econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
TRA wanajichanganya Sana kwenye suala lililotokea Tegeta la wanaodaiwa wafanyakazi wake kushambuliwa.
1. Kwanza, wanadai gari aina ya BMW T229 DHZ limeingia nchini kinyemela hivyo walikuwa wanalifukuza Hilo gari ili walikamate. Swali ni je Hilo gari liliingiaje nchini Kama sio hao hao TRA waliliruhusu?.
2. Pili, TRA wanadai kwamba kwenye regista yao gari yenye usajili wa T229 DHZ ni minibus na sio BMW. Swali linakuja waligundua Hilo suala usiku huo huko Tegeta ndipo wakaanza kumfukuza huyo mwenye gari la BMW? au waligundua kuhusu suala Hilo zamani ila wakawa wanamtafuta mmiliki au wanampa wito ila hafiki TRA ndipo wakaamua kumuambush huko Tegeta? TRA hawajafafanua vizuri kuhusu hili.
3. Tatu, TRA wanadai hawahitaji ruhusa ya mahakama kutekeleza majukumu yao. Ninachojua TRA kabla hawajakuvamia lazima wakupe barua ya summons au taarifa. Je walimpa mwenye gari taarifa kwamba wanamuhitaji?. Na Kama walimpa taarifa akakataa kutii kwanini hawakuongozana na polisi kumkamata kazini kwake, nyumbani kwake baadala ya kufukuzana barabarani Kama majambazi?
4. Nne, TRA hawajaweka wazi mfanyakazi aliyefariki alikuwa kitengo gani. Taarifa zake zipo juu juu. Hakuna maelezo ya ziada. Hata picha yake rasmi hakuna. Hili linazua maswali je alikuwa kweli mfanyakazi wa TRA au kundi la watu wasiojulikana.
5. Tano, kwanini dereva wa BMW alipiga kelele kwamba anatekwa. Kama alijua anatafutwa na TRA na kweli TRA wakamfikia kwanini apige kelele?. Kuna kitu kinafichwa hapa. Watu wengi hukamatwa na TRA lakini huwa hawapigi kelele za kutekwa. Tena kwenye kadamnasi Kama ile ya TEGETA.
6. SITA, kwanini TRA walisubiri mpaka usiku ndipo waanze kumsaka dereva wa BMW. Hawajaelezea sababu ya kutokumtafuta mchana au asubuhi na kuamua kumkimbiza usiku Tena Kwa kuizonga gari yake kwa mbele. TRA wanamaswali ya kujibu.
7. Mwisho, TRA waache kufukuzana na wateja kienyeji. Miaka kama minne nyuma Kuna wafanyakazi wa TRA walifariki wote kwenye kwa ajali wakati wakimfukiza bodaboda mwenye magendo huko Mkoani Songwe. Ni muda wa kutumia mbinu ambazo sio hatarishi kwa wafanyakazi na Kwa wateja pia.