TRA waunde kitengo cha upangishaji wa nyumba, kila mwenye nyumba aripoti TRA anapotaka kupangisha na iwe kwa mujibu wa sheria


Mwenye nyumba anautaratibu wake wa kulipa kodi zake Serikali ni.
Cha msingi ni vyema Serikali ikaweka utaratibu wa kuwasajili na kuwatambua madalali wote ,( ma commission agents, ma brokers, wote kuanzia wa nyumba,viwanja, Magari, mikopo, ajira, wake/ waume, kuzamia nje, nk)

Kisha iwatoze kodi kutokana na kipato watakachokuwa wanapata hao madalali.
Suala la gharama zao zinaweza kuachwa kuwa huria .
Na nyie wapangaji msipende kuhama hama sana ili kujiepusha na hizo gharama za madalali.
Nina wapangaji wamepanga kwangu huu mwaka wa 5
 
Jibu Zuri Umempa hiyo Kiazi..Kujenga sio lelemama ati....
 
Bora kuwe na kitengo serikali za mitaa kwaajili ya kuratibu wapangaji na wapangishaji ambao watakuwa na full data za nyumba ambazo zinahitaji wapangaji na walipwe na serikali iwe ni ajira rasmi na walipwe mshahara kwa skeli za serikali
 
Kinachozungumziwa siyo kodi ya nyumba hapa tunazungumzia gharama za kulipa madalali
 
Kama mnaumia basi jengeni zenu

Mwende mkaweke izo sheria zenu uko kwenye nyumba zenu.

Sio unaweka sheria mbofu mbofu kwenye jasho la Wanaume wenzenu.
Na wewe kama unaona kuweka taratibu ni mzigo Bora uishi kwenye nyumba yako mwenyewe
 
Sawa hayo yote kwa kafanya kwa manufaa ya mwenye nyumba, so mwenye nyumba ndo awajibike kumlipa sio mie mpangaji.
 
Sawa hayo yote kwa kafanya kwa manufaa ya mwenye nyumba, so mwenye nyumba ndo awajibike kumlipa sio mie mpangaji.
Ni manufaa yako mpangaji sio mwenye nyumba dalali Ni wakili wa mpangaji kumbuka hata tatizo likitokea mfano umepangisha jambazi mwenye nyumba mtu wa kwanza kudakwa Ni dalali aliyekupeleka sio mwenye nyumba

Dalali ndie hubeba Zigo la kuwa anakujua vizuri.Risk zote huangukia kwake.

Wewe ndie unayemtuma Kama wakili wako . Kumlipa kazi yake ya uwakili Ni yako
 
MAWAZO YA KIMASIKINI HAYA
Tuwaache wastaafu wanufaike na jasho lao maana nyingi ni za wastaafu property tax ilipwayo inatosha kabisa.
 
MAWAZO YA KIMASIKINI HAYA
Tuwaache wastaafu wanufaike na jasho lao maana nyingi ni za wastaafu property tax ilipwayo inatosha kabisa.
Kustaafu isiwe sababu ya kutolipa kodi na kutafuta huruma ili hali unaingiza kipato tena sometimes kikubwa kuliko cha wale walioko makazini.

Kumbukeni misaada mnayopewa na wazungu ni kodi za watu wakiwemo wastaafu.
 
Mimi nadhani suala la msingi ni kurasimisha hii sector ya upangishaji wa nyumba, madalali wachukue short courses na wasajili biashara zao...

Wenye nyumba za kupangisha wasajili nyumba zao kama za kupangisha kwenye Bodi itakayoundwa na itakayosimamia home owners...dalali yoyote asipangishe nyumba wala kusimamia nyumba ambayo haijasajiliwa kwenye bodi na sheria iwabane kweli kweli na wao ndio wawe wapelekaji wa Kodi ya zuio TRA on behalf ya mpangaji na mmiliki, TRA wawe na kitengo cha kufuatilia nyumba zinazopangishwa na kujua wanaopangisha (madalali) ni nani na kama wanalip kodi ya zuio 10% ya kodi husika
 
Dalali atakuwaje wakili wa mpangaji ? Hakuna mkataba wowote ambao unaonesha Dalali kumdhamini mpangaji
 
Kazi anayofanya Dalali kumpeleka mpangaji chumba cha shilingi 50,000 inatofauti gani na kumpeleka mpangaji nyumba ya TSH 1,000,000. kwanini malipo yatofautiane. Huku achukue 50K wakati huku anachukua 1M.Huo siyo uwizi wa jasho la watu?
 
Itaishia kama nhc
 
Jamaa atakua dalali
 
Mamlaka ya mapato haiwezi kuanza hizo biashara unazotaka

Jifunze mgawanyo wa majukumu
 
Dalali atakuwaje wakili wa mpangaji ? Hakuna mkataba wowote ambao unaonesha Dalali kumdhamini mpangaji
Kwa taarifa yako Hakuna mwenye nyumba material anayeweza mpokea mpangaji asiyeletwa na dalali anayemjua

Ni Kama daladala au bodaboda huwezi kabidhi mtu usiyemjua lazima apitie kwa dalali sembuse nyumba
 
Hongera umetoa mawazo mazuri sana

Katika watanzania 10, wenye mawazo ya ubunifu kama haya yako ni wawili au watatu, na hata wa kuunga mkono mawazo kama haya, ni wachache sana.

Watanzania tungekuwa tunawaza kama hivi, nchi yetu ingekuwa mbali sana, ila bahati mbaya hatuna culture ya ubunifu tuko tu kusubiri wenzetu wabuni halafu ndio tuige.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…