TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

Upo sahihi mkuu , asilimia kubwa ya wanaokwamisha nchi sasa hivi ni wafuasi wa mwendazake waliowekwa kwenye system , sasa sijui wanawafanya hivyo kwa maslah ya nani , au sijui wanajua kua kipenzi chao atarudi tena
Acheni kutafuta excuse. Mbona huyo boss wa Nishati alitoa masharti watu fulani waondoke ndio afanye kazi? Wameondolewa wote bado mnahangaika na visingizio vya sabotage? Mpira ni rahisi ukiwa jukwaani, unaona wanaocheza uwanjani wazembe sana.
 
Hii reverse psychology, mafuta yapo. Watu hamnunui mafuta ya kutosha, mafuta mengi yanaagizwa lakini Tunduma watu wanavuka boda kununua mafuta Zambia.
Hata mimi nahisi hawa wauzaji wanataka kuuza mzigo wao faster kabla ya mzigo wa serikali kuanza kuingia.
 
Kama mwananchi anavyonunua nyanya za jero, kitunguu cha jero, mafuta ya kula ya buku...serikali nayo iko hivyo hivyo...kutonunua vitu in bulk kunaanzia ngazi ya familia hadi taifa...

Au nasema uongo ndugu zangu?
There you are !! Ha ha Haa!!
 
Ewura shida iko kuubwa

Sijaelewa Kwahiyo TPDC watakuwa wananunua Mafuta na Kuuza/Kusambaza?
Kama ndio itakuwa kwa wateja wa Jumla tuu au hata sisi wa reja reja...Kwa maana ya Kuuzia kwenye vituo vya mafuta AKA “Sheli”?
Hizi Wiki Mbili Zijazo watawauzia Kina Nani?
Yaani Mafuta Yakishakuja pale Bandarini watatahifadhi kwenye Store yao/Tank?
Halafu wanawauzia Makampuni?
Kama ni vituo vya mafuta vipi vya kwao au ?
 
petroli.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, alibainisha hayo jana mkoani Dar es Salaam, akitafsiri kwamba ni hali inayoiweka nchi katika hali ya hatari endapo hatua zinazokwenda kuchukuliwa hazitafanikiwa.

“Hivi karibuni kumekuwa na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi. Kwa sasa hivi mafuta yaliyopo ndani ya nchi yanatosha kwa siku 15 tu. ikitokea chochote kama meli haitakuja ndani ya wiki mbili, nchi itakuwa haina mafuta. Hii siyo nzuri kwa usalama wa nchi,” alisema.

Dk. Mataragio alikuwa anazungumza wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uelewa kwenye eneo la miradi ya kimkakati ya mafuta na gesi.

Alisema kumekuwa na ongezeko la bei na serikali ikaamua kufanya uchunguzi kujua sababu za bei kupanda, huku akifafanua hatua za dharura za sasa ni kwamba TPDC imeshaagiza mafuta ambayo yanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote.

"Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda. Hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu," alisema.

Dk. Mataragio alisema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.

"Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia," alisema.

Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Mkongo wa Juu TPDC, Gaston Canuty, alisema shirika hilo lipo katika mikakati yake ya kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini na limeanzisha mchakato wa kumpata mbia watakayeshirikiana naye kuagiza mafuta.

Mhandisi Aristides Katto kutoka TPDC, akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye vituo vya kuuzia magari, alisema tangu shirika lianzishwe mwaka 2004, takribani asilimia 60 ya umeme katika gridi ya taifa unatokana na gesi.

“Nyumba zaidi ya 600 zimeunganishiwa gesi, magari zaidi ya 600 makubwa na madogo yameunganishiwa gesi na mengi ambayo yameunganishiwa ni zinazofanya biashara ya UBA na BOLT.

"Futi za ujazo bilioni 596 ndizo zilizotumika hadi mwezi Juni mwaka huu. Kati yake, viwandani ni asilimia 19.1303, umeme asilimia 80.8479, taasisi, magari na nyumbani asilimia 0.0218,” alibainisha.

Katto alisema tangu shirika hilo lilipoanza hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, nchi imeokoa dola za marekani bilioni 17.07 (sawa na trilioni 39.1) ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje ya nchi.

Vilevile, alisema kampuni binafsi 10 zimepewa ruhusa ya kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari na moja tayari imeshakamilisha kujenga kituo eneo la TAZARA.

Kuhusu kituo cha gesi kwa mabasi ya mwendokasi, alisema wanatarajia kufungua zabuni ya kutangaza hilo leo na mkandarasi atakayepatikana atakijenga

Nipashe

Kwa Alie Elewa:

Sijaelewa Kwahiyo TPDC watakuwa wananunua Mafuta na Kuuza/Kusambaza?
Kama ndio itakuwa kwa wateja wa Jumla tuu au hata sisi wa reja reja...Kwa maana ya Kuuzia kwenye vituo vya mafuta AKA “Sheli”?
Hizi Wiki Mbili Zijazo watawauzia Kina Nani?
Yaani Mafuta Yakishakuja pale Bandarini watatahifadhi kwenye Store yao/Tank?
Halafu wanawauzia Makampuni?
Au Tayari wana Vituo vyao?
 
Zamani serikali ilikuwa inaagiza kwa Bulk Procurement,
Huu mfumo haupo tena?
Au ndio Todc ame take over?
Sijajua Tofauti ya Uagizwaji na usanbazwaji wa Zamani na sasa hivi!
Yaani Sijajua Role ya Tpdc sasa hivi!
 
Naona kuna washenzi fulani kila yanapotokea mapungufu ya utawala wa Samia Suluhu wanaelekeza hasira kwa Magufuli.

Wapuuzi wengine wanamtetea kuwa anahujumiwa na genge la mwandazake! Very silly allegations,

Kuweni na akili za kuelewa mambo, rais aliyepo madarakani hawezi kuhujumiwa kirahisi kwenye mambo nyeti ya kugusa uchumi wa nchi kama haya.

Udhaifu wake msiufunike kwa kuendelea kumsafisha kwa jasho la Mwendazake.

Mafuta yataenda kupanda na bidhaa zitapanda na hali ya maisha itakuwa ngumu.
 
[emoji631] Kule Alska na awii amejanza mafuta mpaka maeneo hayo yakuwa na tetemeko la Ardhi kutokana na mzigo mzito
Umeandika ujinga ujinga tu. Hebu soma uediti ulichoandika.

Alska ### Alaska, awii ### Hawaii, amejanza #### ndio nini?, yakuwa ### ndio nin?

Punguza spidi ya uandishi mbele ya wajuba rijali [emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
 
Ndio nashangaa yaani hawa mfu wamefufuka wanataka kuonesha wanaweza wakati yaliwashinda halafu anaongea uwongo bila kuwa na aibu. Hayo yakuleta mafuta si nyinyi ndio mnaratibu fungueni kila mtu alete anavyotaka halafu tuone ushindani. Msomi mzima unaongea uwongo unaingiza siasa unadhani watu wajinga. Pumbavu kabisa. Mafuta ya baba yenu mpaka muuziwe bure msilete ujinga wenu kama wa kila contract Suma JKT imekuwa kama kampuni mnauwa private sector
Punguza mihemko, uwongo #### uongo.
 
Kama mwananchi anavyonunua nyanya za jero, kitunguu cha jero, mafuta ya kula ya buku...serikali nayo iko hivyo hivyo...kutonunua vitu in bulk kunaanzia ngazi ya familia hadi taifa...

Au nasema uongo ndugu zangu?
Tukaombe tenda ya kujenga ma bunkers ya kuweka akiba ya mafuta.
 
petroli.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, alibainisha hayo jana mkoani Dar es Salaam, akitafsiri kwamba ni hali inayoiweka nchi katika hali ya hatari endapo hatua zinazokwenda kuchukuliwa hazitafanikiwa.

“Hivi karibuni kumekuwa na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi. Kwa sasa hivi mafuta yaliyopo ndani ya nchi yanatosha kwa siku 15 tu. ikitokea chochote kama meli haitakuja ndani ya wiki mbili, nchi itakuwa haina mafuta. Hii siyo nzuri kwa usalama wa nchi,” alisema.

Dk. Mataragio alikuwa anazungumza wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uelewa kwenye eneo la miradi ya kimkakati ya mafuta na gesi.

Alisema kumekuwa na ongezeko la bei na serikali ikaamua kufanya uchunguzi kujua sababu za bei kupanda, huku akifafanua hatua za dharura za sasa ni kwamba TPDC imeshaagiza mafuta ambayo yanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote.

"Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda. Hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu," alisema.

Dk. Mataragio alisema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.

"Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia," alisema.

Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Mkongo wa Juu TPDC, Gaston Canuty, alisema shirika hilo lipo katika mikakati yake ya kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini na limeanzisha mchakato wa kumpata mbia watakayeshirikiana naye kuagiza mafuta.

Mhandisi Aristides Katto kutoka TPDC, akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye vituo vya kuuzia magari, alisema tangu shirika lianzishwe mwaka 2004, takribani asilimia 60 ya umeme katika gridi ya taifa unatokana na gesi.

“Nyumba zaidi ya 600 zimeunganishiwa gesi, magari zaidi ya 600 makubwa na madogo yameunganishiwa gesi na mengi ambayo yameunganishiwa ni zinazofanya biashara ya UBA na BOLT.

"Futi za ujazo bilioni 596 ndizo zilizotumika hadi mwezi Juni mwaka huu. Kati yake, viwandani ni asilimia 19.1303, umeme asilimia 80.8479, taasisi, magari na nyumbani asilimia 0.0218,” alibainisha.

Katto alisema tangu shirika hilo lilipoanza hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, nchi imeokoa dola za marekani bilioni 17.07 (sawa na trilioni 39.1) ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje ya nchi.

Vilevile, alisema kampuni binafsi 10 zimepewa ruhusa ya kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari na moja tayari imeshakamilisha kujenga kituo eneo la TAZARA.

Kuhusu kituo cha gesi kwa mabasi ya mwendokasi, alisema wanatarajia kufungua zabuni ya kutangaza hilo leo na mkandarasi atakayepatikana atakijenga

Nipashe
Blah blah tu kama kawaida yao
 
Mafuta Yana tozo na kodi zaidi ya 25, hayo yatakayoagizwa na tpdc yataondolewa kodi??

Maccm bana sijui nani aliyaloga
 
Upo sahihi mkuu , asilimia kubwa ya wanaokwamisha nchi sasa hivi ni wafuasi wa mwendazake waliowekwa kwenye system , sasa sijui wanawafanya hivyo kwa maslah ya nani , au sijui wanajua kua kipenzi chao atarudi tena
kua #### kuwa
 
Back
Top Bottom