Upo sahihi mkuu , asilimia kubwa ya wanaokwamisha nchi sasa hivi ni wafuasi wa mwendazake waliowekwa kwenye system , sasa sijui wanawafanya hivyo kwa maslah ya nani , au sijui wanajua kua kipenzi chao atarudi tenaMama ana kazi kweli kweli,
Huku ajenge inchi ,
Huku apambane na upinzani uchwara,. Huku apambane na maadui zake wakiwa ndani ya ofisi yake
Hii nchi ina watu wa ajabu sana.Mtu anasema serikali ilikua inaficha, inawezekana vipi?Kama mafuta hamna maana yake tungeona vyombo vya usafiri vimekwama. Huku kuficha ni kupi?Unawezaje kuficha ukosefu wa mafuta nchini? Ebu tupe hiyo mbinu aisee.
Samia akiwa na mawazo ya kijinga kama haya yako atapata sana.Upo sahihi mkuu , asilimia kubwa ya wanaokwamisha nchi sasa hivi ni wafuasi wa mwendazake waliowekwa kwenye system , sasa sijui wanawafanya hivyo kwa maslah ya nani , au sijui wanajua kua kipenzi chao atarudi tena
Unasema ya kijinga kwa sababu nimegusa mshonoSamia akiwa na mawazo ya kijinga kama haya yako atapata sana.
Kwa maelezo haya mimi sijamuelewa, yaani yeye kama mtendaji analalamika, na hajuhi ni sababu zipi zimepelekea hili tatizo, badala yakuja na njia sahihi za kutatua hili tatizo. Haoni aibu kabisa, anawaambia wananchi hivi na bado yupo ofisini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, alibainisha hayo jana mkoani Dar es Salaam, akitafsiri kwamba ni hali inayoiweka nchi katika hali ya hatari endapo hatua zinazokwenda kuchukuliwa hazitafanikiwa.
“Hivi karibuni kumekuwa na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi. Kwa sasa hivi mafuta yaliyopo ndani ya nchi yanatosha kwa siku 15 tu. ikitokea chochote kama meli haitakuja ndani ya wiki mbili, nchi itakuwa haina mafuta. Hii siyo nzuri kwa usalama wa nchi,” alisema.
Dk. Mataragio alikuwa anazungumza wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uelewa kwenye eneo la miradi ya kimkakati ya mafuta na gesi.
Alisema kumekuwa na ongezeko la bei na serikali ikaamua kufanya uchunguzi kujua sababu za bei kupanda, huku akifafanua hatua za dharura za sasa ni kwamba TPDC imeshaagiza mafuta ambayo yanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote.
"Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda. Hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu," alisema.
Dk. Mataragio alisema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.
"Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia," alisema.
Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Mkongo wa Juu TPDC, Gaston Canuty, alisema shirika hilo lipo katika mikakati yake ya kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini na limeanzisha mchakato wa kumpata mbia watakayeshirikiana naye kuagiza mafuta.
Mhandisi Aristides Katto kutoka TPDC, akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye vituo vya kuuzia magari, alisema tangu shirika lianzishwe mwaka 2004, takribani asilimia 60 ya umeme katika gridi ya taifa unatokana na gesi.
“Nyumba zaidi ya 600 zimeunganishiwa gesi, magari zaidi ya 600 makubwa na madogo yameunganishiwa gesi na mengi ambayo yameunganishiwa ni zinazofanya biashara ya UBA na BOLT.
"Futi za ujazo bilioni 596 ndizo zilizotumika hadi mwezi Juni mwaka huu. Kati yake, viwandani ni asilimia 19.1303, umeme asilimia 80.8479, taasisi, magari na nyumbani asilimia 0.0218,” alibainisha.
Katto alisema tangu shirika hilo lilipoanza hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, nchi imeokoa dola za marekani bilioni 17.07 (sawa na trilioni 39.1) ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje ya nchi.
Vilevile, alisema kampuni binafsi 10 zimepewa ruhusa ya kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari na moja tayari imeshakamilisha kujenga kituo eneo la TAZARA.
Kuhusu kituo cha gesi kwa mabasi ya mwendokasi, alisema wanatarajia kufungua zabuni ya kutangaza hilo leo na mkandarasi atakayepatikana atakijenga
Nipashe
We mkongomani kaa kimya tuachie nchi yetuSijaelewa yeye anashauri, analalamika au anafanyaje sasa!
Kabisa!Unasema ya kijinga kwa sababu nimegusa mshono
Kwani mafuta yaliwahi kuisha au kupungua? Mnatua hasira zenu kwa magufuli bila kufikiriEnzi za mtukufu KAYAFA asingethubutu kuongea huo ukweli.
Yaani kwa akili zako za kawaida inadhani mama alikua mfuasi wa magu , kwel ww ndio hujui lolote , wakati kuna kipindi alitaka kuondoka kwenye nafasi aliyokuwepo ,wakongwe waka mplease tu ,.Kabisa!
Na siamini kama atakuwa na akili za kijinga kwamba eti wafuasi wa Magufuli wanamkwamisha!
Kwani yeye ni mfuasi wa nani?
Na hao wafuasi wa Magufuli ni kina nani? Wanamfuata kwenye lipi?
Umesoma mpaka mwisho!!?..Umeambiwa Kuna mafuta yapo njiani,muda wowote yanaingiaUsubirie siku 15,then ndipo tuhoji manake mpaka sasa kwa hali hii wafanyabiashara washatake advantage na hii situation manake mafuta yataanza kupanda ndani ya siku hizi 15.
Yani unataka na mimi niwe mpumbavu wa kula maneno ya kwenye vijiwe?Yaani kwa akili zako za kawaida inadhani mama alikua mfuasi wa magu , kwel ww ndio hujui lolote , wakati kuna kipindi alitaka kuondoka kwenye nafasi aliyokuwepo ,wakongwe waka mplease tu ,.
Ikitokea hiyo meli ikazama au kuungua itakuwaje?Umesoma mpaka mwisho!!?..umeambiwa Kuna mafuta yapo njiani,muda wowote yanaingia
Unaota jamaa,amkaIkitokea hiyo meli ikazama au kuungua itakuwaje?
Kweli eeeh,na maji naa umeme mgao ulikua hausemwi na sisi hatuoni pia.Enzi hizo mambo yalikua hayasemwi
Kwamba hayo niliyosema hayawezi kutokea?Unaota jamaa,amka
Kwa hapo tujipe moyo si ndo manake, what if hayajafika?Umesoma mpaka mwisho!!?..umeambiwa Kuna mafuta yapo njiani,muda wowote yanaingia
Siyo kujipa moyo,tumeagiza,yapo njiani,muda wowote yanaingia,wiki mbili ni zaidi ya muda wowoteKwa hapo tujipe moyo si ndo manake, what if hayajafika?
Ndio kama wewe ambao mnaiombea nchi mabaya ,Ikitokea hiyo meli ikazama au kuungua itakuwaje?