TRA fanyeni kazi yenu kwa ufanisi! Watu hawaombi risiti na wenye maduka hawatoi risiti kikamilifu!

Hili jambo sijui limewashinda TRA au vipi? Kama vipi waajiri watu kukagua Kila anaetoka kwenye badhi ya maduka makubwa.

Ukweli ni kwamba watu hawaombi risiti na wauzaji hawatoi,la sivyo wawe wanafanya ukaguzi wa kushtukiza wakibaini wapige faini hapo hapo maana kuna kulega kutoa risiti tofauti na wakati wa Magu..

Pili polisi washirikoshwe kwenye kukagua bidhaa zote ambazo wateje wananunua kama hakuna risiti faini zihusike mbona watu watadai risiti tuu?..

Angalau TFS wameweza kwenye mkaa kwa nini TRA mnakuwa wazembe? Yaani Nina ushahidi kabisa watu hawadai risiti kabisaa na jamaa usipodai hawakupi.
 
Hizi elimu zianzie shule na huu ndio uzalendo wenyewe hata mtaani watu waelimishwe kwamba huduma wanazohitaji zitapatikana kwa watu kudai risiti,ukinunua anaelipa kodi ninunuzi ukiacha unampa faida muuzaji .
 
Kama mtazania mzalendo ungetoa taarifa polisi haraka au TRA task force chap...hapo ungekuwa umesaidia...
Watuwekee namba za kuwataarifu japo kwa sms maana mimi kila duka nikinunua nisipodai risiti hawanipi nikidai wanatoa chap tena huku wanaogopa kuhisi labda ni Afisa wa TRA..

Uchunguzi niliofanya ni kwamba kipindi cha Magu walikuwa wanatoa risiti fasta bila mteja kudai lakini saizi hawatoi tena risiti maana TRA hawafanyi Kazi yao..

Yaani ukidai ndio wanatoa kwa shingo upande,sasa huu ni upuuzi TRA waweke namba za kuwataarifu kwenye maduka hayo kama ilivyo kwenye mabasi kuna namba za Traffick.

Mara wasingizie network haifanyi Kazi mara sijui nini,hakuna mtu yuko tayari kulipa kodi kwa hiari bila kusukumwa.
 
Umeshauri vizuri mimi niliwahi kushauri hapa wakanitukana! Tatizo hata hao tra sasa hivi upigaji umerudi tena sijui nani wa kumsaidia samia maana inavyoonekana ni kama hawamwogopi tena.
 
Ni vile watu hawaelewi binafsi siko tayari kumnugaisha mfanyabiashara kwa jasho langu bora hiyo fedha iende Serikalini na hata wakisema inaibiwa hawawezi iba yote..

Ni suala la uelewa tuu,kodi nalipa Mimi mfanyabiashara ni njia ya kupitia,wao Kwa kuwa ni wakwepa kodi hawataki tudai risiti kwa sababu otaonyesha ukubwa wa biashara yao na hivyo Kumbe watabainika kuwa walikuwa wanakwepa kodi.
 
Wewe utakuwa kapumbavu! Mbona tumevuka lengo la makusanyo kwa mwezi September? Wacha tu watu waendelee hivyo hivyo!
Umevuka lengo na nani ? Toa upumbavu wako hapa,wamekusanya kwa 94%

Pesa inayotakiwa takiwa kukusanywa ni nyingi zaidi ya hiyo.
 
WEWE NI MUUONGO
 
kwanini wahangaike kufuatilia risiti wakat tozo zipo. wafanya biashara wakilazimishwa kulipa kodi watafunga biashara zao, so bora wasilipe.
 
Duh mtanzania mzalendo nawe ukashiriki kukwepa kodi. Nchi ngumu sana hii.
 
Ni kweli mkuu. Umeongea vizuri ila si wafanyabiashara wote ni wakepa kodi.
 
Huku ulaya kodi inayokusanywa,matunda yake yanaonekana bila ubadhirifu. Sasa Tz kodi kibao na sasa tozo juu na matumizi ya serikali yasioonesha kwa upande wa viongozi kutokuonyesha kubana matumizi ,matokeo yake wananchi wanakosa motisha kuhakikisha wafanyabishara wanatoa risiti. Ukweli mchungu..
Ni kweli mimi naamini watanzania walishazoea kukwepa kodi ma ikitokea mtu anafatilia kodi kikamirifu watamuona ni adui yao! Lakini wakumbuke tunakoomba misaada hawana utani kwenye kodi lakini huku tumachekeana!
i
 
Mwanza inaongoza kutotoa risiti
 
Ach roho mbaya, hatujaridhika na matumizi ya kodi zetu ndo mana hatuombi risiti.
 
wacha watu waibe maana serkalin huko viongoz wanaiba sana na hawaoneshi matumiz bora ya kodi, zaid ya kupanda mindege ya hasara kama walivyosema, na kutoana lunch nje za nchi,...acha watu waibe tu...kula kulana
 
Huo mchezo kawaida K'koo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…