Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, mamlaka hiyo imevunja Rekodi ya kukusanya Kodi kiasi cha Shilingi Trilioni 2.51 kwa Mwezi Desemba 2021 ikiwa ni kiwango cha juu kabisa kukusanywa katika Mwezi tangia kuanzishwa kwake. Katika kipindi cha Desemba 2020, TRA ilikusanya pungufu ya kiasi hicho kwa asilimia 20. Aidha Makusanyo kwa miezi 6 iliyopita ni Shililingi Trilioni 11.11 ikilinganishwa na Trilioni 9.24 zilizokusanywa kwa kipindi kama hicho mwaka 2020.
Pongezi kwa Mhe. Samia, pongezi kwa Kamishna Kidata kwa kutokusanya kodi ya dhulma lakini matokeo yanaonekana. Watanzania lipeni Kodi kwa hiari mjenge nchi yenu.
Kazi Iendelee.
cc:
Suzy Elias