Sisi tulikua hatuzitaki kabisa hizo TOZO
"SISI" ni akina nani nyie mliokuwa hamzitaki kabisa hizo TOZO? Wala tusihangaike kutafuta majibu mbali - ninyi ni wapinga maendeleo mliozoea DEZO katika maisha yenu! Mimi nawafananisha nyie na TOBO na huyo mwingine aliyeko Kanada ambako wanakaa na kulishwa tu kama MALKIA WA NYUKI. Si mnajua kazi ya Malikia wa Nyuki na nini huwa kinamtokea meishoni!? DEZO ni utumwa in disquise jamani!
 
Sisi tulikua hatuzitaki kabisa hizo TOZO

Hb za asubuhi wananchi wa kiharaka na waishio nje ya kiharaka tunamshukuru mkuu wa kituo cha jeshi cha MAPINGA CTC kwa msaa wa kuchangia mifuko 20 ya cement kwa ajili ya ujenzi wa madarasa vyumba viwili na ofisi ya walimu moja ujenzi huu utakuwa nguvu za wananchi niwaombe wanachi wenzangu tujitoe kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi huu kuanzia sasa tunapokea mchanga,cement,tofari na nondo ili tufanikishe hili na jumamosi tutakuwa na harambee ya kuchimba msingi wa madarasa hayo naomba kuwasilisha.🙏🏿🙏🏿

My take: Wewe hutaki kutoa kodi kwa maendeleo ya watoto hawa, Mwenzako kachangia toka mfukoni mwake mifuko 20 ya cementi (15 *15000sh =225000 sh). Huyu daima ataipongeza kodi hiyo, kwa sababu Brigedia wa kesho ndio atatoka katika shule hiyo. Nami namuunga mkono na niko tayari kuchangia kwa maendeleo ya watoto wetu. Sisi hata kabla ya kodi ni wachangiaji wazuri wa maeneo ya Elimu na Afya. Kumbuka shule hiyo hatasoma mtoto wa Samia wala wa Mwigulu bali ni wa kwako na wa kwangu.
 
Hapana. Tozo zifutwe kabisa. Huu ni unyang'anyi. "Double taxation: On capital employed and on profit realized".
 
Hahaha elimu ni tatizo hufahamu kuna kitu kinaitwa kanuni? Ndio maana kuongoza watanzania ni kazi watu hamjisomei unakariri tu, waziri apo kabadilisha kanuni
Kwa hiyo hapa alikuwa anadnganya umma?
 
Mkuu una akili timamu?
 
Rais Mkapa the best tz president though alikuwa mbabe kwa wapinzani haswa Wapemba. Aliziondoa kodi zote za kijinga na kuziita zenye "maudhi" na raia tukaanza kuona raha kuzaliwa tz. Ina maana za Mkapa zilikuwa hazijapitishwa na bunge?
 
Ndio na nyie mlipe kodi kwa income zenu hizo.Hii kodi uwe mfanyakazi au mkulima ni unalipa.

Wafanyakazi wanakatwa kwa sababu ni rahisi kuwakata sio nyie mnaokwepa kodi
Huna unalojua, subirini tu muda wenu utafika kuni ziwawakie....
 
Hakika Serikali ya Awamu ya Sita ina uongozi sikivu na madhubiti wenye kujali wananchi wake kwa kuhakikisha huduma za kijamii na miundombinu safi inapatikana.

Katika kufanikisha hilo serikali mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilileta tozo katika miamala ya simu na kukusanya Bilioni 63 hadi sasa zinazoelekezwa katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Baada ya kuanza kwa tozo hizo wananchi walikuwa na mapokeo tofauti, lakini kutokana na imani yao kwa serikali wakapaza sauti kuiomba serikali kupunguza viwango vya makato ya tozo ili kuwapa wepesi wa gharama za maisha.

Ni dhahiri Rais wetu mzalendo na mpenda maendeleo mwenye moyo wa mama alilipokea na kuunda kamati iliyofanyia kazi maombi ya wananchi. Na sasa kazi nzuri iliyofanywa na kamati hatimaye imezaa matunda na kuleta faraja kwa wananchi.

Vifijo na nderemo vimetawala kila kona ya nchi wakifurahia kupunguzwa kwa viwango vya tozo. Wananchi wanatarajia maendeleo ya huduma nzuri na miundombinu safi inatakayotekelezwa kutokana na makato ya tozo hizo.

Hongera sana Mama la Mama #SamiaSuluhuHassan
 
Ni kweli unaamini haya au unajitoa ufahamu ?
 
Hopeless
 
Kwani hizo TOZO zilianzishwa na nani?
 
Biashara ya watumwa ingekuwepo hadi leo, Maccm yote tungeyatoa hata bure tu.
 
ni lini mtaanza kuwa na akili
miezi miwili iliyopita alisema mama Samia ametoa millioni 100 kwenye mshahara wake wa urais soko la kariakoo lijengwe mbona mpaka sasa hamna hata dalili ya kulijenga?
 
Nilidhani serikali sikivu Ingeiondoa kabisa au hata kama hawezekani kuiondoa basi angalau ingetukata 30 asilimia tu.

Hata hivyo tumemkosa mtu wa kututetea baada ya wabunge kuungana na serikali kwenye hili.
 
Rais Mkapa the best tz president though alikuwa mbabe kwa wapinzani haswa Wapemba. Aliziondoa kodi zote za kijinga na kuziita zenye "maudhi" na raia tukaanza kuona raha kuzaliwa tz. Ina maana za Mkapa zilikuwa hazijapitishwa na bunge?

Aliziondoaje? Kwa kutoa tamko tu au kwa kufuata process ya kisheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…