TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

Wamekanusha bana japo wanasema sio rasmi. So tusubiri.
 

Attachments

  • 20230812_000828.jpg
    126.3 KB · Views: 4
Hamna cha lema wala nani kikubwa ni kulipa kodi tena wamehurumiwa wanatakiwa kulipa zaidi ya 365000
Wengine ni hawa bajaji za abiria
Bajaji za mizigo wote hawa wanapata hela bila kukatwa kodi
Usipolipa kodi maendeleo yatatoka wapi ?
wamezoea vya bure hakuna haja ya kulalamika kuna watu wana biashara ndogo kuliko hata bajaji na wanalipa kodi vizuri tu bila shida
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Walitakiwa kutozwa kodi kubwa zaidi ya hii ili iwe fundisho waache kuishangilia CCM.
 
M

aafisa usafirishaji
 
Hiyo kodi ndogo sana wangeweka laki na nusu ili akili ziwakae sawa wawe na ujasiri wa kuhoji matumizi ya kodi zao
Nakuunga mkono mkuu....popote duniani mageuzi yalitokea baada ya life kutight....siku tukibanwa vizuri tutaelewa umuhimu wa kupiga kura...tutaelewa umuhmu wa kuchagua viongozi sahihi....tutaelewa namna ya kudai haki zetu za msingi....tutapata nguvu ya kuhoji matumiz ya serikal...yaan kiiujumla tutakuwa very aggressive...tutaacha ujinga
 
Vizuri sana TRA. Walipe kodi kabisa, walisema na wakaandamana kuwa wanapata milioni tatu kwa mwez. Kama kuna watu wana laki7 na wanalipa kodi, kwanini wao wsichangie uchumi wataifa? Ilichelewa sana
 
Ugumu uko kwenye kuikusanya hiyo kodi, kama kuna pikipiki huko vijijini hazina hata no.au kama no zipo ni bandia au pikipiki haina hata kadi na haijawahi kufanywa chochote na polisi, hiyo kodi itakusanywa vipi?
 
Iko hivi, mifumo yao hauwezi kuilinganisha na huku, usipolipa kodi ulaya maisha yako yatasimama na hauwezi kuishi, lkn kwetu haulipi kodi na unaishi vizuri tu.Hakuna apendaye kulipa kodi duniani kote.Mfumo unawalazimisha wala sio hiali yao, mfano kwa sasa tunalipa kodi ya majengo lkn ulishasikia mtz anagombana na serikali kuhusu hiyo kodi? Kama hautaki kuilipa hiyo kodi basi usiweke umeme nyumbani kwako, je utakuwa na maisha ya namna gani? Sasa ulaya mifumo ya hivyo ni mingi huna pakuchomokea unabanwa kila kona na kodi utailipa tu, Gas, maji, umeme huduma za benki, kadi za usafiri, bima nk utalipa tu upende usipende. Huku watu wanaishi kama mang'ombe halafu unawafuata polini eti unataka maziwa ndoo 5 kwa kila ng'ombe.
 
Vizuri sana TRA. Walipe kodi kabisa, walisema na wakaandamana kuwa wanapata milioni tatu kwa mwez. Kama kuna watu wana laki7 na wanalipa kodi, kwanini wao wsichangie uchumi wataifa? Ilichelewa sana
TRA wanasema sio taarifa rasmi kutoka kwao πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ulishasikia Ulaya mtu anahangaika na ada ya shule ya mtoto au kulipa bima ya afya kama NHIF kila mwaka? πŸ˜€ Ulishaskia raia anaenda kununua dawa pharmacy ya jirani baada ya kujilipia matibabu kwa pesa zake ila hospitali haina dawa? Ulishawahi sikia raia wanalipa sungusungu na ulinzi shirikishi na wazoa takataka kwa pesa zao mtaani ilihali serikali inakusanya kodi kwenye halmashauri? πŸ˜€

Hayo ni machache tu ila kuna kila sababu ya wabongo kukwepa kulipa hio michango ya kodi kwa serikali maana haina mantiki yeyote zaidi ya kuwachangia wezi watakaogawana hizo hela kwenye warsha semina pamoja na kwenye budget za miradi.
 
Kulipa Kodi ni fahari kwa Nchi yako. Acha vijana walipe kodi. Barabara zinajengwa, Reli ya SGR inajengwa, Mifumo ya Maji inajengwa Shule za Msingi, sekondari vituo vya Afya n.k Ongeza vya kwako ktk list
 
Walipe tu maana mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliposema biashara ya bodaboda ni umaskini na laana, baadhi ya madereva wa vyombo hivyo walikuja juu na kusema kazi hiyo inalipa sana ndiyo maana wanaifanya.
Mmoja alisema anapata kipato cha zaidi ya Sh30,000 -40,000 kila siku, sawa na Sh900,000-1,200,000 kwa mwezi.


 
Hiyo kodi ndogo sana wangeweka laki na nusu ili akili ziwakae sawa wawe na ujasiri wa kuhoji matumizi ya kodi zao
Hili kundi la boda boda likiamua nchi inakomboka.
Hoja si kulipa bali matumizi ya kinacholipwa.
Lakini pia kundi la viongozi wa dini au makanisa na waganga wa kienyeji linatakiwa kulipa kodi. Msingi wa kodi ni kwa kila anayepata faida katika transactions zake za kuishi.
Na lisiwepo kundi lisilolipa kodi kisheria(hasa wanasiasa, watendaji wakuu, na majaji) isipokuwa kwa sababu maalum kwa busara ya kamishna mkuu. Tusidanganyane na kunyonyana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…