TRA waunde kitengo cha upangishaji wa nyumba, kila mwenye nyumba aripoti TRA anapotaka kupangisha na iwe kwa mujibu wa sheria



Wazo zuri. Hili naliandika ktk diary yangu bali litakuwa na marekebisho madogo. Nitagombea Urais 2025 tukiwa hai. Nikishinda urais kwanza nyumba zote zilizotaifishwa na Serikali nitazirudisha kwa wamiliki, nyumba zote zilizojemgwa na serikali wanasiasa wakauziana nitazitaifisha na kumilikiwa na sheirika la nyumba. Utaanzishwa sheria ya upangaji ili mpangaji alipe kodi kwa mwezi na isizidi kodi ya miezi miwili. Yaani mwezi mmoja na mwezi unaofata. Na mwezi unaofata utalipa mwezi mmoja mmoja. Na iwe sheria kutolipwa Kofi kwa siku 60 ni sawa na kumwambia mwenye nyumba kuwa hutoendelea kupanga na anahaki ya kuleta mpangaji mwengine. Ila kwa huruma yake anaweza kukuvumilia.

Usimamizi wa walipa Kofi utakuwa chini ya hamlshauri na wenyeviti wa serikali za mitaa badala ya TRA.

Moja ya Sera ktk chama nitakachogombea kitafata Serikali ya majimbo 10 (autonomous) yatakayopewa mamlaka zaidi ya kujiamulia mambo yao wenyewe sawa na mamlaka yaliyopo jimbo la Zanzibar ktk mfumo wa serikali ya ccm.

Na majimbo hayo 10 tutayapa mamlaka zaidi ya jimbo la Znz kwasasa
 
Kibox manyoya unacho ww fanya kazi hakuna mteremko siku hizi[emoji23][emoji23][emoji23]
Watu wanapig huku na huku kaa kijana ngoja madalali wa kihaya wapate taarifa😀😀😀
 
TRA ni mbali naona serikali ya mitaa inaweza kupewa Jukumu hili na ikawa rahisi sana yaani nikitaka kupanga chumba mtaa fulani naenda moja kwa moja ofisi ya serikali za mitaa napewa sifa ya nyumba zilizopo basi naonyeshwa. inaweza hata kuwekwa kiwango cha TSH 10,000 Kwa kila mpangaji ikakuza mifuko ya SM
 
Kodi za majengo tu Halmshauri ziliwashinda, ndio ije kuwa hii ya kukusanya kodi zinazotokana na kupangisha?
 
Kwani mtumishi wa umma anaelipa PAYE anafanya biashara gani ya kupata faida kupitia hiyo kazi alioajiriwa na serikali?
Anafanya biashara ya kuwahudumia walipa Kodi kwa kutumia taaluma yake.
 
Ujumbe huu umfikie Waziri mwenye dhamana Mhe. Mwiguru Lameck Nchemba.
Wazo zuri sana hili
 
Hauna point hapa Chief.
Who is dalali? Simply ni agent wa kumuunganisha mteja na mwenye nyumba.
Sasa why adai kodi ya mwezi mmoja? Kwanini usiwepo utaratibu akalipwa na mwenye nyumba maana ndiye alompa kazi ya kusaka wateja?

Kwanini isiwepo means nzuri ya wenye nyumba kupata platform ya kutangaza nyumba zao zinazopangishwa na watu wakapata nafasi ya kuziona ma katika malipo hayo Serikali ikakusanya kodi?

Dalali kama ni muhimu kwanini formula yake inaumiza mpangaji pekee?
 
Sawa, ila kaa ukijua TRA wenyewe ni moja ya taasi failure hapa nchini..
Sio kila kazi wafanye wenyewe, sema labda tungesajili madalali ili nao walipe kodi, maana kumbuka mwenye nyumba analipa kodi kupitia kodi ya majengo.
Ni kweli TRA kuna vitu inafeli. Ila wakiamua kuweka mifumo madhubuti ya kukusanya kodi hii ya zuio kwenye kodi za nyumba wanaweza kuongeza makusanyo sana tu. Hii kodi ya zuio kwenye kodi za nyumba/majengo kiuhalisia analipa mpangaji, akishalipa anampa cheti mwenye nyumba kuwa amemkata kodi na amepeleka TRA.
 
Wapangaji ndio huenda kuwaomba madalali wawatafutie nyumba za kupanga Sasa unataka mwenye nyumba amlipe kwa lipi?

Wewe unaenda kuomba huduma ya dalali halafu eti ohh mwenye nyumba amlipe kwa lipi wakati mkataba wa kikazi Ni wewe mtafuta nyumba ya kupanga mumeingia na dalali wako uliyemkuta kijiweni au popote kuwa nitafutie nyumba.Wewe ndio umlipe kwa hiyo huduma aliyokuwa na huyo dalali huyo ndie uende ukamripoti TRA

Ieleweke wazi contract ya kikazi ya kutafuta nyumba Ni yako wewe na dalali wako sio mwenye nyumba

Waziri alivyoliweka haliko sawa kisheria .Watu wanaenda wenyewe kwa madalali kwa hiari yao bila shuruti na kuingia mikataba nao ya kutafuta nyumba at a fee of course ambayo Ni Kodi ya mwezi mmoja
 
Ujumbe huu umfikie Waziri mwenye dhamana Mhe. Mwiguru Lameck Nchemba.
Wazo zuri sana hili
Halina chochote Hilo wazo ujinga mtupu

Mpangaji ndie humfuata dalali amtafutie nyumb
Kwa maneno mengine kazi ya kutafuta nyumba dalali hupewa na mpangaji ndio maana dalali aweza hangaika na kumuonyesha mpangaji nyumba kibao achague atakayo

Dalali hamfuati mpangaji Bali mpangaji ndie humfuata dalali kumuomba amsaidie kazi .Mwajiri wa Dalali Ni mpangaji aliyempa kazi ya kutafuta nyumba
 
Wenye nyumba wanalipa kodi,inaitwa With holding Tax,mpangaji huwa analipa kwa niaba ya mwenye nyumba,inaitwa with holding tax(kodi ya zuio),halafu wanakatana kwenye kodi.n

Nina zaidi ya miaka 15 ya kupangisha nyumba sijawahi kulipa hiyo kodi Kwenye biashara yangu ya upangishaji
Kodi ya Ardhi tu ndio wameanza kulipa wapangaji kupitia huu mfumo wa luku
 
udalali ni ajira labda waweke regulation dhidi yao sio TRA kuchukua jukumu vijana wengi wamejiajiri huku acheni mawazo potofu ukilipa ya mwezi ni fresh kwani unalipa tena
Ni wizi kwa sababu hawalipi kodi yoyote, na kama alivyosa Lukuvi mlipaji anatakiwa awe mwenye nyumba, lakini pia wasilipwe kodi ya mwezi...
 
Kutumia dalali hujalazimishwa katafute mwenyewe basi hujazuiwa pita kila nyumba gonga hodi uliza Kama wanapangisha Kama unaona kazi ya dalali haina maana
Mmeshawaroga wenye nyumba hata nyumba ikiwa empty na ukajua analazimisha uende kwa dalali...Kwa kifupi ni asilimia 0.001 ya nyumba zinapangishwa bila dalali. Kiasi kwamba inaondoa maana nzima ya udalali...

Chukueni tu asilimia kadhaa, mwezi mmoja jamani??
 
Wenye nyumba mnajikutaga mmemaliza maisha ila elfu 70 70 za wapangaji mnazitaka.

Yaani mnataka kufanya biashara bila running costs au sio? Maana kodi ya ardhi sijui majengo tunawalipia kwenye umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…