TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

Stupid move.

Hapo mnataka kuniambia kuna mturuki ataleta pua yake tena hapa Tanzania?

They will come when meko is gone
Mkuu huwajui Waturuki wewe ni Mataperi mno... Bora tu wasije kwanza huwashika shika Makalio hovyo mabinti wetu kule Samaki samaki Masaki hadi uliye pemeni ndio unaona aibu.
 
Hivi Muwekezaji aje na mitambo kisha anataka mikopo ya ndani ya Bank zetu kama sio Taperi huyo ni nani sasa na wa nini sasa? Bora wameshitukiwa... na yale Mamisri yashachemsha kule rufiji wanapotaka kufua umeme hadi Raisi wa China kaingilia kati manaa kaona mmmh!
 
Mkuu huwajui Waturuki wewe ni Mataperi mno... Bora tu wasije kwanza huwashika shika Makalio hovyo mabinti wetu kule Samaki samaki Masaki hadi uliye pemeni ndio unaona aibu.
Mbona wanajenga SGR?
 
Nilifungua biashara nikapewa makadirio kama kawaida nikalipa awamu ya kwanza, biashara haikufanya vizuri kutokana na eneo awamu ya pili wakaendelea kunidai, biashara ikafa kwa kulipa mikodi na nadaiwa mpaka sahivi mapato mengine, nimefunga biashara, sijui kwanini TRA wasiwe USER FRIEND na walipa kodi, sahivi nataka kufungua biashara ingine mkoa mwingine naambiwa maliza kwanza deni la awali na uombe maombi ya kuhamisha TIN
Mimi nimefungua Biashara October 2020, nikakutana na makadirio lukuki
 
Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya Waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha.

Waturuki walitegemea kupata mkopo kwenye moja ya mabenki ya ndani, kitu ambacho kimechelewa. Mategemeo yao ilikuwa ni kupata mkopo mwezi wa 4 lakini hadi Desemba mkopo ulikuwa bado haujapitishwa. Kwa maana hiyo hawakuwa na jinsi ya kuanza operations zao.

Hii kampuni ipo maeneo ya Mbezi Afrikana na kwa bahati mbaya, magari ya TRA wamevamia jioni hii na kufunga ile ofisi na kumchukua mtu anayesimamia ile mali maana wengine inaonekana wako nje ya nchi. Na kwa sababu hakuna kazi, ni mmoja wao amebakia pale kulinda mali.

Hivi si wameambiwa mishahara ya TRA ishushwe? hasira tunahamishiwa mbuzi wa azazeli
 
Wewe wa wapi hakuna mwekezaj anakuja na mtaji, wanakuja na kuchukua mikopo kwenye bank ndo biashara zinazofanywa, tofauti na hapo utaambiwa unatakatisha fedha
BOT huzuia pesa zote zinazotoka nje kuja kuwekeza na wengi hubambikiwa kesi za utakatishaji fedha uhujumu uchumi, waziri Mpingo akimaliza kuisafisha TRA ahamie BOT napo apasafishe pia
 
Na wasiporudi hao Waturuki itakuwaje?

READ! Taarifa inasema Waturuki wamekosa mkopo wa benki za ndani

Maana yake hawakuja na mtaji!

Ndio haya Marehemu Mengi alikuwa anayasema wakati ana bifu na Wahindi, walikuwa wanamwambia tumekuja na briefcase la makaratasi ya business plan za kutajirikia hapa hapa kwenu! Yani sisi ni vichwa panzi.

Magufuli fukuza hao Waturuki!

Thank God Almighty tumepata kichaa mzalendo Ikulu hapapatikii wazungu, hafagilii wageni!

ALHAMDULLILAH ALA KULLI HAAAL HADHA MIN FADLI RABBI
Kama wanakopesheka kulingana na vigezo vya kibenki kwa nini wasipewe mkopo!? Kwani wamekuzuia na wewe kutimiza masharti ili upewe mkopo!? Punguza wivu kama wewe mwenyeji umeshindwa kuziona fursa nchini mwako hilo si kosa lao wao wageni.
 
Twende taratibu, yaani Waturuki wanakuja kuwekeza nchini mwetu kwa kutegemea kukopa kwenye benki za ndani?
Are we serious??
Kabla hatujamlaumu TRA au mtu yeyote, tujiulize hao ni wawekezaji au wanatupotezea muda?
Huo ujinga wa kufikiri bank ipo kwa mkopo wa mwenyeji ni ujinga mtupu, Bank zinafanya biashara zinamkopesha yeyote aliyepo Mazingira ya Tanzania na mwenye uwezo wa kurejesha mkopo acha ubaguzi wako
 
Kama wanakopesheka kulingana na vigezo vya kibenki kwa nini wasipewe mkopo!? Kwani wamekuzuia na wewe kutimiza masharti ili upewe mkopo!? Punguza wivu kama wewe mwenyeji umeshindwa kuziona fursa nchini mwako hilo si kosa lao wao wageni.
Naunga mkono hoja yako kwa 100%
 
Unajua maana ya Local Bank? Yaani unsye muita muwekezaji aje mikono mitupu ategemee mkopo toka Local Bank? Hakuna haja ya kuwa na Kituo cha Uwekezaji.
Bank zinafanya biashara usizipangie wa kumkopesha wapo huru acha ubaguzi wako
 
Hii ni kutoka officer mmoja ya Tra nilimuhoji na akanieleza kuwa tatizo watu hawajui sheria za kodi. TRA hawawezi kuotta kuwa biashara fllani imefungwa au inapata hasara. Unachotakiwa kufanya ni kufile notice au maelezo juu ya mwenendo wa biashara yako. Sasa mtu anaanza biashara leo anapata misuko suko anafunga hata kwa miaka kadhaa ili ajipange na anakaa kimya. Siku anapata nguvu anafungua tena anaenda tra anakutana na deni kubwa.
Huo utetezi wa huyo TRA ni wa kizushi, utakuta mfanyabiashara kafanyiwa ukaguzi na maofisa wa TRA na ana Tax Clearence safi cha ajabu eti wanaenda kumkagua tena? Ukaguzi juu ya ukaguzi kwanza ni dharau kwa wakaguzi wa TRA waliopita na hii ndiyo kero namba one kwani huzalisha Rushwa kukomoana pindi mfanyabiashara akigoma kutoa Rushwa hubambikiwa kodi kubwa na hata kesi haramu za kishetani za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi, TRA ifumuliwe isukwe upya vinara wa kufunga Account za wafanyabiashara wote wachunguzwe na Takukuru.
 
ufanyike uchunguzi kwa maofisa wa TRA Nchi nzima hususani wale vinara wa kuwabambikia kodi kubwa kufunga Account za wafanyabiashara kwani hao ndiyo wapenda Rushwa zaidi
 
Tumeshamaliza kampeni mzee na watu tayari ni wakimbizi wa kisiasa achana na habari za lissu za kusema alituambia
 
ufanyike uchunguzi kwa maofisa wa TRA Nchi nzima hususani wale vinara wa kuwabambikia kodi kubwa kufunga Account za wafanyabiashara kwani hao ndiyo wapenda Rushwa zaidi
Festa wanaweka kwenye majina ya ndugu na marafiki. Na pia kwenye mali siyo benki
 
Hao Waturuki pia hawakujiandaa vyema kuwekeza Tanzania. How comes zaidi ya miezi sita mko na mitambo (assets) ugenini bila kuanza biashara? No way, let them go!
Hujui uachokisema. Watu kama hawa walioonesha utashi na wakawa na assets, huwa wanasaidiwa katika nchi zinazojua nini maana ya wafanyibiashara. Mfumo wa kodi wa Tanzania kamwe hauwalei wafanyibiashara unataka kuvuna tu, kana kwamba biashara siku zote lazima ifanikiwe/ ipate faida! Ujinga na kamwe hakuna kitakachoendelea. Nioneshe mwajiri mmoja Tanzania anayeajiri wafanyikazi hata 300 tu, labda ukitoa makampuni ya migodi.
 
Kwa kweli mifumo ya ulipaji kodi ni ya kipuuzi, halafu kutwa tunaambiwa na kushauriwa jiajirini kujenga uchumi wa taifa, ajira itabaki kuwa tamu aisehh kuliko unajiajiri na kuacha ajira ukitegemea kujiajiri kutafanya vizuri unajikuta unakua masikini zaidi, serikali waliangalie hili.
Hahahah ndio unalitambua hilo sasa mkuu?
 
Wengi wa wawekezaji wa namna hii ni matapeli wanaotegemea kupata fedha kutoka Tanzania badala ya kuja na fedha yao. Mwekezaji gani anakuja mikono mitupu akitegemea kupata msaada serikalini kama siyo matapeli? Uturuki yenyewe apeche alolo. Hawa hawana tofauti na matapeli wengi wa kigabacholi walioletwa na wakoloni wakaendelea kuwa mafisadi wanaokula na watawala mafisadi kama ilivyozoeleka.
 
Back
Top Bottom