TPDC mnakwamisha Mradi wa Gesi Asilia (CNG) kwa kumkomoa Rais Samia

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Serikali Kupitia Rais imepambana sana kuhakikisha miradi mikubwa inafunguka kwa ajili ya kunufaisha Watanzania wote.

kwanini Mataragio na Genge lako hapo TPDC mnakwamisha mradi wa Gesi asilia? Mnazuia vibali vya makampuni kufungua vituo vya kujaza Gesi kwenye magari kwa maelekezo ya nani? Hata hao wenye sheli walishaomba vibali ili nao wawe na pampu za Gesi asili bado mmewanyima wakati sisi tulijua labda wao ndio wanawapeni rushwa mgomee vibali?

Je, tukisema unamkwamisha Rais katika kuleta maendeleo itakuwa uongo? Nchi nzima vituo vya kujaza Gesi kwenye magari vipo VIWILI tu kweli jamani miaka 60 ya Uhuru ndio aibu hizi?

Serikali ikatoa hela ikaleta mitungi ya Gesi kwa ajili ya magari mkajipendelea mkawekea wafanyakazi wenu tu hapo TPDC halafu wooooote wamekuja kujazana kwenye kituo cha ubungo kujaza gesi wakati mnajua hapana uwezo kuhudumia magari mengi?

Kama hamtaki kutoa vibali kwa nini mlifungia gesi magari ya staff wenu? kwanini msifungue kituo chenu hapo mikocheni mpate raha huko huko pamoja na mamishahara na marupurupu na mafuta ya petrol kibao mnayojipatiaga mnaona mje kujazana na walala hoi hapo ubungo!

Tukisema Mataragio umechoka akili au unafanya kazi kwa mazoea tutakuwa tumekosea?

Rais atuondolee aibu hii aibu hii ya kukaa foleni vituon kujaza gesi masaa!

Fukuza Mkurugenzi TPDC, huyo ashavimbiwa maisha.
 
Nimekuwa najaza Tazara kwa muda mrefu sasa, kuna siku nilipita jioni pale ubungo nyomi niliyokuta hadi barabara ya lami, nikaamua kuondoka........sijui kuna mkono wa nani kwenye kuzuia uwekezaji kwenye vituo vya kujaza gesi kwenye magari. Huenda serikali ya hangaya haijawa tayari kuruhusu biashara ya gesi ili waendelee kuvuna kodi kubwa kwenye mafuta.
 
Kumbe nyie huko Dar mmeshaanza kutumia na gesi kabisa!! Wakati huku kijijini ata umeme bado hatupati achilia mbali mtandao wa simu.
Ila watu wa mjini mnajipendelea sana.

Niulize swali...kwani Gesi mnajazia Bure? Kwanini walete urasimu hadi kitu kinacholipiwa? au wanaleta Yale mambo ya kwenda benki kuwapelekea faida ila unakuta network inasuasua na wahudumu wamerelax kabisa hadi unarudi na pesa zako ulizowapelekea ...nchi yetu inashangaza kwa mengi sana.
 
Serikali Kupitia Rais imepambana sana kuhakikisha miradi mikubwa inafunguka kwa ajili ya kunufaisha Watanzania wote.

kwanini Mataragio na Genge lako hapo TPDC mnakwamisha mradi wa Gesi asilia? Mnazuia vibali vya makampuni kufungua vituo vya kujaza Gesi kwenye magari kwa maelekezo ya nani? Hata hao wenye sheli walishaomba vibali ili nao wawe na pampu za Gesi asili bado mmewanyima wakati sisi tulijua labda wao ndio wanawapeni rushwa mgomee vibali?

Je, tukisema unamkwamisha Rais katika kuleta maendeleo itakuwa uongo? Nchi nzima vituo vya kujaza Gesi kwenye magari vipo VIWILI tu kweli jamani miaka 60 ya Uhuru ndio aibu hizi?

Serikali ikatoa hela ikaleta mitungi ya Gesi kwa ajili ya magari mkajipendelea mkawekea wafanyakazi wenu tu hapo TPDC halafu wooooote wamekuja kujazana kwenye kituo cha ubungo kujaza gesi wakati mnajua hapana uwezo kuhudumia magari mengi?

Kama hamtaki kutoa vibali kwa nini mlifungia gesi magari ya staff wenu? kwanini msifungue kituo chenu hapo mikocheni mpate raha huko huko pamoja na mamishahara na marupurupu na mafuta ya petrol kibao mnayojipatiaga mnaona mje kujazana na walala hoi hapo ubungo!

Tukisema Mataragio umechoka akili au unafanya kazi kwa mazoea tutakuwa tumekosea?

Rais atuondolee aibu hii aibu hii ya kukaa foleni vituon kujaza gesi masaa!

Fukuza Mkurugenzi TPDC, huyo ashavimbiwa maisha.
Namshukuru Mh. Rais Samia kumtimua mkurugenzi wa TPDC! jaman wana JF tukazane kufichua hawa goigoi kupitia jukwaa maana hata mama anasoma humu! kamtwanga tofali puuuu
 
Akili zenu huwa zinawatosha wenyewe. Kabla ya kutoa lawama fahamu kwanza jinsi sector inavyoendeshwa.

EWURA ndio taasisi inayohusika na vibali vya biashara ya mafuta na gas Tanzania; kwenye ‘mid stream and downstream’ sio TPDC.
 
Whatever sie tumeanza na TPDC
 
Whatever sie tumeanza na TPDC
Sasa shida yako ilikuwa upate vituo vya gas?

Au kutumbuliwa kwa Mataragio?

Maana hivyo vitu viwili havina uhusiano, kama shida yako ni vituo vya gas muhusika ni EWURA.

Ila kama shida yako ilikuwa kuona bwana Mataragio anatimuliwa hapo umeshinda.

Lakini aina maana TPDC itaongeza ufanisi.
 
Serikali Kupitia Rais imepambana sana kuhakikisha miradi mikubwa inafunguka kwa ajili ya kunufaisha Watanzania wote.

kwanini Mataragio na Genge lako hapo TPDC mnakwamisha mradi wa Gesi asilia? Mnazuia vibali vya makampuni kufungua vituo vya kujaza Gesi kwenye magari kwa maelekezo ya nani? Hata hao wenye sheli walishaomba vibali ili nao wawe na pampu za Gesi asili bado mmewanyima wakati sisi tulijua labda wao ndio wanawapeni rushwa mgomee vibali?

Je, tukisema unamkwamisha Rais katika kuleta maendeleo itakuwa uongo? Nchi nzima vituo vya kujaza Gesi kwenye magari vipo VIWILI tu kweli jamani miaka 60 ya Uhuru ndio aibu hizi?

Serikali ikatoa hela ikaleta mitungi ya Gesi kwa ajili ya magari mkajipendelea mkawekea wafanyakazi wenu tu hapo TPDC halafu wooooote wamekuja kujazana kwenye kituo cha ubungo kujaza gesi wakati mnajua hapana uwezo kuhudumia magari mengi?

Kama hamtaki kutoa vibali kwa nini mlifungia gesi magari ya staff wenu? kwanini msifungue kituo chenu hapo mikocheni mpate raha huko huko pamoja na mamishahara na marupurupu na mafuta ya petrol kibao mnayojipatiaga mnaona mje kujazana na walala hoi hapo ubungo!

Tukisema Mataragio umechoka akili au unafanya kazi kwa mazoea tutakuwa tumekosea?

Rais atuondolee aibu hii aibu hii ya kukaa foleni vituon kujaza gesi masaa!

Fukuza Mkurugenzi TPDC, huyo ashavimbiwa maisha.
Kwa hiyo wewe #Mtemi mpambalioto ndiye mmojawapo wa wale watu kwenye kikundi kinachoshauri kuondolewa watenda kazi kwa kuzingatia sheria ili kukidhi maslahi binafsi lakini kama sehemu ya kulipiza visasi kwa watu aliowarithi mkuu wa nchi sio?

Jana tarehe 23/2/2023 ulipandisha uzi "Yesterday at 5:40 PM" ukidai Mkurugenzi wa TPDC James Mataragio pamoja na genge lake wanamkwamisha rais........hamadi na leo muda mfupi uliopita mkurugenzi huyo ametenguliwa na kuteuliwa mtu fulani ambaye wewe ndiye ulikuwa unampigia chapuo ijapokuwa kwenye bandiko hukumtaja inavyoonesha umetimiza malengo yako kama ulivyotaka.....jiko la moto mnalichochea wenyewe kwa ajili ya kuinjika sufuria la kutokotesha kitoweo lakini isivyo bahati hamtaweza kuliipua litawaunguza mbele ya safari
 
Kumbe nyie huko Dar mmeshaanza kutumia na gesi kabisa!! Wakati huku kijijini ata umeme bado hatupati achilia mbali mtandao wa simu.
Ila watu wa mjini mnajipendelea sana.

Niulize swali...kwani Gesi mnajazia Bure? Kwanini walete urasimu hadi kitu kinacholipiwa? au wanaleta Yale mambo ya kwenda benki kuwapelekea faida ila unakuta network inasuasua na wahudumu wamerelax kabisa hadi unarudi na pesa zako ulizowapelekea ...nchi yetu inashangaza kwa mengi sana.
Nimeupenda sana huo mfano wa "Benki."
 
Kwa hiyo wewe #Mtemi mpambalioto ndiye mmojawapo wa wale watu kwenye kikundi kinachoshauri kuondolewa watenda kazi kwa kuzingatia sheria ili kukidhi maslahi binafsi lakini kama sehemu ya kulipiza visasi kwa watu aliowarithi mkuu wa nchi sio?

Jana tarehe 23/2/2023 ulipandisha uzi "Yesterday at 5:40 PM" ukidai Mkurugenzi wa TPDC James Mataragio pamoja na genge lake wanamkwamisha rais........hamadi na leo muda mfupi uliopita mkurugenzi huyo ametenguliwa na kuteuliwa mtu fulani ambaye wewe ndiye ulikuwa unampigia chapuo ijapokuwa kwenye bandiko hukumtaja inavyoonesha umetimiza malengo yako kama ulivyotaka.....jiko la moto mnalichochea wenyewe kwa ajili ya kuinjika sufuria la kutokotesha kitoweo lakini isivyo bahati hamtaweza kuliipua litawaunguza mbele ya safari
Naona kuna genge maalum linafanya kazi na Samia; tena limejipachika ujasiri wa hali ya juu sana.
Inaelekea wameanza kujisahau, na kutokumbuka kwamba wanakula na kipofu.
 
Akili zenu huwa zinawatosha wenyewe. Kabla ya kutoa lawama fahamu kwanza jinsi sector inavyoendeshwa.

EWURA ndio taasisi inayohusika na vibali vya biashara ya mafuta na gas Tanzania; kwenye ‘mid stream and downstream’ sio TPDC.
Hii thread ilianzishwa mahususi kwa haya yaliotokea leo sio bure.. mataragio no mchapa kazi hakuna mfano
 
Namshukuru Mh. Rais Samia kumtimua mkurugenzi wa TPDC! jaman wana JF tukazane kufichua hawa goigoi kupitia jukwaa maana hata mama anasoma humu! kamtwanga tofali puuuu
Wewe chawa uliinusa hii sio bure, hahaaa ndio kafanya uhuni kuinajisi katiba na kumteua mzanzibar hii ni hatari sana
 
Kwa hiyo wewe #Mtemi mpambalioto ndiye mmojawapo wa wale watu kwenye kikundi kinachoshauri kuondolewa watenda kazi kwa kuzingatia sheria ili kukidhi maslahi binafsi lakini kama sehemu ya kulipiza visasi kwa watu aliowarithi mkuu wa nchi sio?

Jana tarehe 23/2/2023 ulipandisha uzi "Yesterday at 5:40 PM" ukidai Mkurugenzi wa TPDC James Mataragio pamoja na genge lake wanamkwamisha rais........hamadi na leo muda mfupi uliopita mkurugenzi huyo ametenguliwa na kuteuliwa mtu fulani ambaye wewe ndiye ulikuwa unampigia chapuo ijapokuwa kwenye bandiko hukumtaja inavyoonesha umetimiza malengo yako kama ulivyotaka.....jiko la moto mnalichochea wenyewe kwa ajili ya kuinjika sufuria la kutokotesha kitoweo lakini isivyo bahati hamtaweza kuliipua litawaunguza mbele ya safari
ashakula imetosha! sasa akae atakayenyanyua miradi!
tunataka Gesi ya CNG ifke mikoani sio kuishia kufunga kwenye magari ya staff wa TPDC
 
Kazi ya ewura sijawahi ijua, wana mishahara minono wanachofanya hata sikijui au mi ndiyo mbu3 labda, nisaidie I!
 
Back
Top Bottom