Tozo za Miamala: Serikali yapunguza viwango kwa 30%. Watoa huduma za simu waridhia kupunguza 10%
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba tozo zilikuwepo tokea awali kabla ya ubunifu wa comrade zungu? au unataka kutuingiza chaka.....
Tozo kwenye miamala siongelei kwenye talktime (ingawa hata huko tozo ilikuwepo kama kodi) kwenye miamala kulikuwa na kodi lukuki kabla ambazo bado zipo, kodi ya zuio, vat n.k. (kubadilisha majina tuzo, kodi, n.k.) haibadilishi kwamba huo ni utozaji
 
Walio enda burundi warudi sasa yumbani kumenoga
 
Acha kupigia debe mambo yanayowauumiza wananchi, huyu mama kashafeli mapema kuwaongezea tozo watu maskini akati nchi ina madini ya kutosha, tuna viongozi mizigo sana nchi hii
 
Kumtumia bibi yako pesa kijijini hapo unakuwa umefanya biashara gani na umetengeneza faida kiasi gani ili ukatwe kodi. Kimsingi makampuni ya simu ndo yanayofanya biashara kwenye hizi transactions maana wanakata kiasi cha pesa. Sasa hii kodi tunayokatwa na serikali ambayo imebatizwa jina la tozo mantiki yake ni ipi hasa......waache kulaghai watu kwa ujanja ujanja, eti tumepunguza tozo kwa 30%...
 
Uzi kama huu unashushaa hadhi ya mtu na kuonesha jinsi uwezo wa kudadavua mambo ulivyo chini ya kiwango.

Ukosee afu useme umekuwa msikivu badala ya kuomba msamaha?.

Mama atuombe msamaha haraka sana.

La sivyo 2025 chama kitakuwa na hari ngumu mno.
 
Mwendo wa Rais Samia analeta Raha sana,

MAMA GO GO GO TUNAKUOMBEA
 
MAMBO MATATU ALIYOYAFANYA RAIS SAMIA KWENYE TOZO ZA E-MONEY,
___________________________

1. Kupunguza tozo za miamala ( e-money) kwa 30%

2. Kushawishi makampuni ya e-money na wao kushusha makato yao kwa 10%,

3. Kuendelea kuwa msikivu kwa kushughulikia kero za wananchi kwa haraka,

NB, Hili punguzo linamaana gani ?!

Katika kila shilingi tuliyokatwa awali ni senti 60 tu ndio itachukuliwa na mwanachi Mama amemrudishia|amembakishia senti 40 katika kila muamala anaofanya,

Kama awali ulikatwa Tshs 10,000 Leo utakatwa Tshs 6,000 tu huku Tshs 4,000 Mama akiirudisha|akiibakisha kwako.

...Kazi iendelee | Mama ni habari nyingine ...View attachment 1919029
Ndo ujinga niusemao huu... HIVI KWANI ALIYEPANDISHA NI NANI HADI IONEKANE ANAYESHUSHA NI MSIKIVU..!?
 
sisi hatutaki tozo kbs... madini yetu yameenda wapi hadi wananchi wanyonge tukatwe kodi.. tuliambiwa Nchi tajiri
 
MAMBO MATATU ALIYOYAFANYA RAIS SAMIA KWENYE TOZO ZA E-MONEY,
___________________________

1. Kupunguza tozo za miamala ( e-money) kwa 30%

2. Kushawishi makampuni ya e-money na wao kushusha makato yao kwa 10%,

3. Kuendelea kuwa msikivu kwa kushughulikia kero za wananchi kwa haraka,

NB, Hili punguzo linamaana gani ?!

Katika kila shilingi tuliyokatwa awali ni senti 60 tu ndio itachukuliwa na mwanachi Mama amemrudishia|amembakishia senti 40 katika kila muamala anaofanya,

Kama awali ulikatwa Tshs 10,000 Leo utakatwa Tshs 6,000 tu huku Tshs 4,000 Mama akiirudisha|akiibakisha kwako.

...Kazi iendelee | Mama ni habari nyingine ...View attachment 1919029
Inaanza kutumika lini?
 
Wafute pia gharama ya kutumia mobile bank.
Huna Salio kwenye simu huwezi pata huduma za kibank huu ni upuuzi mtupu hakuna sehemu yeyeto duniani.
Nimeishiwa Salio kwenye simu nataka ninunue Salio bank Ili nipate Salio kwenye simu eti ni lzm niwe na Salio kwenye simu huu ni upuuzi mtupu
 
Usitukane fuatilia bei duniani ni kiasi gani sasa hivi na usafirishaji bei imeongezeka hivyo bei inapanda automatically
Mafuta yanapanda duniani kote sawa, sasa serikali ndo iongeze na makodi yao kupitia mwanya huu na kuongeza mizigo mingine ya kodi kupitia mitandao ya simu.
 
Kumtumia bibi yako pesa kijijini hapo unakuwa umefanya biashara gani na umetengeneza faida kiasi gani ili ukatwe kodi. Kimsingi makampuni ya simu ndo yanayofanya biashara kwenye hizi transactions maana wanakata kiasi cha pesa. Sasa hii kodi tunayokatwa na serikali ambayo imebatizwa jina la tozo mantiki yake ni ipi hasa......waache kulaghai watu kwa ujanja ujanja, eti tumepunguza tozo kwa 30%...
Kweli kabisa mkuu, hatuingizi chochote sisi hadi tukatwe iyo kodi. Makampuni ya simu ndo yangebanwa mbavu sio sisi tena.
 
Kodi haitozwi hivyo kwamba kila muamala ni 500, kodi lazima iwe na usawa yule mwenye kidogo alipe kidogo na mwenye kikubwa alipe kikubwa
Hii tozo si inalipwa kwa range yaani so watu wenye kipato tofauti kwenye hiyo range wanalipa sawa tofauti na VAT
 
Huu sasa ni undondocha.
Kushangilia punguzo la makato haramu ya e- money ni ujinga wa karne.
Kama viongozi wangekuwa na akili timamu wangetumia rasilimali lukuki za nchi hii kuzalisha matrilioni ambayo yangeleta elimu bure halisi chekechea mpaka University, afya bure kwa matibabu yote muhimu, n.k n.k
 
Back
Top Bottom