TRA 2025: Tupeane Mbinu za kufaulu Usaili (Interview) Za TRA

TRA 2025: Tupeane Mbinu za kufaulu Usaili (Interview) Za TRA

Habarini Wakuu!!!!!!

Kama mlivyoona kwenye mitandao ya kijamii. Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania wametoa fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.

Fursa ni nyingi kweli na wamegusa fani nyingi tu. Jumla ya nafasi walizotangaza ni 1596.

Kwa hiyo Wakuu kama kuna mtu ana link ya Group ambao wana solve maswali kwa ajili ya kujiandaa na Interview hii naomba uweke link hapo chini ili watu tujumuike wote.

Ushirikiano ni muhimu watu wote watoboe. Cha muhimu kufika kwenye Oral.

Na kama una hints au topic au maswali unajua yataulizwa, tusaidie kuweka chini hapo kwenye comment ili wengi wafaidike.

Shukran.
1. Fanya Utafiti wa Kina Kuhusu TRA
- Jifunze kuhusu historia, dhamira, malengo, na sera za TRA. Fahamu majukumu ya idara unayofanyiwa usaili na jinsi shirika linavyofanya kazi.
- Tambua mabadiliko yoyote ya hivi karibuni au sera mpya, hasa yale yanayohusiana na TRA 2025, ili uweze kuzungumzia mambo ya sasa.

2. Elewa Nafasi Unayoiomba
- Soma maelezo ya kazi kwa uangalifu ili kuelewa mahitaji, ujuzi na sifa wanazotafuta.
- Jiandae kuelezea jinsi uzoefu wako, elimu yako, na ujuzi wako unavyolingana na mahitaji ya nafasi hiyo.

3. Andaa Majibu kwa Maswali ya Kawaida ya Usaili
- Tafakari maswali kama “Ni nini unajua kuhusu TRA?”, “Kwa nini unataka kufanya kazi hapa?”, “Ni changamoto gani unazoweza kukabiliana nazo katika nafasi hii?” na “Umeweza vipi kukabiliana na changamoto katika kazi zako za awali?”
- Tumia mifano halisi ya mafanikio yako na jinsi ulivyoweza kushughulikia matatizo kazini.

4. Ongeza Ujuzi wa Msingi wa Kitaalamu
- Kama nafasi unayoiomba inahusisha elimu ya sheria za ushuru, hesabu au usimamizi wa rasilimali, hakikisha umejifunza misingi ya mada husika.
- Angalia kama kuna vipimo vya kitaaluma au mafunzo maalum yanayoweza kukusaidia kujitayarisha kwa majukumu ya nafasi hiyo.

5. Mazoezi ya Usaili
- Fanya mazoezi ya kujibu maswali ya usaili na rafiki, mwajiri wa awali, au kupitia video ili kuongeza kujiamini.
- Jifunze kutumia lugha ya mwili inayoonyesha utulivu na kujiamini, kama vile kuangalia jambo kwa undani, tabasamu la kujali, na kuweka msimamo mzuri.

6. Mavazi na Matarajio ya Kitaalamu
- Hakikisha unavaa mavazi yanayofaa kwa usaili. Mavazi safi, ya kisasa na ya kitaalamu huonyesha uzito wa tukio hilo.
- Jiandae kufika kwa wakati na kuwa na nakala za wasifu (CV), barua ya ombi, na hati nyingine muhimu.

7. Kujiandaa Kujulisha Maswali
- Kuwa na maswali yako mwenyewe kuhusu utamaduni wa kazi, maendeleo ya shirika, fursa za mafunzo na maendeleo ya taaluma ndani ya TRA.
- Maswali haya yanaonyesha kuwa umefanya utafiti na una nia ya kweli ya kujifunza zaidi kuhusu shirika.

8. Dhibiti Hisia na Wasiwasi
- Fanya mazoezi ya kupumua kwa kina na tafakari kabla ya kuingia kwenye usaili ili kupunguza wasiwasi.
- Kumbuka kuwa usaili ni mazungumzo; lengo ni kuonyesha uwezo wako na kujifunza kuhusu nafasi hiyo pia.

9. Fuata Miongozo ya Mawasiliano
- Jifunze kusikiliza maswali kwa makini kabla ya kujibu. Usikimbilie, bali toa majibu yenye muundo, na hakikisha unaelezea wazi malengo yako na jinsi utakavyosaidia TRA kufikia malengo yake.

Kwa kufuata vidokezo hivi, utakuwa umejiandaa vizuri na kuongeza nafasi yako ya kufanikiwa katika usaili wa TRA 2025. Kumbuka, mazoezi na utafiti wa kina ni ufunguo wa kujiamini na kuonyesha ufanisi wako.

Ova
 
Huyo kapigiwa assist katika namna ambayo yeye mwenyewe hajui ni nani aliempigia hio assist mpaka leo kwa hio usiseme katoboa mwenyewe kuna mtu kampitishia connection ndio akaingizwa na hamjui huyo mtu mpaka leo
Sijui kwanini nikisikia ishu ya connection na nikilinganisha jinsi nilivyofight bila hiyo connection huwa nabaki kushangaa.

Sikatai kuwa hamna connection lakini Utumishi kwa asilimia nyingi wanatenda haki.
 
Hiki kipengele cha kujaza TIN NUMBER then kina nyota ya Mandatory, kimekaaje, ni kwamba kama hauna TIN inabidi ukakatiwe hiyo TIN ndio uje ukijaze hapa kwenye portal?
 
Sijui kwanini nikisikia ishu ya connection na nikilinganisha jinsi nilivyofight bila hiyo connection huwa nabaki kushangaa.

Sikatai kuwa hamna connection lakini Utumishi kwa asilimia nyingi wanatenda haki
Watu wanapenda kukatisha wengine tamaa tu hamna lolote.

Wadau kibao wanachomoka mtaani na wengi wao ni hawa hawa tunaogonga nao cheers mtaani.
 
Hiki kipengele cha kujaza TIN NUMBER then kina nyota ya Mandatory, kimekaaje, ni kwamba kama hauna TIN inabidi ukakatiwe hiyo TIN ndio uje ukijaze hapa kwenye portal?
Eeh hapo Tin ni mandatory sema kupata Tin si dakika 5 tu kwenye site yao ya Tra.
 
Watu wanapata bwana usiwavunje moyo watu machungu yakupoteza gharama zako kufanya interview ukakosa usilete kuwaaminisha watu ajira zinatangazwa geresha acha watu wapambane nawao waone usikatishe watu tamaa kila mtu na njia yake kwenye hii Dunia tulia dada subili
Kupata wanapata ndio, lakini je hao wanaopata kwa uwezo wao ni wangapi ukiwalinganisha na hao wanaochomekwa na ndugu zao(connection), as a matter of fact kati ya hizo nafasi 1,600 nafasi ambazo zitakuwepo kama sandakalawe kwa ajili ya nyie wengine ambao hamna connection hazitazidi 200 zilizobaki zote 1,400 tayari mpaka sasa hivi zina watu wameshaandaliwa.

Kumbuka hizi ni kazi za TRA taasisi ambayo ni ndoto ya karibu kila mtanzania kuifanyia kazi, maana ukishaingizwa kwenye payroll tu miaka miwili baadae unakuwa sio wewe tena.
 
Nimewaambia wanaona nawaonea wivu eti 😹
Wanajua Tanzania hii wanaijua sana kuliko wengine..!!
Acha waendelee kupeana moyo kwenye hamna wajinga hawa, wanafikiri hii Tanzania ni meritocratic country na wakati nchi inanuka corruption na nepotism kila mahali, na ndio maana ukienda maofisini huko wamejaa wamejaa vilaza watupu na waledi hamna kabisa ila ndio wana enjoy maisha na madharau kibao.
 
Naomba kujua kwa nini wanahitaji TIN number mwenye ile portal yao ya ajira. Ina maana kama sina na imewekwa redstar ina maana sitoweza ku apply?
Changamka ingia kwenye TRA portal unapata TIN faster si una nida yako? Mchawi nida tuu
 
Wakuu msaada hapa kwenye kujaza Qualifications ni kwamba una - upload file moja lenye vyeti vyote ( yani kuanzia cheti cha kuzaliwa hadi chuo ) ??

Au inabidi tu upload cheti kimoja moja ??
Bila shaka portal na tangazo la ajira vyote vina maelekezo!
 
Hiki kipengele cha kujaza TIN NUMBER then kina nyota ya Mandatory, kimekaaje, ni kwamba kama hauna TIN inabidi ukakatiwe hiyo TIN ndio uje ukijaze hapa kwenye portal?
Mbona Tin unaweza kupata mwenyewe ukiingia kwenye TRA portal? Chamsingi uwe na Nida tuu….
 
Wakuu hebu tusaidizane namna ya kuitengeneza password kwenye account ya kuombea ajira maana nimechemsha
 
Hapana mkuu kwenye kufungua account ya ajira pale baada ya verify password kwa mara ya pili ndio inakuja enter one time passcode, na yenyewe pia ina sema verify, bila ya hiyo passcode haifunguki kabisa
Wanakutumia kwenye email hyo passcode chungulia kwenye email yako alafu iandike hapo.
 
Back
Top Bottom