TRA wanajichanganya sana kwenye suala la Tegeta

TRA wanajichanganya sana kwenye suala la Tegeta

Inawezekana ikawa kweli jamaa aliyededishwa ni kitengo ,nimeona msigwa ,mwigulu ,muliro wamekasirika sana ,halafu jamaa account yake amewafollow stars tu ,nahisi kwa ajili ya kupata info.
Na alikuwa anasoma CBE. Waajiri wake TRA hawana hata picha yake official. Tanzia yake imetangazwa na Bodi ya Wakurugenzi halafu ni Dereva. Hata kama wanatuona mafala sio kiasi hichi😔😔
 
Hakuna kitu hapo...

Na asikudanganye mtu, hao walikuwa walewale, genge la kuteka na kuua watu kwa jina la "sisi ni polisi". Safari hii walikwenda kwa sura ya "sisi wafanyakazi wa TRA" eti wanasaka Kodi usiku. Hii kweli ni Bongolala...!!!

Ni ajabu kuwa polisi nao kwa ujinga wao wanarukaruka kama vyura kwa kuruhusu watu kuji - impersonate kama mapolisi Ili kufanya uhalifu na ujambazi wao...

Angalia tukio/jaribio la kutekwa kwa wakili na mwanaharakati Alfonce Lusako ofisini kwake...

Angalia kauli za kujichanganya za polisi. Yaani Polisi wanasema walienda kwenye ofisi hizo kumkamata mtu aitwaye Emmanuel Mweta...

Cha ajabu wanafika pale na kuanza kumshambulia na kum - harass mtu mwingine asiye huyo wanayedai walikuwa wanamtafuta...

Hawa kama sio majambazi na wauaji wasiojulikana mnadhani ni kina nani...?

Hata hawa wanaojiita "TRA" huko Tegeta, walibadili staili tu. Safari hii waliamua kwenda kufanya uhalifu wao kwa jina la "wafanyakazi wa TRA" kumbe ni "wasiojulikana", majambazi ma - CCM..!!
 
Hayo matukio siyafuatilii kabisa. Ni mambo yanayonajisi moyo ukiyachunguza chunguza. Nawaachia polisi ndio wenye kazi yao.
Hebu nikumbushe Jambo moja kwenye Ile video ya jaribio la Kiluvya kuna mahali plate namba ya watekaji ilionekana? Maana kwenye movie ya Kamanda eti plate number ilibadilishwa😂
 
Mzee Warioba ana miaka 85.

Umri huo hakuna namna anaweza mikiki y urais wala kampeni zake.

Dr. Slaa naye ameshakongoroka.

Hiv Upinzani mmeshindwa kabisa kuandaa mtu wa kuogombea?

Kama hamuez kupata mgombea je ikitokea zari mkashinda mtapata wapi mawaziri?
 
TRA wanajichanganya Sana kwenye suala lililotokea Tegeta la wanaodaiwa wafanyakazi wake kushambuliwa.

1. Kwanza, wanadai gari aina ya BMW T229 DHZ limeingia nchini kinyemela hivyo walikuwa wanalifukuza Hilo gari ili walikamate. Swali ni je Hilo gari liliingiaje nchini Kama sio hao hao TRA waliliruhusu?.

2. Pili, TRA wanadai kwamba kwenye regista yao gari yenye usajili wa T229 DHZ ni minibus na sio BMW. Swali linakuja waligundua Hilo suala usiku huo huko Tegeta ndipo wakaanza kumfukuza huyo mwenye gari la BMW? au waligundua kuhusu suala Hilo zamani ila wakawa wanamtafuta mmiliki au wanampa wito ila hafiki TRA ndipo wakaamua kumuambush huko Tegeta? TRA hawajafafanua vizuri kuhusu hili.

3. Tatu, TRA wanadai hawahitaji ruhusa ya mahakama kutekeleza majukumu yao. Ninachojua TRA kabla hawajakuvamia lazima wakupe barua ya summons au taarifa. Je walimpa mwenye gari taarifa kwamba wanamuhitaji?. Na Kama walimpa taarifa akakataa kutii kwanini hawakuongozana na polisi kumkamata kazini kwake, nyumbani kwake baadala ya kufukuzana barabarani Kama majambazi?

4. Nne, TRA hawajaweka wazi mfanyakazi aliyefariki alikuwa kitengo gani. Taarifa zake zipo juu juu. Hakuna maelezo ya ziada. Hata picha yake rasmi hakuna. Hili linazua maswali je alikuwa kweli mfanyakazi wa TRA au kundi la watu wasiojulikana.

5. Tano, kwanini dereva wa BMW alipiga kelele kwamba anatekwa. Kama alijua anatafutwa na TRA na kweli TRA wakamfikia kwanini apige kelele?. Kuna kitu kinafichwa hapa. Watu wengi hukamatwa na TRA lakini huwa hawapigi kelele za kutekwa. Tena kwenye kadamnasi Kama ile ya TEGETA.

6. SITA, kwanini TRA walisubiri mpaka usiku ndipo waanze kumsaka dereva wa BMW. Hawajaelezea sababu ya kutokumtafuta mchana au asubuhi na kuamua kumkimbiza usiku Tena Kwa kuizonga gari yake kwa mbele. TRA wanamaswali ya kujibu.

7. Mwisho, TRA waache kufukuzana na wateja kienyeji. Miaka kama minne nyuma Kuna wafanyakazi wa TRA walifariki wote kwenye kwa ajali wakati wakimfukiza bodaboda mwenye magendo huko Mkoani Songwe. Ni muda wa kutumia mbinu ambazo sio hatarishi kwa wafanyakazi na Kwa wateja pia.
Hata mimi nimekuwa na shaka kuwa kweli huyo wa kwenye picha ni mfanyakazi wa TRA. Maani sioni wakisema ni mtumishi TRA tawi gani hapa mjini.
 
Kwa maswali haya naona ulitaka wakuandikie gazeti zima ndo uelewe na bado ungeuliza alivyoingia kazini alivaa boksa ya rangi gani.

Cha muhimu watuhumiwa watatu wameshakamatwa na kwa staili hii ya kujichukulia sheria mkononi na kwa polisi ninavyo wajua watu wajiandae kukamatwa kwenye zoazoa utaenda kushinda mahakamani kesi ndiyo lakini utakuwa umekaa gerezani mahabusu siyo chini ya mwaka mzima kwa kesi ya mauaji.

Kwahiyo ni muda wa kila mtu kuangalia step zake
Polisi watamkata yoyote ili kutisha watu, lakini hao task force a.k.a watu wasijulikana sasa hivi ni kuwapiga kiberiti tu wakijitokeza.
 
Wasipoangalia tutaanza kuwawinda na kuwaua popote wanapokuwa
Serikali imewalea, (kumbatia), watu wasiojulikana kwa muda mrefu tume zinaundwa nyuma ya mikamera majibu nyuma ya pazia

Watekaji, (wasiojulikana), ni taasisi kubwa tena haiguswi, wanakuteka halafu hawakuachii hivi hivi bila kilema, kama una bahati mbaya wanakupoteza kwa muda wanaotaka wao
 
Kwanza TRA huwa hawakamati wenyewe ni aidha wanaweka road block kisha askari ndio wanasimamisha magari
Pili kama sio road block bali ni kutafuta magari mitaani pia hawafanyi wenyewe bali hukutumia kampuni za madali kama YONO na Maembe nao pia hawafanyi peke yao bali husaidiwa na jeshi la polisi
Huo ndio utaratibu rasmi

Cha kushangaza jamaa alianza kufukuzwa tangia posta ,walikuwa na uwezekano wa kupiga simu kwa traffic na kuisimamisha kwa mbele ,mwenye gari akiona kasimamishwa na traffic hutii fresh.
 
TRA wanajichanganya Sana kwenye suala lililotokea Tegeta la wanaodaiwa wafanyakazi wake kushambuliwa.

1. Kwanza, wanadai gari aina ya BMW T229 DHZ limeingia nchini kinyemela hivyo walikuwa wanalifukuza Hilo gari ili walikamate. Swali ni je Hilo gari liliingiaje nchini Kama sio hao hao TRA waliliruhusu?.

2. Pili, TRA wanadai kwamba kwenye regista yao gari yenye usajili wa T229 DHZ ni minibus na sio BMW. Swali linakuja waligundua Hilo suala usiku huo huko Tegeta ndipo wakaanza kumfukuza huyo mwenye gari la BMW? au waligundua kuhusu suala Hilo zamani ila wakawa wanamtafuta mmiliki au wanampa wito ila hafiki TRA ndipo wakaamua kumuambush huko Tegeta? TRA hawajafafanua vizuri kuhusu hili.

3. Tatu, TRA wanadai hawahitaji ruhusa ya mahakama kutekeleza majukumu yao. Ninachojua TRA kabla hawajakuvamia lazima wakupe barua ya summons au taarifa. Je walimpa mwenye gari taarifa kwamba wanamuhitaji?. Na Kama walimpa taarifa akakataa kutii kwanini hawakuongozana na polisi kumkamata kazini kwake, nyumbani kwake baadala ya kufukuzana barabarani Kama majambazi?

4. Nne, TRA hawajaweka wazi mfanyakazi aliyefariki alikuwa kitengo gani. Taarifa zake zipo juu juu. Hakuna maelezo ya ziada. Hata picha yake rasmi hakuna. Hili linazua maswali je alikuwa kweli mfanyakazi wa TRA au kundi la watu wasiojulikana.

5. Tano, kwanini dereva wa BMW alipiga kelele kwamba anatekwa. Kama alijua anatafutwa na TRA na kweli TRA wakamfikia kwanini apige kelele?. Kuna kitu kinafichwa hapa. Watu wengi hukamatwa na TRA lakini huwa hawapigi kelele za kutekwa. Tena kwenye kadamnasi Kama ile ya TEGETA.

6. SITA, kwanini TRA walisubiri mpaka usiku ndipo waanze kumsaka dereva wa BMW. Hawajaelezea sababu ya kutokumtafuta mchana au asubuhi na kuamua kumkimbiza usiku Tena Kwa kuizonga gari yake kwa mbele. TRA wanamaswali ya kujibu.

7. Mwisho, TRA waache kufukuzana na wateja kienyeji. Miaka kama minne nyuma Kuna wafanyakazi wa TRA walifariki wote kwenye kwa ajali wakati wakimfukiza bodaboda mwenye magendo huko Mkoani Songwe. Ni muda wa kutumia mbinu ambazo sio hatarishi kwa wafanyakazi na Kwa wateja pia.

Ni kwasababu wanataka kupewa rushwa na njia ni kutishia watu badala ya kwenda kiofisi
 
Back
Top Bottom