna kodi ya kutoa- Hizi ni Multiple taxations kwenye huduma ambazo basically ni kwa huduma zinazoshabihiana, hupaswi kuendelea kuongeza makato katika makato ambayo tayari yapo, kufanya hivyo ni too much

3. Kuongeza makato kwenye huduma ambayo ni ya msingi kwa wananchi ni kutaka wananchi warudi katika ugumu wa maisha wa zamani wakati tayari kuna unafuu wa maisha waliokwisha upata kwenye kufanya shughuli zao za kiuchumi. Maendeleo siyo tu kujenga mabarabara na mashule tu, Maendeleo ni pamoja na wepesi wa kurahisisha maisha ya wananchi. Sasa hata hilo serikali inataka kuitwaa?

4. Hatua ya kuongeza hizi kodi itaua ajira za watu kibao kwa sababu wananchi watapunguza kutumia huduma hizi za miamala kutumia kampuni za simu, wale mawakala wataanza kukosa pesa

5. Haya makato yanazidi kuyatajirisha makampuni ya Simu kwa pesa za burebure kutoka kwa wananchi,maana pale serikali inapoongeza makato haya ili ipate hela nyingi, basi na makampuni hayo nayo pia yanatumia opportunity hiyo nayo kuongeza pesa yanayochukua kwenye miamala hiyo. Yaani Just imagine sasa hivi makampuni ya simu yanakaribia kuchukua pasu kwa pasu na serikali katika kile yanachomkamua mwananchi. Sasa kwa nini sisi wananchi tuwe ng'ombe wa kukamua kuzidi kutajirisha haya makampuni

6. Haya makato kiufupi yataua uchumi mdogomdogo uliokuwa uliokuwa umejiambatanisha na huduma hizi za miamala kupitia simu. Sasa kodi yenye kuua uchumi mdogo kwa ajili eti ya kujenga uchumi mkubwa ni kodi ya ajabu kwa sababu uchumi mdogomdogo ndiyo unagusa wananchi wengi ambao wanategemea kuta hela ya kula on a daily basis

7. Serikali iione hizi huduma kama aid to trade kusaidia wananchi na siyo source ya kutegemea kwa ajili ya kodi
Kodi hizi zipungizwe by 50% bado serikali itapata fedha za kutosha kutokana na turnover kubwa itakayosababishwa na wananchi kuendelea kutumia online transactions kwa idadi kubwa.
 
"Hizi gharama mpya za mitandao ni dalili kuwa hatujuani hali zetu. Hayo makato sio mzigo kwa wenye uwezo bali kwa "wanyonge" ni mzigo mzito. Hakika matajiri na mali zao na maskini na watoto wao."- Dr. Stephen Munga

TATIZO SIO KUTOLIPA KODI TATIZO KODI HAZIANGALII HALI ZA WATU AS IF WOTE TUNALIPWA 12M KAMA WABUNGE.

KODI ZIJE KULINGANA NA KIPATO CHA MTU NA HUO UNYONYAJI KISA WAO WANA VIPATO VIKUBWA. KWA WASIFIKIRI KUPUNGUZA MATUMIZI YA SERIKALI KWANZA.???
Kuna haja ya wabunge kulipwa 3M kwa mwezi na posho ya 100,000 kwa siku ili waweze kuona hali ya maisha jinsi ilivyo mtaani! Bila kuwa taste of their own flesh wataendelea kutufanya sie mandezi tu miaka yote!

Mbunge kulipwa 12M ni excessive na anasa! Kama raia wote tungekuwa na access ya hio hela hata makato yangekuwa elf 20 kwa kila muamala hamna mtu angelalamika!
 
Ushauri wangu

Binafsi naunga na ninakubaliana na tozo mpya za miamala ya simu,Ni wajibu wangu Kama mtanzania kushiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yangu kwa kulipa Kodi halali zote zinazotozwa na serikali yangu.

Watanzania wenzangu tuiunge mkono serikali ya awamu ya sita kwa kulipa Kodi ili iweze kutuletea maendeleo chanya.

Hakuna nchi yoyote duniani imewahi kupata maendeleo bila ya Kodi,hata ughaibuni wanalipa Kodi.
 
Ni ushenzi kuachia matumizi mabaya ya pesa na wizi halafu ukamue wananchi wako mwenyewe ...ila siyo mbaya watakipata wanachokitafuta ingawaje WaTz hawana la kufanya zaidi ya kulia na miti
 
Maoni

Tozo mpya za Serikali katila miamalq tunayofanya zipo juu sana tofaut na hali ya kifedha ya wananchi tulio wengi, Namaanisha ya kwamba tozo katika MIAMALA haziendani na vipato vyetu sisi raia wazalendo,

Nafahamu serikali yetu ina lengo zuri la KUKUSANYA MAPATO & KUKUZA SEKTA YA FEDHA kwenye Upande wa BANKING, lakini Tozo hizi kimsingi zitaleta mkwamo katika Majambo hayo mawili hapo

Hivyo Serikali yetu nadhani iangalie uwezekano wa KUPUNGUZA hizi Tozo za kizalendo katika miamala tunayofanya,
Kusudi serikali ifanikishe hayo Majambo mawili kwa pamoja laasivyo huo mkwamo utaturudisha Nyuma kama taifa

( Reduction ya Nusu na robo katika kila TOZO itafaa sana kwa sisi wananchi kuchangia maendeleo )

Samahan kwa uandishi wa hovyo
 
Kuhusu tozo za miamala ya simu mie bado nipo pamoja na mh. Raisi kwan amelazimika kutoka na hali halis aliyoikuta ya mtanguliz wake.

Tuvumilieni na tumpe matumaini na tumkosoe kwa staha kwakuwa yeye Ni binadam hataacha mapungufu ila sio matusi Kama wafavyo wahuni.

Haya mnayoyaona Sasa Ni matokeo ya mwendazake na lilikuwa Jambo la muda tu lazima yangetokea na nahis yangepita hapa.

Mama amekaa muda mchache ila ameleta matumaini makubwa kwa wananchi,tusimbeze badala yake tunpe muda tu hali itaimarika.
Hapa ndipo napata ukakasi, "....kutokana na hali aliyoikuta....", una taarifa zozote za hali aliyoikuta? Ipi? Yeye amezungumzia lengo la kuongeza hizo tozo ni barabara na maji ambayo kimsingi huyo aliyemtangulia alikuwa akifanya tu bila kuongeza tozo huku chini bali juu.

Mkwere alichukua nchi ikiwq imefutiwa madeni(mwaka 2000) na haikuwa na pesa pia, Mkapa pia hakukuta pesa kwa mujibu wa taarifa za wakati huo, waliunganisha mikoa yote kwa barabara n.k

Tunaelewa zaidi ya tunachoambiwa, tunazungumza tusichokuwa na hakika nacho.
 
Wakate kwa% na isizidi 1% ya hela unayotuma so ka.a.utatuma laki wanakata 1000 kidogo afadhali sio.kwa makato ya sasa
 
Back
Top Bottom