Kwa mtazamo wangu kuna matatizo ya msingi katika mifumo yetu ya kodi na sekta binafsi kiujumla yanayopelekea Hali hii ya kukwepa kutoa risiti.
1. Viwango vikubwa vya Kodi visivyoakisi uhalisia wa faida katika biashara. Kwa biashara ambazo sio kampuni ambazo ndio majority kwa hapa Tz, TRA wanakadiria kodi kwa kuangalia mauzo tu. Hawajali nature ya biashara. Iweje mtu anayeuza hardware akakadiriwa sawa sawa na mfanyabiashara wa nguo wakati profit margin zao hazifanani? Mfano Mfuko wa Cement unaouzwa 15000 utakuta faida yake haizidi 700. Ila Jeans la 15,000 faida inaweza kuwa 3000. Hivyo sio sahihi kuwatoza kiwango sawa cha kodi kisa mauzo ni 15,000. Hili linaweza kupelekea wenye biashara zenye faida ndogo kukwepa kutoa risiti. Maana anaweza kujikuta faida yote aliyopata inakuja kumezwa na kodi.
2. Sekta binafsi isiyo rasmi kwa kiwango kikubwa. Hili linaathiri sana upande wa VAT. Unakuta kwenye Supply chain yupo mtu/watu wenye kuuza bidhaa au kutoa huduma ambao sio VAT registered au hawako kabisa kwenye mfumo rasmi. Matokeo yake muuzaji wa mwisho hana uwezo wa ku-claim VAT yoyote kwenye huduma hizo za katikati na hii kupelekea sehemu ya faida yake kwenda TRA. Kwa style hio wengine ndo maana huamua kutotoa risiti.
So the bottom line is kunahitajika a thorough review of our Tax system. Naamini watu wengi wako tayari kuchangia maendeleo kupitia kodi. Ila ni muhimu upatikane mfumo sahihi wa ukadiriaji wa kodi.