TRA: Taarifa kuhusu madai ya Diamond Platnumz

TRA: Taarifa kuhusu madai ya Diamond Platnumz

Vipi kwa Wafanya biashara wasio kuwa Maarufu? Lets say ndio mfanya Biashara yuko huko Manyoni Singida, Huu ujinga mtupu, Taasisi zinafanya kazi kwa kuangalua nani kalalamika?
Wanalalamika walalahoi wanapiga kimya
 
Kodi ni takwa la kisheria ni wajibu wa kila mtu anayeingiza kipato kulipia ili taifa litoe huduma na maendeleo kwa watu wake. Lakini ku over tax mfanya biashara/raia hiyo si sahihi na haikubaliki kisheria. Lakini na wewe dogo Diamond show off zimezidi dogo, mara upeleke kundi la chawa wako WC-Qatar, mara kununua Private jet mara Zenj na watu kibao kwa gharama zako, mamlaka zinasohusika na kodi zinaona vitimbwi vyako vyote. Slow down dogo and grow up.
 
Sasa kama mmempa barua na mnasema sheria haziruhusu kuzungumzia taatifa za mlipa kodi waraka huu ni wa nini?
Walaka wa wito...

Mama wa vitenge kariakoo nae aliitwa... kwa style hii sababu alitumia style hii kulalamika...
 
Hata sheria ya kodi iliyokiukwa ni siri.

Hapa TRA wangeweka bayana sheria mfano wale walipa kodi ambao hawakudai risiti za mashine walituweka wazi TRA umma ukajifunza.

Tunaelewa masuala ya benki gani , aina ya akaunti ya benki, account number ya benki ni taarifa za siri za mlipakodi hizo zinafaa TRA wasi share na umma kama walivyosema ktk taarifa kwa umma .

Hii ya TRA kuficha ni sheria gani imevunjwa haikubaliki.
Una weza kuishitaki mamlaka kwa kukiuka sheria kama unahisi hivyo...

Walizuia kontena, dhahabu nk kwa sheria na taratibu zilizo wekwa..,

Kutokujua sheria ni kosa kisheria... ni wajibu wako kujua sheria na kuifata
 
Tatizo ni kwamba huwa mna ‘bias listening’ wakati sakata likiwa linaendelea. Matokeo yake mna kuwa na premise ya kujiaminisha ukweli mnaotaka nyinyi.

Sasa kama ulifuatilia sakata baada ya NHC kuwa inamdai Mbowe kodi ya zaidi ya miaka 5 nyuma, waliamua kumtoa kwa kukiuka mkataba na wakaweka wazi jengo wana mpango walikubadilishia matumizi ivyo litavunjwa wakishamtoa.

Mbowe akakata rufaa, akashindwa; mengine ni facts mnazotaka nyinyi lakini NHC waliweka wazi eneo wanalivunja kufanya uwekezaji mwingine baada ya hapo.
Simba, Yanga na hata TFF ziliwahi kumbwa na kadhia hii kwa nyakati tofauti...

Kodi ilipwe...
 
Alipe Kodi Ili Nchi Iweze Kufanya Mambo Yake
Huyo dogo kama umesikia interview yake , ameelezea vizuri mnoo! kuna jambo haliko sahihi pale TRA katika kadhia hii, na Diamond ameonesha kulipa kila kodi anayopaswa kulipa.

Hata ivyo, amedai kuwa na ushirikiano muda wote anapotakiwa TRA, na akasisitiza kwakuwa TRA ndio waaimamizi wa Kodi, ilipaswa wamwite Office zao ili kumfafanulia mambo ambayo kwa namna moja au nyingine Dogo hayafaham!

Katika hili, kitengo cha kutoa elimu kwa wateja kimepwaya!
 
Kungekuwa hakuna sheria hiyo, bank gani ingekibali kuingilia acc za wateja wake??

ni wajibu wako kujua sheria na kuifata
Ndio TRA pamoja na wewe mnaulizwa ni sheria gani insyoruhusu jambo hilo? Jibu ni kutaja sheria na sio kuuliza maswali tena juu ya maswali.
TRA hata ukiwauliza base ya kuchaji kodi kwa bidhaa fulani (mfano laptop 1 iliyoingia kama learning material) ambapo ziko exempted kwa ushuru, wanakuwa hawana hiyo base badala yake wanakugeuzia kibao mteja uwaoneshe sheria inayosema bidhaa ipo exempted kwa kodi. Yaani hawataki kujibu swali la base ya taxation yao. Ndicho ulichokifanya hapa mkuu
 
Katika hili, kitengo cha kutoa elimu kwa wateja kimepwaya!
Yule bwana Kayombo amekuwa mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa mlipakodi kwa miaka zaidi ya 10 ila hamna anachojifunza. Wasaidizi wake nao hawajifunzi chochote, hawana update ya mabadiliko ya sheria za kodi yanayofanywa na bunge wakati wa kupitisha bajeti nk
Haieleweki hata wanafanya kazi gani ikiwa walipa kodi wengi hawajui kwa nini wanalipa kodi.
 
Mm walinipigia tar 20 Mkuu jamaa alipe Kodi no excuse
Wewe ujamuelewa diamond yeye hajapinga kuhusu kulipa kodi ebu fungua hiyo video umsikilize vizuri anachodai kwanini wamemfungia account zake bila kumpa maelezo yoyote na hajapokea taarifa yoyote wewe angalau umepokea taarifa hiyo ndio hoja yake ya msingi nashangaa wewe unaamisha lengo
 
Back
Top Bottom