TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

Ntaendelea kutumia,.usafiri wa mungu tu..mpaka kieleweke
 
Magari ya kazi kama ya mizigo ama abiria etc ni public necessity. Magari haya tunayonunua kujirahisishia usafiri binafsi sio personal necessity wala public necessity mana jiulize kila mtu akiwa nalo yatapita wapi.
yatapita barabarani,

Na kama viongozi wanaona barabara hazitoshi suluhisho ni kuongeza na kuborasha barabara sio kuzuia watu kununua magari kwa kuwawekea Ushuru kandamizi wakati wao enjoy to kwenye ma V8
 
Ukiangalia kodi ya kununua gar ya mwaka huu. Ni bora ukanunue la mwaka 2000.
Hakina uhalisia kabisa! Nlitegemea gari la miaka ya karibuni mfano 2015-2018 kodi iwe ndogo ili kuepuka kuagiza magari chakavu yanayochafua mazingira lakini inakuwa ni kinyume kabisa, yaani ni nafuu kidogo kuagiza gari chakavu kuliko lisilo chakavu!
Tz bado tuna safari ndefu sana..
 
Mimi mwenyewe huwa nashangaa Sana Yani sheria inalazimisha watu wanunue magari chakavu badala ya magari ya hivi karibun
 
Magari kuanzia ya 2015 kuja juu hayanunuliki kodi ya kufa mtu badala yake gari za 2007 ndio zinaitwa new model hapa bongo...

Afu wanaosema uchakavu unaongeza kodi siwaelewi mana gari za zamani ndio kodi ipo chini

Watunga Sera wa hii nchi sijui huwa wanaishi vijijini [emoji1]
 
Twende kwa mifano dhahiri Legacy BM9 2010 na VW Jetta ya 2010...tena kwa VW jamaa wa valuation ni wavivu kiasi kwamba kwa VW zote wameweka flat rate kuanzia VW Jetta, Golf, Touran etc CIF wameweka ni $9000

Mkuu unaeleweka vizuri sana ila bahati mbaya unabishana na hewa hapo utapotezewa muda wako tu mkuu.
 
Dogo usijifanye mjuaji sana utadhani wewe ndio Makonda katika nchi hii, gari za bei na ushuru wa namna hiyo zipo nyingi tu. Kwa kukusaidia tu tafuta gharama ya Prado ya mwaka 2019, halafu urudi hapa.

Mpotezee tu huyo mkuu.
 
Nenda kaangalie Subaru Legacy BM9 ya 2009/2010/2011/2012 uone gari ni $3500-5000 ushuru wake ni 22,000,000-25,000,000 mzee
Serikali ya CCM inakomoa raia wake, vyombo vya usafiri ukivipiga kodi kubwa unakwamisha maendeleo.
Tushirikiane kuondoa hawa watawala kila mtu mahali alipo, maana maendeleo ya watu binafsi nchi hii itakuwa ni ndoto!!
Watawala wanajinufaisha wenyewe, wanadai eti wanatetea wanyonge!!
Eleweni maana yangu, wanajiuzia mashangingi bei chee wananchi ni dhuluma tuu wala sio kodi hiyo ni wizi!!
 
Bei ya gari huangaliwa ikiwa mpya.... then mahesabu ya depriciation hufuata... HATA UKIPEWA BURE, KODI UTALIPA... Gari ya mwaka gani? Brand gani? Ikiwa mpya inauzwa shilingi ngapi? Bei ya sasa ni shilingi ngapi? CC ngapi?

Inhibitive, kuna levy brabra pia
 
Nimetumia kikokotoo cha TRA nimechoka kabisa, ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari yenyewe

Watunga sheria wako ndio waliopitisha huo ushuru. Nia na madhumuni yake ni kuwa ushindwe kununua ili magari yawe machache kupunguza msongamano wa magari barabarani.
Watunga sheria walisahau kuwa gari ni nyenzo na inahitajika katika maendeleo na sio kitu vha starehe kama mawazo yao yalivyo.
Badala ya kuongeza miundombinu wao wakaona bora kuweka kodi kubwa kupunguza idadi ya magari bila kujua wanarudisha maendeleo nyuma.
 
Hawataki na sisi tundeshe DISCOVERY 4 hawa.... Kwa kiwa wao wanauziwa yale ma VX R bei ndogo juu kwa juuu
Watunga sheria wako ndio waliopitisha huo ushuru. Nia na madhumuni yake ni kuwa ushindwe kununua ili magari yawe machache kupunguza msongamano wa magari barabarani.
Watunga sheria walisahau kuwa gari ni nyenzo na inahitajika katika maendeleo na sio kitu vha starehe kama mawazo yao yalivyo.
Badala ya kuongeza miundombinu wao wakaona bora kuweka kodi kubwa kupunguza idadi ya magari bila kujua wanarudisha maendeleo nyuma.
 
Me ningekuwa serikali ningepunguza kodi ya kuingiza magari ila ningeweka sheria ya gari zaidi ya miaka kumi kutoingia nchini
Na hv majirani zetu kama Uganda Kenya Zambia Malawi kodi zao za kuingiza magari zipoje? Isije ikawa ndo watu wanagiza magarinwanaenda kuyaregister huko alafu wanayarudisha hapa nchini
 
yatapita barabarani,

Na kama viongozi wanaona barabara hazitoshi suluhisho ni kuongeza na kuborasha barabara sio kuzuia watu kununua magari kwa kuwawekea Ushuru kandamizi wakati wao enjoy to kwenye ma V8
Kujenga more roads kunahitaji pesa kwaiyo tuendelee kutoa zaidi ushuru ili wajenge zaidi. Ukitaka kwenye sherehe ule na kunywa zaidi mchango wako pia lazima uwe zaidi.
 
Back
Top Bottom