TRA inazalisha mabilionea wengi kupitia wafanyakazi wake

AWAMU YA UPIGAJI nchi imepoteza dira na usimamizi wa Fedha za Umma Wasimamizi nao Wapigaji

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Thank you. Watu wengi wamejaa wivu kuliko uhalisia.
Kabisa mkuu, unajua tatizo huanzia vyuoni watu wanapoishi kama vile wanafanana. Wote mpo hostel, wote labda mna pesa za mkopo, mnafanana kwa kila namna ila mnasahau kuwa background ni tofauti, mkitoka chuo ndo utofauti unaanza kuonekana baada ya kuchagua mtindo wa maisha.

Mfano: Vijana wawili wamesoma pamoja.

Kijana wa 1 ametoka kwenye familia ambayo wazazi hawamtegemei mshahara wa M2 na access ya mikopo VS Kijana wa 2 ambaye huko kwao wanamtazama yeye, ana wadogo zake halafu akakimbilia kuoa halafu akaoa familia ambayo wakwe wanamtegemea yeye.

Kama huyu kijana wa pili hana akili ya maisha anaweza dhani mwenzike ni fisadi au freemason.
 
Kuna mwamba mmoja ana Malori ya mizigo matatu, kuna moja mwanangu ndiye anaye lipush. Ila wanasema kwa wale wa maofisini ambao hawana interaction na wafanya biashara uchumi wao ni wakawada, ila kwa wale wanainteract na wateja wanapiga mnooo,ila yote tisa kwa wale ambao wapo bandari wale ndio mabilionea.

Sijui labda hii Technology ya AI inayokuja inaweza ikaautomate vitu vingi na kupunguza upigaji sehemu nyingi.Ndio maana bongo kuendelea kazi mnooo, mzungu akipewa task au project ataifanya kwa uaminifu na ubunifu mkubwa na kuacha alama ya kazi yake,ila ukija kwa mbongo mara zote hutizama mapufungufu ili apige na si kuyaboresha hayo mapungufu.

Halafu wale wachache ambao ni waaminifu, wabunifu na wachapakazi huwagwa wanatengwa au kuundiwa zengwe na ndio maana kuna wengine hukimbilia sekta binafsi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hamna maendeleo ya kutisha hapo, ni maisha ya kati.
Maendeleo ya kutisha unayajua ww? Billionare unawajua ww?
Kufikia ukwasi wa billion si rahis kama unavyodhani. Billion si millions kuna gape kubwa sana
Haya bhana.
 
Nilicho kiandika na ulichojibu ni tofauti, labda umekosea ku reply.
 
Atakapokuja kiongozi kuwapukutisha account zao naomba kelele zisiwe nyingi
unadhani kwa tend hii masisiemu watakubali kumweka madarakani mtu mwenye msimamo kama marehemu jiwe?, never again.

watakuwa makini sana wasirudue kosa. la kuomba Mungu ni kuhakikisha wanafarakana na kunyukana wao kwa wao ili chama chao kivurugike.

nje ya hapo sahau kupata kiongozi atakayefanana na magu mpaka kiama.
 
Polisi hawana maisha huwezi wafananisha na watu wa tra
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…