TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

Mama ana kazi kweli kweli,
Huku ajenge inchi ,
Huku apambane na upinzani uchwara,. Huku apambane na maadui zake wakiwa ndani ya ofisi yake
Upo sahihi mkuu , asilimia kubwa ya wanaokwamisha nchi sasa hivi ni wafuasi wa mwendazake waliowekwa kwenye system , sasa sijui wanawafanya hivyo kwa maslah ya nani , au sijui wanajua kua kipenzi chao atarudi tena
 
Upo sahihi mkuu , asilimia kubwa ya wanaokwamisha nchi sasa hivi ni wafuasi wa mwendazake waliowekwa kwenye system , sasa sijui wanawafanya hivyo kwa maslah ya nani , au sijui wanajua kua kipenzi chao atarudi tena
Samia akiwa na mawazo ya kijinga kama haya yako atapata sana.
 
petroli.jpg


Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, alibainisha hayo jana mkoani Dar es Salaam, akitafsiri kwamba ni hali inayoiweka nchi katika hali ya hatari endapo hatua zinazokwenda kuchukuliwa hazitafanikiwa.

“Hivi karibuni kumekuwa na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi. Kwa sasa hivi mafuta yaliyopo ndani ya nchi yanatosha kwa siku 15 tu. ikitokea chochote kama meli haitakuja ndani ya wiki mbili, nchi itakuwa haina mafuta. Hii siyo nzuri kwa usalama wa nchi,” alisema.

Dk. Mataragio alikuwa anazungumza wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uelewa kwenye eneo la miradi ya kimkakati ya mafuta na gesi.

Alisema kumekuwa na ongezeko la bei na serikali ikaamua kufanya uchunguzi kujua sababu za bei kupanda, huku akifafanua hatua za dharura za sasa ni kwamba TPDC imeshaagiza mafuta ambayo yanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote.

"Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda. Hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu," alisema.

Dk. Mataragio alisema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.

"Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia," alisema.

Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Mkongo wa Juu TPDC, Gaston Canuty, alisema shirika hilo lipo katika mikakati yake ya kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini na limeanzisha mchakato wa kumpata mbia watakayeshirikiana naye kuagiza mafuta.

Mhandisi Aristides Katto kutoka TPDC, akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye vituo vya kuuzia magari, alisema tangu shirika lianzishwe mwaka 2004, takribani asilimia 60 ya umeme katika gridi ya taifa unatokana na gesi.

“Nyumba zaidi ya 600 zimeunganishiwa gesi, magari zaidi ya 600 makubwa na madogo yameunganishiwa gesi na mengi ambayo yameunganishiwa ni zinazofanya biashara ya UBA na BOLT.

"Futi za ujazo bilioni 596 ndizo zilizotumika hadi mwezi Juni mwaka huu. Kati yake, viwandani ni asilimia 19.1303, umeme asilimia 80.8479, taasisi, magari na nyumbani asilimia 0.0218,” alibainisha.

Katto alisema tangu shirika hilo lilipoanza hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, nchi imeokoa dola za marekani bilioni 17.07 (sawa na trilioni 39.1) ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje ya nchi.

Vilevile, alisema kampuni binafsi 10 zimepewa ruhusa ya kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari na moja tayari imeshakamilisha kujenga kituo eneo la TAZARA.

Kuhusu kituo cha gesi kwa mabasi ya mwendokasi, alisema wanatarajia kufungua zabuni ya kutangaza hilo leo na mkandarasi atakayepatikana atakijenga

Nipashe
Kwa maelezo haya mimi sijamuelewa, yaani yeye kama mtendaji analalamika, na hajuhi ni sababu zipi zimepelekea hili tatizo, badala yakuja na njia sahihi za kutatua hili tatizo. Haoni aibu kabisa, anawaambia wananchi hivi na bado yupo ofisini.
 
Maelezo marefu ila ukisoma vizuri utagundua TPDC ndiyo chanzo cha uhaba huo wa mafuta unaotarajiwa.

Pambafu kabisa.
 
Kabisa!
Na siamini kama atakuwa na akili za kijinga kwamba eti wafuasi wa Magufuli wanamkwamisha!

Kwani yeye ni mfuasi wa nani?

Na hao wafuasi wa Magufuli ni kina nani? Wanamfuata kwenye lipi?
Yaani kwa akili zako za kawaida inadhani mama alikua mfuasi wa magu , kwel ww ndio hujui lolote , wakati kuna kipindi alitaka kuondoka kwenye nafasi aliyokuwepo ,wakongwe waka mplease tu ,.
 
Usubirie siku 15,then ndipo tuhoji manake mpaka sasa kwa hali hii wafanyabiashara washatake advantage na hii situation manake mafuta yataanza kupanda ndani ya siku hizi 15.
Umesoma mpaka mwisho!!?..Umeambiwa Kuna mafuta yapo njiani,muda wowote yanaingia
 
Yaani kwa akili zako za kawaida inadhani mama alikua mfuasi wa magu , kwel ww ndio hujui lolote , wakati kuna kipindi alitaka kuondoka kwenye nafasi aliyokuwepo ,wakongwe waka mplease tu ,.
Yani unataka na mimi niwe mpumbavu wa kula maneno ya kwenye vijiwe?

Nmekuuliza wafuasi wa Magu ni wapi na wanamfuata kwenye lipi hadi waanze kumhujumu Samia?
 
Back
Top Bottom