Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya kutuma na kutoa Fedha na kupunguza viwango vya tozo kwa 30%
Pia Serikali imejadiliana na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%
Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi Septemba 01, 2021
Kwahio Punguzo hilo, litakuwa ni Ongezeko la Asilimia ngapi kutoka tulipokuwepo Awali....
Hii inanikumbusha story ya ukitaka kumchemsha chura ongeza moto kidogo kidogo..., ila huenda hapa ni kuweka moto mkali kuliko ili ukipunguza kidogo mtu aone ahueni ila kumbe bado ni moto mkali
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 31, 2021 ametia saini mabadiliko ya tozo za miamala ambapo serikali imepunguza 30% na makampuni ya simu Kupunguza 10% kutoka kwenye gharama za awali za ufanyaji wa miamala.