TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

Ila mafuta ulikuwa unapata, vp sasa hivi uwazi upo? Je mafuta yapo ya uhakika?,so impact ya kukosekana kwa mafuta ina ambatana na upandaji wa gharama za maisha, sasa bora kipi uwazi bila mafuta au uficho na mafuta ya kutosha.
Subiri siku 15 zipite ndio uje useme nimekosa mafuta , ila sasa hivi bado yapo, kipindi cha jiwe vitu vilikua vikikosekana lawama zinaenda kwa wafanya biashara kua wameficha mfano mafuta ya kula na sukari kulikua hakuna ukwel
 
Subiri siku 15 zipite ndio uje useme nimekosa mafuta , ila sasa hivi bado yapo, kipindi cha jiwe vitu vilikua vikikosekana lawama zinaenda kwa wafanya biashara kua wameficha mfano mafuta ya kula na sukari kulikua hakuna ukwel
Usubirie siku 15,then ndipo tuhoji manake mpaka sasa kwa hali hii wafanyabiashara washatake advantage na hii situation manake mafuta yataanza kupanda ndani ya siku hizi 15.
 
Kwani mliwah kukoss mafuta?
Ndio nashangaa yaani hawa mfu wamefufuka wanataka kuonesha wanaweza wakati yaliwashinda halafu anaongea uwongo bila kuwa na aibu. Hayo yakuleta mafuta si nyinyi ndio mnaratibu fungueni kila mtu alete anavyotaka halafu tuone ushindani. Msomi mzima unaongea uwongo unaingiza siasa unadhani watu wajinga. Pumbavu kabisa. Mafuta ya baba yenu mpaka muuziwe bure msilete ujinga wenu kama wa kila contract Suma JKT imekuwa kama kampuni mnauwa private sector
 
petroli.jpg


Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, alibainisha hayo jana mkoani Dar es Salaam, akitafsiri kwamba ni hali inayoiweka nchi katika hali ya hatari endapo hatua zinazokwenda kuchukuliwa hazitafanikiwa.

“Hivi karibuni kumekuwa na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi. Kwa sasa hivi mafuta yaliyopo ndani ya nchi yanatosha kwa siku 15 tu. ikitokea chochote kama meli haitakuja ndani ya wiki mbili, nchi itakuwa haina mafuta. Hii siyo nzuri kwa usalama wa nchi,” alisema.

Dk. Mataragio alikuwa anazungumza wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uelewa kwenye eneo la miradi ya kimkakati ya mafuta na gesi.

Alisema kumekuwa na ongezeko la bei na serikali ikaamua kufanya uchunguzi kujua sababu za bei kupanda, huku akifafanua hatua za dharura za sasa ni kwamba TPDC imeshaagiza mafuta ambayo yanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote.

"Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda. Hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu," alisema.

Dk. Mataragio alisema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.

"Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia," alisema.

Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Mkongo wa Juu TPDC, Gaston Canuty, alisema shirika hilo lipo katika mikakati yake ya kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini na limeanzisha mchakato wa kumpata mbia watakayeshirikiana naye kuagiza mafuta.

Mhandisi Aristides Katto kutoka TPDC, akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye vituo vya kuuzia magari, alisema tangu shirika lianzishwe mwaka 2004, takribani asilimia 60 ya umeme katika gridi ya taifa unatokana na gesi.

“Nyumba zaidi ya 600 zimeunganishiwa gesi, magari zaidi ya 600 makubwa na madogo yameunganishiwa gesi na mengi ambayo yameunganishiwa ni zinazofanya biashara ya UBA na BOLT.

"Futi za ujazo bilioni 596 ndizo zilizotumika hadi mwezi Juni mwaka huu. Kati yake, viwandani ni asilimia 19.1303, umeme asilimia 80.8479, taasisi, magari na nyumbani asilimia 0.0218,” alibainisha.

Katto alisema tangu shirika hilo lilipoanza hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, nchi imeokoa dola za marekani bilioni 17.07 (sawa na trilioni 39.1) ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje ya nchi.

Vilevile, alisema kampuni binafsi 10 zimepewa ruhusa ya kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari na moja tayari imeshakamilisha kujenga kituo eneo la TAZARA.

Kuhusu kituo cha gesi kwa mabasi ya mwendokasi, alisema wanatarajia kufungua zabuni ya kutangaza hilo leo na mkandarasi atakayepatikana atakijenga

Nipashe
Haya majitu ya cccm uongozi wa nchi umeshayashinda, sijui tutayachekea chekea hadi lini, ipo siku gesi za kuhudumia wagonjwa mahospitaln mtaambiwa zimeisha.
 
Sidhani kama kauli hii itamfanya aendelee na kazi yake kwa muda mrefu. Nasema sidhani.
Ukiona hivi ujue kuna fukuto. Wanasiasa na matajiri wameshamuingilia. Yupo tayari kwa lolote ukiona hivi. Tuendako ni kubaya zaidi.

Hatukujua sisi kama mafuta yaliwahi kushuka hadi kufikia ziro ila katuambia wakati serikali na waziri wanasema bei imepanda soko la dunia, mara tumetoa tozo.
 
Anatapata tapata tu ila muda utaongea tu na atajulika nani mkweli ila kadili siku zinavyo enda wanazidi kuumbuka na kuna siku watakataana na kugombana wao kwa wao.
We jamaa una akili sana. Huko mbele tutashuhudia wakimtukuza sana JPM na yeyote atakayembeza atakuwa adui yao. Muda utasema.
 
Back
Top Bottom