TRA wanajichanganya sana kwenye suala la Tegeta

Kwa uchambuzi huo, hao ni TRA kweli?
Lakini wapigwe tu maana hakuna namna!
 
TRA Tanzania Kuna maswali yenu huku
Hayo maswali yanajirudia ila Kimsingi yapo maswali mawili tu

Majibu

1. Afisa uchunguzi yoyote Sifa yake Kuu ni " Machale kumcheza" kwahiyo maafisa hapo kulituhumu hilo Gari ni jambo la Kawaida sana
Kayombo amesema hilo Gari lilitiliwa shaka hivyo lilisimamishwa kwa sababu ya ukaguzi na endapo ingedhihirika Kuna Jinai police wangetaarifiwa kwa hatua za ukamataji

2. Utendaji KAZI wa Kila siku wa TRA hauhitaji KIBALI cha Mahakama vinginevyo KAZI za Mahakama zingekuwa ni kutoa vibali vya TRA kila siku na Kesi za Wananchi zisingesikilizwa

Summons huhitajika kwenye utekelezaji wa majukumu maalumu

Na mwisho Customs department - TRA wanafanya KAZI saa 24 miaka yote kabla hata TRA haijaasisiwa

Ahsante sana 😄🌹
 
'Kwanini TRA walisubiri mpaka usiku ndipo waanze kumsaka dereva wa BMW. Hawajaelezea sababu ya kutokumtafuta mchana au asubuhi na kuamua kumkimbiza usiku Tena Kwa kuizonga gari yake kwa mbele. TRA wanamaswali ya kujibu'.........Hapa ndipo kwenye mashaka zaidi
 
Acha kuumiza kichwa, yule dogo hakuwa muajiriwa wa TRA. Wamebebeshwa gunia la mavi kwa lazima hivyo wanaenda nalo hivyohivyo mpaka mambo yatakapopoa, wao ni sehemu ya dola hivyo wamepewa jukumu la kuvifichia aibu vyombo vinavyowaongoza wasiojulikana.
 
Ungekuwa na ABC ya mbinu wanazotumia wakwepa kodi, ungejiona unaliuza ujinga
 
Na baadaye watatoka lakini ile maiti haitafufuka.
 
Wale hawakuwa TRA, unadhani yule dogo iliyededishwa alikuwa anaishi hewani? Watu wanamfahamu na ndiyo maana wanashangaa katoka lini kitengo kuingia TRA?
Hawa madogo wanatumika vibaya acha waonje joto ya jiwe, wametesa na kuua sana so let them feel the music as well. What goes around comes around.
 
Probably kuna jambo hatulijui,
Niliuliza kama TRA wana uwezo wa kumfukuzia mtu na kutaka kumkamata bila uwepo wa askari polisi tena usiku,ama tra nao ni kama jeshi?
 
Kwani hujui 80% hapo TRA ni kitengo 😂😂😄😂
 

Inawezekana ikawa kweli jamaa aliyededishwa ni kitengo ,nimeona msigwa ,mwigulu ,muliro wamekasirika sana ,halafu jamaa account yake amewafollow stars tu ,nahisi kwa ajili ya kupata info.
 
Hao ni vijana wahuni tu aka vishoka walikuwa wanafukuzia dili

Siku hizi Kuna vijana hapo tra eti unaweza kuwatuma kwa madeni wako wakadai madeni yenye VAT

Hii huduma mpya sijui?;comissiona anaowatumia? Wadai Kodi kwa utaratibu huu
 
Kwanza TRA huwa hawakamati wenyewe ni aidha wanaweka road block kisha askari ndio wanasimamisha magari
Pili kama sio road block bali ni kutafuta magari mitaani pia hawafanyi wenyewe bali hukutumia kampuni za madali kama YONO na Maembe nao pia hawafanyi peke yao bali husaidiwa na jeshi la polisi
Huo ndio utaratibu rasmi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…