TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria


 

 
sasa kwa nini mashuleni tunatumia kiingereza?
Boss hujui kweli hilo? Tumeachiwa nchi na mkoloni na official language Kiingereza na tulilishwa madini Kiingereza ni bora kuliko lugha yetu ya Kiswahili, na utaalam wetu mwingi tumesomea kwao kwa lugha ya kiingereza, na njaa zetu hizi kuanza kuweka kila kitu kiswahili sina uhakika
 
Historia ya Tz inatuambia kwamba PMs hawawi Marais (except Nyerere). Msuya alijaribu hakuwa, Malecela alijaribu hakuwa, Sumaye alijaribu hakuwa, Salim Ahmed alijaribu hakuwa, Lowassa alijaribu hakuwa, Pinda alijaribu hakuwa, Majaliwa atajaribu na hatokuwa...

Wakati fulani nafikiri ni bora kuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuliko kuwa Waziri Mkuu kama unataka kugombea Urais wa JMT.

Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje akaja kuwa rais, Big Ben (Mkapa) alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje akaja kuwa rais.
 
Namuona Mataragio akisaini na huyu muingereza, matumaini ni kwamba nia ni njema kwa taifa.

Maana Samia anachukuliwa kama ni kivuli cha JK ambaye haaminiwi na kundi lililomuamini JPM. Ni kazi ya kina January kuonyesha kwamba imani hii potofu juu ya awamu ya sita ni potofu kweli.

Uwe ni uzalendo kwa asilimia mia moja, ingawa uzalendo wa kweli ni siri ya moyo wa mtu, hauwezi kuonwa wala kutazamwa kwa macho ya kibinadamu.
 
Wakati fulani public perception inani-drive kutamani kwamba kama hekima ilimuongoza mama kurudisha mtu wa zamani kwenye cabinet aliyekwishashindwa na kuondolewa basi bora angemrudisha Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (MB) kwa sababu ni Tecnocrat and Institutional Memory kwenye wizara hiyo, sekta hiyo, taaluma hiyo kwa viwango vilivyotukuka kitaifa na kimataifa KUMZIDI Makamba.

Naamini Muhongo angesimamia maslahi ya nchi kama alivyofanya kwamba wawekezaji mmoja mmoja wazawa kwenye uchumi wa gesi wata-pool mitaji yao chini ya uangalizi, uwakala na uratibu wa TPDC badala ya mtu binafsi.

Japo leo sijajuwa TPDC inaposukumwa ku-hire consultant wa kigeni kwa gharama kubwa za mabilioni je, gharama hizo zitalipwa toka kwenye hisa za serikali au kwenye hisa za wananchi mmoja mmoja walio-pool rasilimali zao TPDC?


Taswira kwa hisani ya google.
 
😅
 
Ni ajabu sana kwamba hata mabeberu wanathamini uzalendo ilhali mafisadi hawana uzalendo katu.

Hii inamfanya beberu aonekane kama malaika na fisadi aonekane kama ibilisi kwa sababu beberu ana wajibu wa kuona himaya ya nchi yake inakuwa endelevu wakati fisadi ana jukumu kubwa la msingi la kuhujumu na kufisha kila kinachotafutwa kwa ajili ya kuendeleza taifa.

Kwa hulka hizi, ni rahisi kwa beberu kupenya tundu la sindano kuliko fisadi. Mabeberu wako kwa mujibu wa mfumo, itikadi na sheria za mataifa yao ambazo hizi zinatambua uwepo wao, lakini mafisadi wanazuka nje ya wigo wa sheria na wala hawana itikadi ya kusimamia.

Kuondoa ubeberu kunahitaji kufanya mabadiliko ya mfumo, itikadi na sheria ila kuondoa ufisadi kunahitaji dhamira ya kizalendo tu maana hauna uhalali wa kuwepo kisheria.

Iko siku Tz itarejea kwenye Azimio la Arusha ikiwa imeishakomba rasilimali ambazo Azimio hilo la Arusha lingetakiwa kuzilinda!
 
Ubeberu ni dhana zilizoko huku afrika. Zipo kichwani zaidi na ni za kihisia kuliko uhalisia. Huyo huyo mzungu anayejenga hospitali huko Muhutwe au munjebwe anaitwa rafiki wa maendeleo lakini akifanya kama mtoto wa Margret Thatcher kutaka kuipindua nchi fulani ya afrika ndio anaitwa beberu.

Ufisadi husababishwa na sababu nyingi kwa wakati mmoja. Tamaa ya mali inayoambatana na mimi peke yangu ndio nipate. Malengo ya kweli ya kutaka kuwa mfanya biashara mkubwa na anayeishi vizuri na familia yake. Dhuluma kwa maana ya neno lenyewe. Zote hizo ni sifa za ufisadi.

Lakini kisichokuwa cha kwako huwa hakiliki hata siku moja. Kama umepangiwa na Mungu upate kitu fulani hata wakiziba kwa namna ipi utapata tu.

Na tatizo la ufisadi unakuwa na mali ambazo kiuhalisia sio haki yako, ni jasho la walipa kodi wenye kuishi wakiwa wananung'unika kila kukicha hivyo kuwa na hizo mali za wizi hata kama ni wa kisomi kwa namna ipi bado ni kama umeshikilia tu kitu kisichokuwa cha kwako.

Baba yangu mzazi aliwahi kuniambia miaka ya nyuma kuwa mali ya wizi (ufisadi) huwa haimfikii mjukuu hata siku moja, huisha kwa aibu inayoyafuata maisha ya mwizi husika. Pia huambatana na maisha ya wasiwasi, simu ikilia mhusika anajua ni jamaa wa TAKUKURU wanampigia mapigo ya moyo yanaanza kwenda kasi, ilimradi hana amani na mali ambayo sio ya kwake.
 
Ni rahisi kwa waziri mkuu kuhusishwa na matokeo mabovu ya watendaji wengine kwa maana ya mawaziri wenzake.

Ni cheo ambacho mema yako hayaonekani hata kama ni mengi sana lakini baya moja tu linakuondoa.
 



Huyo ndio main senior partner wa hiyo Law ame specialise kwenye mikataba ya mafuta na Gas.

He has background ya accounts why is that important main aspect ya contract consideration kwenye natural resources ni finances. Sasa ina maana kama nchi hatuna accountants wakujadili hayo mambo.

Hatuna wataalamu wengine wa kujadili vipengele vingine kama vya mazingira in terms of environmental costs and so forth. Hao watu lazima wapo. Wana sheria wana draft tu mkataba in legal terms in the end.

Mambo mengine ni ignorance tu ya viongozi wetu; huko nyuma mbona watu hao hao walikuwa wanajadiliana bila ya consultants.

Matumizi mabaya ya hela za serikali na uwezo wa mdogo wa waziri kwenye sector ndio unapelekea mambo kama haya.
 
Kila zama na wahanga wake:-

1. Mwl Nyerere: GAPEX kashfa ya Nyakyoma.

2. Mwinyi: V.G. Chavda na P.G. Chavda $3.5 million za debt conversion program (DCP) 1993 kwa ajili ya mashamba ya katani. Agustino Mrema na wanasiasa wengine walitajwa kunufaika lakini wakafanikiwa kukwepa mkono wa sheria.

Mwinyi: 1995 kashfa ya Mohamed Enterprises ya kusambaza chakula kisichofaa kwa matumizi ya binadamu. Agustino Mrema akaondoka CCM na serikalini.

Mwinyi: 1992 Agustino Mrema alikamata dhahabu ya thamani ya $36,000 JKNIA ikatajwa ni mali ya mkubwa..

3. Big Ben: BoT kwenye bajeti ya 2005/6 ililipa $116 million toka kwenye akaunti ya madeni EPA.

Big Ben: 2001 Idd Simba ajiuzulu kwa kashfa ya sukari. Mporogomyi naye alivuliwa (sikumbuki kwa kashfa ya nini vile sijui minofu ya sangara?)

Big Ben: Ununuzi wa hisa za Kiwira Coal Mine.

Big Ben: Ununuzi wa rada na ndege ya rais, Basil Mramba, Gray Mgonja na Daniel Yona wa mradiakaingia matatani.

4. Kikwete: Waziri wa Ardhi Tibaijuka na AG Frederick Werema wang'olewa kwa kashfa ya Escrow iliyohusu fedha zilizochotwa (Tiba alikuwa mmoja wa wanufaika) ambazo zilihusu wadau wa mradi wa ufuaji umeme IPTL na Tanesco kwa upande wa serikali na fungu kuiendea PAP iliyokuwa mmiliki wa mradi.

5. Magufuli: 2017 Makinikia za thamani ya zaidi ya Tzs.400 tr zamwondoa Sospeter Mwijarubi Muhongo.

2020 $458 ml za drone zamwondoa Kangi Alphaxard Lugola.

NB.
Samia Suluhu naye atakuwa na mbuzi wake wa kafara, hawakosekani na haikwepeki kwenye siasa.
 
Ndipo mama atapogundua kuwa kumbe Kikulacho kii nguoni mwako.


Akili zao zinaganda hawafanyi analysis kabla kufanya miradi mikubwa , wanakulupuka as if Mr Minister ni darasa la saba au ndio personal interest
 
Hatuwezi kuwa sawa, Mtihani ni mmoja wanafundishwa wanafunzi 100. Mmoja anakuwa wa kwanza na mmoja anakuwa wa mwisho.

Ni mapambano mpaka dakika ya mwisho tunapokwenda kaburini.
 
Makamba yeye anamini kila kitu kizuri lazim kitoke nje .juzi hapa kawapa wwhindi tenda ya software as humo ndani hatuna hao watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamba yeye anamini kila kitu kizuri lazim kitoke nje .juzi hapa kawapa wwhindi tenda ya software as humo ndani hatuna hao watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, nitajie kampuni yoyote ya kitanzania ambayo ipo juu kwenye masuala ya kutengeneza software solutions na zikakubalika kimataifa.

Kuna masuala mengine sisi kama watanzania hatuyawezi hata kule DTI hakuna kitu.
 
Mkuu, nitajie kampuni yoyote ya kitanzania ambayo ipo juu kwenye masuala ya kutengeneza software solutions na zikakubalika kimataifa.

Kuna masuala mengine sisi kama watanzania hatuyawezi hata kule DTI hakuna kitu.
Watu kama nyie mnafurahisha kweli umeshawahi kuangalia documentary yoyote ya cyber war.

Watu wanatumiana salamu kwa kuingilia infrastructures za nchi, Iran mitambo yao nuclear enrichment ilipoingiliwa walirudisha salamu kwa kuzima traffic lights na kuchezea kidogo New York subway kwa lengo la kuonyesha ata wao wakiamua wanaweza peleka mazara U.S.

U.S wenyewe na wao wakadai wana uwezo huohuo wakiamua kuingilia mifumo yao mpaka ya maji na kupeleka madhara makubwa aijatokea.

Wewe unashangilia system ya TANESCO kutengenezwa na wahindi halafu kusimamiwa in real time India; we might as well tell them where the nation stores its military ammunition’s.

It’s just stupid, ata watu wakishanunua ndege za vita kitu cha kwanza wana configure electronic systems zake, usidhani waarabu wananunua tu ndege US na software za US.

............................

Na ata hiyo tender ya TPDC ilikuwa kwa ajili ya consultants kuja kuwanoa wataalamu kabla ya majadiliano kuanza; waingie wamejipanga. Sio consultant aje au ashiriki kipindi cha majadiliano na kuweka influence zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…