DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tatizo la nchi hii kodi zote wanataka zikajengee matundu ya choo na madarasa na kugharamia ufahari wa viongozi.
 
Kwa mabilion yanayochezewa wangejikakamua wakajenga express ways hata 4 za inter regions watu wangepita kwa kulipia tolls, mfano DSM-Tunduma ambayo inachukua gari private na baadhi za biashara kama mabasi. Ukiweka 30,000 kwa basi kubwa 20,000 kwa coaster na 10,000 kwa rest of the cars za binafsi kwa siku wangekuwa wanakusanya hela nyingi sana.

Sasa wao mikopo, madarasa na vyoo, zahanati vitu ambavyo vinakuwa liability kwa asilimia 100%
 
You nailed it,got the same point of view
 
Mhimu kupaza SAUTI juu ya hili la mleta Uzi. Kumiliki gari ifike mahali mtu achague mwenyewe kumiliki au kutomiliki kutokana na kumudu gharama za umiliki na sio kununua. Tatizo pengine tutakosa umoja ikiwa Kuna wengine wanataka wamiliki wao TU...japo hata iwe Bei ya kawaida sio wote wataweza ila atleast Kuna wale wenye uwezo Fulani wataweza tu na hivyo serikali kuongeza mapato kupitia mafuta nk. Kuweka Kodi 80-110 % ya Bei ya gari sio sawa kabisa
 
mkuu mtoa mada tatizo sio TRA..wao wanafata sheria iliyopitishwa na wabunge katika kutoza kodi..mwambie mbunge wako kwanza ndio wenye kuamua haya mambo!.
sijui kama hawa jamaa huwa tunawasema kwa haki. ukisoma sheria yao inawataka kusimamia sheria waliopewa,kukusanya na kusifikisha kapu kuu.hawahusiki na kutunga hizo sheria hata kidogo.unakuta mtu anatoka huko ooo wameongeza kodi .hiyo calculator walichokifanya ni kurahisisha tu kitendea kazi kwa kufata sheria nini ninataka.kenya ukiagiza gari zaidi ya miaka mitano mtumba huwezi ingiza huku sisi wameona waweke hiyo ex on age ili kufanya watu washindwe wenyewe. pili hizi rates ni kutokana na makubaliano ya jumuiya ya afrika mashariki kuanzia ushuru wa ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa. shida ninayoiona ni kila mtu atataka kuwa na kodi yake na hapo zamani ndiyo ilikuwa hivo na tulilalamika kwanini A kaleta rav 4 sawa na mimi lakini kodi yake tofauti na yangu ndipo naona walipobudi kikokotoo hicho na kweli kimetufanya tujue tukiagiza kiasi gani tutalipia. na siyo kweli kuwa kodi inaongezeka tu pia kuna wakati pia zinapungua kutokana na aina ya magari yalivyo sokoni. mfano IST ipo sokoni hata kodi yake unaweza ona tofauti na Vitz zile za mwanzo.
 

Aliepeleka mapendekezo ya kodi hizo huko serikalini ni hao hao serikali ambapo TRA ni moja ya taasisi za serikali hivo kama taasisi wana wajibu mkubwa wa kushauri wizara husika, wabunge wetu mnawafahamu kila kitu ni ndio huwezi kua na bunge la kibajaji na msukuma useme watatetea wananchi TRA ndio serikali hao hao
 

Tupaze sauti bidhaa nyingi zinaingilia kwetu lakini ziko juu mno bandari haina faida kwa mwanchi yaani sisi tuna lango la kuingizia magari lakini tunabanwa kizembe kabisa
 
Ubunifu kwa viongozi haupo,wanachowaza ni kumbana mwananchi kwa kila sehemu na ndio maana kila siku tozo mpya inaibuka badala ya kuangalia vyanzo vipya.

Wanakariri mambo hadi sasa inakua aibu wakielezwa wanajificha kwenye kivuli cha uzalendo uchwara, wanahubiri uzalendo ambao hata wao hawana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…