TRA kwenye kodi ya magari wanafanya "wizi" wa wazi kabisa

Tunazidi kulalamika

Kwanini msiache kununua/kuagiza magari

Ova
 
Kodi haiwezi zuia Dumping. Ushawahi Nunua Gari Jipya Ukaona Kodi yake TRA!?
Ni 30% ya Bei.
Gari Mzee ndiyo up to 100%.
Jamaa yupo sawa, gari nyingi bongo ni nzee inabidi ziwe discouraged
Hamna barabara, zilizopo ni two lanes, Sasa miaka hii unaunganisha mikoa na two lanes.
Halafu zinaharibu mazingira kutokana na kutokuwepo miundombinu ya kutosha.
 
Ushuru ndo unajenga barabara unayopita. Tuliza mshono.
Wanakushambulia bure, wana huna kosa. Tatizo ni kuwa watu wanalazimisha kununua magari wakati hawana uwezo. Gari binafsi siyo kitu cha lazima kwani kuna public transport. Kama ulivyosema, anayeona kodi ni kubwa basi ajuwe hana uwezo wa kumiliki gari na atumie ya public.
 
Wabongo utawaweza? Wanapenda kufuata mkumbo bila kutafakari. Utakuta mtu anaenda bar za kishua akiuziwa bia ya eg safari kwa elfu kumi anaanza kulialia bila kujua zile ni kwa wateja wenye uwezo. Usafiri wa umma uko lakini unakuta mtu analazimisha kununua gari huku hata hana uwezo wa kulipia ushuru wake. Wakiambiwa ukweli wanamshambulia aliyewaambia. Hivi kweli mtu kama unashindwa kulipa ushuru wa gari wa sh milioni 5 kuna haja ya kumiliki hilo gari? Kwa nini usipande magari ya umma tu?
 
Nunua mpya mzee uepukane na kodi za kijanja.
 
Halafu utasikia TRA inajiendesha kwa HASARA.[emoji276]
Labda hasara kwa kulipana mshahara isiyoeleweka kama zilivyo kodi zao.
Mkapa alivyoifanyia marekebisho na kuundwa TRA, alikuja na kigezo cha mishahara mizuri ili wasichukue rushwa. Kuna wala rushwa kama wao?
 
Mbona walifuta road license wakaiingiza kwenye mafuta na wanapata pesa nyingi
Mkuu Roadlicence kulikuwa na mianya ya ukwepaji maana kulikuwa na magari yanaswaga tu bila kulipa miaka na miaka so it was easy; Ila hivhi unachosema, gari ambazo zimeingizwa kinyemela sio nyingi kiivyo, Hivyo idea yako ni nzuri ila sio Rahisi sana kuwa implemented kwa sasa; Inawezekana Master plan wazuri wakaiweka katika namna nzuri ya Implementation.
 
Naunga mkono hoja. Leo nimewaza jambo hili. GARI ya milioni 5 kama ist kodi ni asilimia mia ya bei . Gari inafika bandari ya Dar mil 4 ata ikitoka inakua milioni 10. Na hapo bado kuna utitiri wa kodi katika mafuta. Ifike wakati wabunge wa CCM walione hili. Gari sio anasa.
 
akili kisoda huyo
 
Gari sio kwa kila mtu kama unalalamikia Kodi ya 9m TZS (4000 USD) elewa hujafikia hadhi ya kumiliki gari hangaika na Guta, SANLG au FEKON ndo size yako. Asante.
Unakula kwa wazazi wako nakuoga kwa wazazi wako na mpenzi wako naeanakula kwa wazazi wake mnakutana nyumba za wageni tuu
 
Lakini pia viwanda vya nondo vingepata malighafi kibao kutoka nje ya nchi.
Gari hata kama ni screpa hakuna kinachotupwa. Hao wanaosema TRA wanazuia screpa niambieni wapi zipo hizo screpa za bure nikachukue
 
Gari sio kwa kila mtu kama unalalamikia Kodi ya 9m TZS (4000 USD) elewa hujafikia hadhi ya kumiliki gari hangaika na Guta, SANLG au FEKON ndo size yako. Asante.
Unatokea ukoo wa mkoa gani wewe?.

Nadhani huko kwenu gari ni utajiri wakati wenzako ni chombo cha kuikimbiza shilingi ilipo wewe unanujua gari kwenda kuonyesha kijijini kwenu na kwa walio kwenye biashara wanaelewa hii.

Inshort gari kwa kwa kizazi hiki siyo anasa au utajiri.
 
Kodi ya 80% ni maajabu yaliyoko danganyika, na ukiweka na ushuru wa bandari nakuhakikishia kodi inazidi bei ya gari...........kodi ya zaidi ya 100% ni maajabu yanayopatikana Tanganyika pekee, my Lord!!
 
Kodi kubwa sababu unaleta takataka zenye umri uliozidi miaka kumi... hebu hamia kwenye gari mpya tuone kama utaleta kelele tena
 
Kodi kubwa sababu unaleta takataka zenye umri uliozidi miaka kumi... hebu hamia kwenye gari mpya tuone kama utaleta kelele tena
Umeshaambiwa gari mpya hazina unafuu wowote linapokuja swala la kodi za TRA, yaani watu waagize magari wayatumie zaidi ya miaka 10 wewe uite takataka? Nchi za ulaya kuna magari kibao yanauzwa yakiwa used na watu wanayanunua na hayachukuliwi kama takataka, wewe nchi ya kajamba nani uite gari aliyotengeneza majapani takataka wakati huwezi kuunda hata baiskeli, hivi hizi akili za hovyo huwa mnazitoa wapi?
 
Gari sio kwa kila mtu kama unalalamikia Kodi ya 9m TZS (4000 USD) elewa hujafikia hadhi ya kumiliki gari hangaika na Guta, SANLG au FEKON ndo size yako. Asante.
Weyeee, Acha dharau na misifa...! Umewahi kukagua vizuri list na calculation za Import taxes kwenye system ya TRA?

Kwa mfano mimi huwa sioni sababu ya Excise Duty, na hata kama ipo unajua Bongo wanakuchaji % ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…