Tozo za Miamala: Serikali yapunguza viwango kwa 30%. Watoa huduma za simu waridhia kupunguza 10%
Sisi tulikua hatuzitaki kabisa hizo TOZO
"SISI" ni akina nani nyie mliokuwa hamzitaki kabisa hizo TOZO? Wala tusihangaike kutafuta majibu mbali - ninyi ni wapinga maendeleo mliozoea DEZO katika maisha yenu! Mimi nawafananisha nyie na TOBO na huyo mwingine aliyeko Kanada ambako wanakaa na kulishwa tu kama MALKIA WA NYUKI. Si mnajua kazi ya Malikia wa Nyuki na nini huwa kinamtokea meishoni!? DEZO ni utumwa in disquise jamani!
 
Sisi tulikua hatuzitaki kabisa hizo TOZO
1630490477735.jpeg

Hb za asubuhi wananchi wa kiharaka na waishio nje ya kiharaka tunamshukuru mkuu wa kituo cha jeshi cha MAPINGA CTC kwa msaa wa kuchangia mifuko 20 ya cement kwa ajili ya ujenzi wa madarasa vyumba viwili na ofisi ya walimu moja ujenzi huu utakuwa nguvu za wananchi niwaombe wanachi wenzangu tujitoe kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi huu kuanzia sasa tunapokea mchanga,cement,tofari na nondo ili tufanikishe hili na jumamosi tutakuwa na harambee ya kuchimba msingi wa madarasa hayo naomba kuwasilisha.🙏🏿🙏🏿

My take: Wewe hutaki kutoa kodi kwa maendeleo ya watoto hawa, Mwenzako kachangia toka mfukoni mwake mifuko 20 ya cementi (15 *15000sh =225000 sh). Huyu daima ataipongeza kodi hiyo, kwa sababu Brigedia wa kesho ndio atatoka katika shule hiyo. Nami namuunga mkono na niko tayari kuchangia kwa maendeleo ya watoto wetu. Sisi hata kabla ya kodi ni wachangiaji wazuri wa maeneo ya Elimu na Afya. Kumbuka shule hiyo hatasoma mtoto wa Samia wala wa Mwigulu bali ni wa kwako na wa kwangu.
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya kutuma na kutoa Fedha na kupunguza viwango vya tozo kwa 30%

Pia Serikali imejadiliana na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%

Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi Septemba 01, 2021

Taarifa Kamili:

Hapana. Tozo zifutwe kabisa. Huu ni unyang'anyi. "Double taxation: On capital employed and on profit realized".
 
Hahaha elimu ni tatizo hufahamu kuna kitu kinaitwa kanuni? Ndio maana kuongoza watanzania ni kazi watu hamjisomei unakariri tu, waziri apo kabadilisha kanuni
Kwa hiyo hapa alikuwa anadnganya umma?
 
MAMBO MATATU ALIYOYAFANYA RAIS SAMIA KWENYE TOZO ZA E-MONEY,
___________________________


1. Kupunguza tozo za miamala ( e-money) kwa 30%

2. Kushawishi makampuni ya e-money na wao kushusha makato yao kwa 10%,

3. Kuendelea kuwa msikivu kwa kushughulikia kero za wananchi kwa haraka,

NB, Hili punguzo linamaana gani ?!

Katika kila shilingi tuliyokatwa awali ni senti 60 tu ndio itachukuliwa na mwanachi Mama amemrudishia|amembakishia senti 40 katika kila muamala anaofanya,

Kama awali ulikatwa Tshs 10,000 Leo utakatwa Tshs 6,000 tu huku Tshs 4,000 Mama akiirudisha|akiibakisha kwako.


...Kazi iendelee | Mama ni habari nyingine ...View attachment 1919029
Mkuu una akili timamu?
 
Kwa hiyo aliposema kuwa yeye kama waziri hana uwezo wa kuzibadilisha tozo kwa vile zimepitishwa na Bunge alikuwa anadanganya umma?

Rais Mkapa the best tz president though alikuwa mbabe kwa wapinzani haswa Wapemba. Aliziondoa kodi zote za kijinga na kuziita zenye "maudhi" na raia tukaanza kuona raha kuzaliwa tz. Ina maana za Mkapa zilikuwa hazijapitishwa na bunge?
 
Ndio na nyie mlipe kodi kwa income zenu hizo.Hii kodi uwe mfanyakazi au mkulima ni unalipa.

Wafanyakazi wanakatwa kwa sababu ni rahisi kuwakata sio nyie mnaokwepa kodi
Huna unalojua, subirini tu muda wenu utafika kuni ziwawakie....
 
Hakika Serikali ya Awamu ya Sita ina uongozi sikivu na madhubiti wenye kujali wananchi wake kwa kuhakikisha huduma za kijamii na miundombinu safi inapatikana.

Katika kufanikisha hilo serikali mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilileta tozo katika miamala ya simu na kukusanya Bilioni 63 hadi sasa zinazoelekezwa katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Baada ya kuanza kwa tozo hizo wananchi walikuwa na mapokeo tofauti, lakini kutokana na imani yao kwa serikali wakapaza sauti kuiomba serikali kupunguza viwango vya makato ya tozo ili kuwapa wepesi wa gharama za maisha.

Ni dhahiri Rais wetu mzalendo na mpenda maendeleo mwenye moyo wa mama alilipokea na kuunda kamati iliyofanyia kazi maombi ya wananchi. Na sasa kazi nzuri iliyofanywa na kamati hatimaye imezaa matunda na kuleta faraja kwa wananchi.

Vifijo na nderemo vimetawala kila kona ya nchi wakifurahia kupunguzwa kwa viwango vya tozo. Wananchi wanatarajia maendeleo ya huduma nzuri na miundombinu safi inatakayotekelezwa kutokana na makato ya tozo hizo.

Hongera sana Mama la Mama #SamiaSuluhuHassan
 
Ni kweli unaamini haya au unajitoa ufahamu ?
 
TOZO ZA MIAMALA RAFIKI KWA WANANCHI

Hakika Serikali ya Awamu ya Sita ina uongozi sikivu na madhubiti wenye kujali wananchi wake kwa kuhakikisha huduma za kijamii na miundombinu safi inapatikana.

Katika kufanikisha hilo serikali mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilileta tozo katika miamala ya simu nankukusanya Bilioni 63 hadi sasa zinazoelekezwa katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Baada ya kuanza kwa tozo hizo wananchi walikuwa na mapokeo tofauti, lakini kutokana na imani yao kwa serikali wakapaza sauti kuiomba serikali kupunguza viwango vya makato ya tozo ili kuwapa wepesi wa gharama za maisha.

Ni dhahiri Rais wetu mzalendo na mpenda maendeleo mwenye moyo wa mama alilipokea na kuunda kamati iliyofanyia kazi maombi ya wananchi. Na sasa kazi nzuri iliyofanywa na kamati hatimaye imezaa matunda na kuleta faraja kwa wananchi.

Vifijo na nderemo vimetawala kila kona ya nchi wakifurahia kupunguzwa kwa viwango vya tozo. Wnanchi wanatarajia maendeleo ya huduma nzuri na miundombinu safi inatakayotekelezwa kutokana na makato ya tozo hizo.

Hongera sana Mama la Mama #SamiaSuluhuHassan
Hopeless
 
Hakika serikali ya awamu ya sita ina uongozi sikivu na madhubiti wenye kujali wananchi wake kwa kuhakikisha huduma za kijamii na miundombinu safi za kutolia huduma zinakuwepo.

Katika kufanikisha hilo serikali mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2021/2022 ileta tozo katika miamala ya simu ilikukusanya pesa ya kutekeleza miradi hiyo ili kufanikisha azma yake.

Baada ya kuanza kwa tozo hizo wananchi walikuwa na mapokeo tofauti, lakini kutokana na imani ya wananchi kwa serikali wakapaza sauti kuiomba serikali kupunguza viwango vya makato ya tozo, ili kuwapa wepesi wa gharama za maisha.

Nidhahiri Rais wetu Mzalendo mpenda maendeleo alilipokea na kuunda kamati iliyofanyia kazi maombi ya wananchi na sasa kazi nzuri iliyofanywa na kamati hatimaye imezaa matunda na kuleta faraja kwa wananchi.

Vifijo na ndelemo vimetawala kila kona ya nchi wakifurahia kupunguzwa kwa viwango vya tozo wananchi wanatarajia maendeleo na huduma nzuri na miundombi inatakayotekelezwa kutokana na makato ya tozo hizo.
Kwani hizo TOZO zilianzishwa na nani?
 
Biashara ya watumwa ingekuwepo hadi leo, Maccm yote tungeyatoa hata bure tu.
 
ni lini mtaanza kuwa na akili
miezi miwili iliyopita alisema mama Samia ametoa millioni 100 kwenye mshahara wake wa urais soko la kariakoo lijengwe mbona mpaka sasa hamna hata dalili ya kulijenga?
 
Nilidhani serikali sikivu Ingeiondoa kabisa au hata kama hawezekani kuiondoa basi angalau ingetukata 30 asilimia tu.

Hata hivyo tumemkosa mtu wa kututetea baada ya wabunge kuungana na serikali kwenye hili.
 
Rais Mkapa the best tz president though alikuwa mbabe kwa wapinzani haswa Wapemba. Aliziondoa kodi zote za kijinga na kuziita zenye "maudhi" na raia tukaanza kuona raha kuzaliwa tz. Ina maana za Mkapa zilikuwa hazijapitishwa na bunge?

Aliziondoaje? Kwa kutoa tamko tu au kwa kufuata process ya kisheria?
 
Back
Top Bottom