BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema hadi kufikia Desemba 31, mwaka huu kila mtu mzima nchini anatakiwa kuwa na Namba ya Mlipa Kodi (TIN).
Hayo yameelezwa na Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi (TRA), Hamadi Mteri wakati wa ufunguzi wa semina kwa wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).
Alisema wa mujibu wa mabadiliko ya sheria, kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 anapaswa kuwa na TIN ifikapo Desemba 31 mwaka huu, la sivyo litakuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA), Richard Kayombo alisema Juni 30, tarehe ya mwisho wa mwaka fedha 2022/23 watakuwa wamekusanya Sh23.1 trilioni, mafanikio aliyosema yametokana na utoaji wa huduma za kidijitali na mifumo rafiki.
“Kwa sasa TRA imerahisisha mfumo kwa wafanyabiashara, hususani kwenye suala la namba ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN), ulipaji wa kodi na mfumo wa forodha ambapo mteja anaweza kufanya vyote hivi kwa kurahisisha kazi zake," alisema Kayombo.
CHANZO: MWANANCHI
UPDATES…
Alipoulizwa kuhusu madai ya kosa la jinai kwa ambaye mtu ambaye hatakuwa na namba ya TIN kama ambavyo Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi (TRA), Hamadi Mteri alivyonukuliwa, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema “Naomba usininukuu chochote, press release ndio tamko letu.
“Ukitaka kuzungumza kitu chochote ambacho kipo nje ya press release yetu maana yake unachokonoa kitu kingine ambacho hakipo, naomba jikite kwenye press release yetu.
“Ufafanuzi wote upo kwenye press release, na ndicho wananchi wanachohitaji kukijua, hata huyo aliyeandika alijitungia, sitaki kuzungumzia hayo, ndio maana tumetoa press release ili mtu asije kuandika nje ya tulichokiandika.
“Sitafafanua chochote zaidi ya kilichoandikwa kwenye press release.”
Taarifa ya TRA