TRA kwenye kodi ya magari wanafanya "wizi" wa wazi kabisa

TRA kwenye kodi ya magari wanafanya "wizi" wa wazi kabisa

Ndo Mana wahuni wanafanya michongo wanaagiza gari kutoka Japan documents zote zinaonesha gari inaenda Zambia Ila hio cross change inayo fanywa hapo custom ngoma unarudi bongo inatafutiwa plate number maisha yanaendelea
 
Akili yako niyazamani sana.dunia ya leo unashindwa kujua gari ni kitu cha kawaida. Dunia ya leo gari sio ufahari au maisha mazuri bali ni huduma kama huduma zingine.
Nimemshangaa sana huyo Jomba na vidharau vya kishamba, sijui Mtu wa wapi huyo
 
Weyeee, Acha dharau na misifa...! Umewahi kukagua vizuri list na calculation za Import taxes kwenye system ya TRA?

Kwa mfano mimi huwa sioni sababu ya Excise Duty, na hata kama ipo unajua Bongo wanakuchaji % ngapi?
Kama huna pesa gari utaiweza? Pambana na bodaboda.
 
Tatizo vijana kuendesha bodaboda badala ya kufanya kazi za kujenga nchi kama kilimo tusafirishe bizaa.
 
Point ya Jamaa ni valid mkuu, gari pamoja na umuhimu ambao umeusema bado hajafikia kuwa essential item inayohitajika kwenye maisha;

Hivyo kwangu mimi kitu kama gari Kuwekwa kodi hiyo unayosema ni sawa kabisa; Mpaka umewaza hivyo inamaana bado haukuwa na uwezo thabiti kuwa na gari.

Mfano, ukiona unalalamika kwamba Mcdonald, KFC kwamba wanauza vyakula bei juu, its obvious bado hujafika uwezo wa kutumia vyakula vya hapo na sio dhambi usiwachukie wanaomudu hapo au kuwalaumu, vivyo hivyo kwenye gari ungekuwa na uwezo mkubwa kabisa hiyo kodi usingeiona kama kikwazo kabisa, ingekuwa kikwazo kwa watu wengine ila sio kwako.

SO mkuu nimeielewa point yako, ila kimsingi ni kwamba wakati mwingine uwezo wetu ndio unaleta mitazamo fulani inapokuja suala la matumiz ya pesa.
Bado napingana na hii hoja yako,
ni hivi matumizi ya magari hayaishii kwenye anasa peke yake unatakiwa uchukulie upana zaidi hasa uzalishaji mfano unaweza kuta eneo flani watu wanapata changamoto ya usafiri hivyo ni gharama kwenda kupata huduma za kijamii na shughuli za kusafirisha mazao ama raw materials na kuadhiri msisimko wa uchumi.

uwepo wa magari mengi itachochea kupungua kwa gharama za usafirishaji na uchukuzi na kufanya wengi kujikita kwenye uzalishaji kwa maana wanauhakika wa kufikia soko mapema kwa urahisi.
kinachotakiwa ni ukaguzi wa ubora wa chombo kinachotakiwa kuingia nchini na aina ya gari (luxury).
kifupi hatuwezi linganisha na hoja za kfc hapa
 
Bado napingana na hii hoja yako,
ni hivi matumizi ya magari hayaishii kwenye anasa peke yake unatakiwa uchukulie upana zaidi hasa uzalishaji mfano unaweza kuta eneo flani watu wanapata changamoto ya usafiri hivyo ni gharama kwenda kupata huduma za kijamii na shughuli za kusafirisha mazao ama raw materials na kuadhiri msisimko wa uchumi.
Hapo sasa ndio umekuja Vizuri, Gari nyingi za Usafirishaji(Canter, coaster, Bus) Kodi yake ni ndogo kimsingi, isipokuwa bei yake huwa juu wengi huwa hawamudu Bei, you can try it kwa TRA calcultaor kuweka ivi vi-saloon na gari kama Isuzu carries, Fuso Etc na Buses sio kama saloon cars
 
Wizi umekaa kwenye excise duty due to age maana hakuna mantiki yoyote ile maana watu wengi wanaweza kununua magari ya zamani i.e 2000-2010 lakini ukija kwenye gari la kukaribia upya i.e 2015-2021 ushuru wake CIF bado ni kubwa sana
 
Kama mtu anaanza kulalamika tu Kodi ya Kuimport, kuna uwezekanao mkubwa sana akalalamika kwamba kodi ya parking ni kubwa, Spare bei juu etc. Juzi tu utaratibu mpya wa parking ulianzishwa watu wakalalamika kwamba bei ni kubwa, sijui sio rafiki etc; Kila utakachofanya watu watalalamika tu;
Mkuu wewe hauna unachokijua kwanza hakuna kodi ya parking bali ni tozo ile..pia lalamiko kuhusiana na parking ilikua hela inajiongeza kila siku lakini sasa hivi ukiandikiwa unapewa hadi miezi mitano ndo unalipia kwaio hata kama hio siku hauna hela utaja lipa ndani ya muda huo..swala hili haliondoi wizi wa serkikali kwa wananchi kwenye magari sababu hakuna kiwnda chochote kile kinacholindwa
 
Wabongo utawaweza? Wanapenda kufuata mkumbo bila kutafakari. Utakuta mtu anaenda bar za kishua akiuziwa bia ya eg safari kwa elfu kumi anaanza kulialia bila kujua zile ni kwa wateja wenye uwezo. Usafiri wa umma uko lakini unakuta mtu analazimisha kununua gari huku hata hana uwezo wa kulipia ushuru wake. Wakiambiwa ukweli wanamshambulia aliyewaambia. Hivi kweli mtu kama unashindwa kulipa ushuru wa gari wa sh milioni 5 kuna haja ya kumiliki hilo gari? Kwa nini usipande magari ya umma tu?
Kitu ambacho hauelewi wewe ni kwamba watu hawalalamiki kulipoa ushuru bali ni method inayotumika kukokotoa ushuru wa hayo magari ndo tatizo...🤣🤣🤣
 
Wanafanya hivyo kuzuia dumping, bila hizo kodi hii nchi ingekuwa jalala la hayo magari used mbaya zaodi miundo mbinu yetu haiwezi himili magari mengi.

Tafuta pesa
Wangeweka sheria gari ya miaka fulani kurudi chini isiwepo, labda kusiwe na gari ya kuanzia mwaka 90 kurudi chini, nafiki yale mafiati ya madina hapa dar yasingekuwepo teeena
 
Ni 30% ya Bei.
Gari Mzee ndiyo up to 100%.
Jamaa yupo sawa, gari nyingi bongo ni nzee inabidi ziwe discouraged
Hamna barabara, zilizopo ni two lanes, Sasa miaka hii unaunganisha mikoa na two lanes.
Halafu zinaharibu mazingira kutokana na kutokuwepo miundombinu ya kutosha.

Gari gani mpya ambayo kodi ni 30% ya bei?
 
Taja gari moja mpya yenye kodi ndogo.
Huyo Ni kijana unakuta kamaliza Shule huko kijijini kaenda St Augustine University akitoka hapo anapata kazi TRA , matokeo yake ndio hayo.

Linakuwa jitu halijui Jambo lolote tofauti na maisha Yake ya Kijijin. Hana exposure yoyote hata namna Bei za magari zilivyo duniani.
 
Back
Top Bottom