TPA na kampuni ya Dangote waingia makubaliano ya kibiashara kupitia bandari ya Mtwara
Bandari ya Mtwara au huo mkataba namna gani unaongeza huo uzarishaji kutoka 15000 to 43000 kwenye hicho kiwanda cha Dangote...? Muandishi hebu tuweke sawa hapo..

Hicho kiwanda, installed capacity ni 6000ton per day, malighafi kwa kiasi kikubwa inapatikana hapo hapo Mtwara, Coal wanapata songea japo kwa sasa wanatumia Gas ambayo iko hapo hapo mtwara....Hebu tuambieni hiyo bandari itaongeza vipi huo uzarishaji?
Hao chawa wa sa100 hawanaga akili na wana hawawezi kuhoji..wanapewaga script kazi yao ni kukariri tu.

Kimsingi gharama za maisha zimepanda sana na zina panda kila uchwao..serikali haiji na majibu badala yake inakuja na vichaka vya kujifichia..mara kovidi19 mara vita vya ukrain na urusi..sijui vikiisha watakuja na ngojera gani.

Inasikitisha sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na Bwanku M Bwanku.

Ukurasa wa 6 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Jana Ijumaa Machi 18 nimechambua Mkataba mkubwa wa kufanya biashara kupitia Bandari ya Mtwara na zingine ulioingiwa na Serikali kupitia kwa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Dangote.

Mwaka Mmoja wa Rais Samia madarakani na kwasababu ya mazingira mazuri ya Uwekezaji, kufanya biashara na sera nzuri zinazotabirika zilizowekwa na Serikali yake, sasa imani ya Wafanyabiashara na Wawekezaji kufanya biashara na nchi yetu imeongezeka maradufu na ndio maana sasa tunashuhudia ndani ya kipindi kifupi cha Rais Samia namna biashara na uwekezaji mkubwa unaovunja rekodi kuwahi kutokea unavyoshuka nchini. Pata NAKALA yetu sasa ya Gazeti letu hili ili uone maeneo ya Mkataba huo na unavyokwenda kulinufaisha Taifa.

bwanku55@gmail.com

IMG-20220319-WA0009.jpg

IMG-20220319-WA0010.jpg

0a9326c18d7846cdb64d3ebf7d583c8e.jpg

Screenshot_20220318-223121.png
 
Ngoja tuone... Awamu ya tano chupu chupu akimbie nchi...
 
Mkuu, moja kati ya limitation ni warehousing na logistics. Huwezi kuzalisha zaidi ya uwezo wako wa kuhifadhi au kusafirisha. Kuhifadhi kuna gharama sana, na kusafirisha kwa malori nako ni gharama sana. Wakiweza kutumia meli, wataweza kusambaza mzigo haraka, na kuweza kuzalisha zaidi.
Kwa hiyo Magufuri aliyeangaika na kufufua hizo badandari anawekwa upande gani?
 
Hii habari imekaa kimbea mbea,unashindwa kujua lengo hasa wa hayo Makubaliano.Kama swala ni Dangote kutumia bandari ya Mtwara alikuwa anatumia toka JPM akiwepo-sasa issue ni nini?
 
selekali ya rais Samia ina akili sana na inajua kufanya kazi na kuendesha nchi..hii kubwa sana sana hii. Heko mama samia

mnajua kupongeza tu lakini hujui yaliyomo ndio kazi zenu watanzania kusifia tuuu
 
Mbona wewe kama huna uelewa mpana wa mambo?
Uelewa unapimwa na matokeo ya maamuzi yako. Maamuzi mengi ya Magu yalikuwa ya mtu asiye na uwezo wa kuona mwisho akiwa mwanzo. Pima matokeo ya maamuzi yake, linganisha uwiano, halafu utaamua mwenyewe
 
Bwanku M BWanku..Kijana mwenye shahada kutoka chuo kikuu cha UDOM.Hakika huu mwaka upewe teuzi tu,usikate tamaa
 
Uelewa unapimwa na matokeo ya maamuzi yako. Maamuzi mengi ya Magu yalikuwa ya mtu asiye na uwezo wa kuona mwisho akiwa mwanzo. Pima matokeo ya maamuzi yake, linganisha uwiano, halafu utaamua mwenyewe
Ukirudi nyuma Magu kakarabati bandari hawa wanatumia kilikarabati, bila ukarabati wangetumia nini? Mbona unaongea kimipasho na wala sio kimaarifa kama ulivyosema?
 
Ukirudi nyuma Magu kakarabati bandari hawa wanatumia kilikarabati, bila ukarabati wangetumia nini? Mbona unaongea kimipasho na wala sio kimaarifa kama ulivyosema?
Umeona wapi mpasho hapo?

Tuongee facts.

Serikali ya Magu ndio ilileta frustration kwa Dangote mpaka akataka kufunga kiwanda chake.
Serikali ya Magu ndio ilileta frustration kwenye kilimo cha korosho mpaka sasa haijarudi kwenye hali yake ya awali.
Serikali ya Magu ndio ilileta frustration kwenye uchimbaji wa gesi mpaka makampuni ya uchimbaji yakahamia Msumbiji.

Sasa ni sawa aliwekeza kwenye ukarabati, lakini akaleta matatizo kwenye sekta ambazo ndio zingekuwa mtumiaji mkuu wa hiyo bandari. Huko ndiko kukosa maarifa. Alikuwa hana uwezo wa kuunganisha dots, single dimensional thinker.
 
Nimekwambia acha mìpadho na ngonjera zisizo na vina wala vituo!
Frustrations za wakwepa kodi kisa wawekezaji?
Matajiri kuwadhulumu wakulima kisa hawana mtetezi?
Wewe unaongelea korosho! Mazao yote yaliyoleta neema kwa wakulima wetu yalishaharibiwa na watangulizi wake na kuzika kabisa thamani ya mazao hayo!
Kukarabati bandari zetu kulikuwa na fursa nyingi nchini hapa!!
 
Wamekubaliana kwa lipi?Au TPA imetoa bure storage kwenye maghala yake Mtwara, Dar na Tanga,kwa hiyo Dangote hatalipa storage charge?
The looser ni TPA.
Dangote aache kulialia kama mtoto,anunue au akodi meli ya kusafirisha cement yake in bulk kutoka Mtwara hadi bandari za Dar na Tanga, harafu akodishwe sehemu yakujenga mitambo ya kuifunga kwenye mifuko.
 
Nimekwambia acha mìpadho na ngonjera zisizo na vina wala vituo!
Frustrations za wakwepa kodi kisa wawekezaji?
Matajiri kuwadhulumu wakulima kisa hawana mtetezi?
Wewe unaongelea korosho! Mazao yote yaliyoleta neema kwa wakulima wetu yalishaharibiwa na watangulizi wake na kuzika kabisa thamani ya mazao hayo!
Kukarabati bandari zetu kulikuwa na fursa nyingi nchini hapa!!
Halafu utasikia ni tajiri namba moja huku anataka burebure!
 
Inatusaidia nini sisi walala hoi?
Anza kujisaidia mwenyewe. Katafute kazi kwa Dangote. Utangoja sana kusaidiwa,omba omba wahed.

Jiulize, wewe unaisaidia nini nchi yako? Huna kiwanda hata cha kutengeneza pipi hapo nyumbani kwako.
 
Back
Top Bottom