Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

Waliweka VAT kwenye miamala tukavumilia,

Wameanzisha hizi tozo, naona wanatuchora tu. Eti maoni ili iwe nini?

Hapa kuna bilioni kadhaa zinatafutwa. Zikifika tukiwa wakaki wanaondoa hizi habari zao.
 
Binafsi naunga na ninakubaliana na tozo mpya za miamala ya simu,Ni wajibu wangu Kama mtanzania kushiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yangu kwa kulipa Kodi halali zote zinazotozwa na serikali yangu...
Mkuu wewe ni kada wa ccm, unadhani una utashi wa kukataa hata kama akilini mwako unajua kabisa sio sahihi?
 
Hao TCRA Wana serikali yao labda.Walivyokuwepo wapumbavu kwamba wanategemea kuna mtu atasema anafurahia kulipa kodi?

Nani kawatuma kufanya huu upuuzi wao?
 
Leo kuna jamaa nimemsikia alitaka kutumiwa 20000 anayodai mtumaji akataka amkate na ya kutumia , jamaa akasema nitaifata nauli ni 500 kwenda mia 500 kurudi makato ni 4000 kutuma na kutoa
 
Acheni kumlaumu mwendazake ,kama mumekosa ubunifu na uthubutu semeni tu, mwendazake kafanya mengi bila kuleta athari za kodi kwa mtu wa kawaida, katika miaka mitano alijifunga kibwebwe baada ya kukuta jungu kuu halina kitu hakusubiri kulialia na kumlalamikia mtangulizi wake, yeye alipata kodi kwa kuziba mianya ya wizi kama vile malipo ya Tanesco kwa makampuni hewa, kuwakaliaa kooni wachimbaji madini wakubwa, kuzuia safari na vikao visivyo vya lazima,

kwa kkfupi alibana matumizi, sasa siku 100 tu watu wameanza kulia kila kukichwa ni kumkamua ng'ombe maziwa ambaye hana hata malisho. Juzi nimemsikia Mzee Warioba akisma serikali ipunguze matumizi kwa viongozi wake, siku hizi misururu imerudi tena, kila siku makongamano, kila siku watu wanakwea pipa.

Matumizi na mapato haviendani, mara watu wapelekwa wakaona wanyama,mara wakaone sijui nini. RIP mwendazake, ulisema tutakukumbuka na kweli tumeanza kukumbuka hata mwaka haujapita.
 
Yaani wanamuuliza marehemu anajisikiaje kufa?Au angependelea afe kwa namna gani wakati ameshakufa?TCRA is the bunch of hooligans![emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
Asking dying experience from the dead![emoji2815][emoji2815][emoji2815][emoji2815][emoji848][emoji848][emoji2984][emoji2984][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Mkuu wewe ni kada wa ccm, unadhani una utashi wa kukataa hata kama akilini mwako unajua kabisa sio sahihi?
Mkuu hili nalikubali si tu sababu ya Mimi kuwa member wa CCM bali Ni kutokana na uzalendo Niko nao katika kulipa Kodi ambayo baadae inaleta maendeleo kwa taifa letu.

Kwa maoni yangu hii Kodi tunayokatwa kwa miamala ya simu Ni ndogo,naomba iwe maradufu
 
CCM inaenda kufa labda tu kwakuwa wameshika mpini
 
Waziri kasema hawezi kubadiri tena nasisi tunasema tutawabadirisha wao personaly.
Kilicho fanywa na serikali hakina tofauti na mfugaji aliekuwa na kuku anamtagia yai la dhahabu kila siku. Mfugaji alimchinja kuku akitumaini kupata mayai mengi kwa wakati mmoja. Mambo ya uchumi yana taratibu zake, ukiyapeleka kipolisi utakwama.
 
CCM waliiba kura ili wawe na bunge linaloonea wanaowaita wanyonge.
Hao wanataka watu watoe maoni halafu...
Wao ni ccm ha ccm ni wao ni sawa na mtu umefungwa kwa kutokuwa na kosa halafu aliyekufunga anakuja gerezani anakuuliza 'kwani unajisikiaje sasa?!' seriously!
 
kwa namna hii itakuwa ni vigumu sana kuwa na huduma za kifedha Jumuishi,Ni hatua iliyoletwa na ubinafsi na kushindwa kujua kwamba mpango wa fedha jumuishi ulilenga nini, Mpango huu ulilenga kuwajumuisha watu wa kada mbalimbali zikiwemo kaya maskini wale wanaopata Pesa za kaya maskini yaani TASAF,Hivyo Mpango huu ulilenga hawa kaya maskiniwawekewe fedha kwenye simu zao,ili kuwapungua gharama za kuzifuatilia pia na usalama wa fedha.Na wananchi wengi walishajisajili na kupata namba zao za NIDA.Ni mwananchi yupi wa kaya maskini atakayehitaji kuwekewa tena kwenye simu,je usalama wa hao wakaotembea na hizo fedha kwenda kulipa utalindwaje, kulingana na na hali ya sasa ya kiuchumi,je wanajua watu wenye miamala mikubwa ya pesa wana options nyingi, kuliko wenye miamala midogo.Je wametofautisha kati ya mzunguko wa fedha na kiasi cha fedha??UKIWA NA BUNGE LENYE KUPITISHA VITU KAMA HIVI BILA KUFANYA MAREJEO NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA
View attachment 1857058
 
Hapo unajidanganya, usitarajie matokeo ya kubashiri. The means determine the end.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…