Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Hebu ona hapa chiniAma kweli TRA ni jini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hebu ona hapa chiniAma kweli TRA ni jini.
Pitia post #21Kodi karibu na bei uliyonunulia, yaani upumbavu wetu umetufanya tuwe watumwa kwa misheria ya kijinga tuliyojiwekea wenyewe, kila kona ni hivyo hivyo tuu na mitozo isiyo na akili ndio maana hakuna siku tutaendelea
Nadhani hii nchi tuna utaahira fulani hiviHebu ona hapa chiniView attachment 2353107hiyo gari inauzwa usd 14,000 sawa na 32,000,000 lkn ushuru ni 41,00,00View attachment 2353108
Nadhani hii nchi tuna utaahira fulani hivi
Hapana, nchi bado inaamini gari ni anasa na gari inatakiwa kumikiwa na matajiri tu, na kununua gari inamaanisha una pesa hazina kazi.Nadhani hii nchi tuna utaahira fulani hivi
Kwanza taabu inaanziaga Kwny CIF, wanaweka unrealistic.Ukija hapo Kwny excise duty due to age hapo Napo Ni shughuli pevu:Hebu ona hapa chiniView attachment 2353107hiyo gari inauzwa usd 14,000 sawa na 32,000,000 lkn ushuru ni 41,00,00View attachment 2353108
Yaa uchavu unaua sana kwa beiKwanza taabu inaanziaga Kwny CIF,wanaweka unrealistic.Ukija hapo Kwny excise duty due to age hapo Napo Ni shughuli pevu:
- used vehicles aged 8 years but not more than 10 years charged at the rate of 15%
- used motor vehicles aged more than 10 years from the year of manufactures charged at the rate of 30%.
Mara nyingi kwa hesabu za kodi za hii nchi kodi hukaribia au kuzidi bei ya gari.Inawezekana. Tanzania Kodi huwa inakaribia kuwa sawa na thamani ya bidhaa
Na huyo mzee wake Mzee Turky ndie alifanikisha Lissu kuweza kupata ndege ya kupelekwa Nairobi kipindi kile ameshambuliwa(Aliwadhamini).Huyo ni mbunge,mtoto wa marehemu Turky aka Mr White alirithi ubunge wa baba yake,baada ya baba yake kufa ,yeye na wabunge wenzake wanatakiwa walitazame hilo suala la kodi.Kodi haitakiwi iwe sawa au ikaribiane na thamani ya bidhaa.Wakati wa kutunga sheria wao wanapiga makofi tu na kupongeza matokeo yake ndiyo hayo.
Hata kwa gari zingine utaratibu uko hivyohivyo. Yaan ukiagiza IST labda CIF to Dar ni 5.5mil basi mjomba TRA akija na calculator yake anapita nae anga hizo hizo, tofauti kidogo sanaKodi karibu na bei uliyonunulia, yaani upumbavu wetu umetufanya tuwe watumwa kwa misheria ya kijinga tuliyojiwekea wenyewe, kila kona ni hivyo hivyo tuu na mitozo isiyo na akili ndio maana hakuna siku tutaendelea
Basi kama ni hivyo hapo hachomokiNa huyo mzee wake Mzee Turkey ndie alifanikisha Lissu kuweza kupata ndege ya kupelekwa Nairobi kipindi kile ameshambuliwa(Aliwadhamini).
Kuna kitu hakiko sawa kwenye hiyo kodi ukiitazama kwa uhalisia wa thamani ya kitu na si kwa jicho la kikotoo cha TRAView attachment 2353083
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfanyabishara maarufu wa Zanzibar, Toufiq Salum Turky, bado hajalipa Sh. milioni 308.5 za kodi kutokana na kuingiza gari la kifahari aina ya Benzi, Januari, mwaka huu.
Naibu Kamishina wa TRA Zanzibar, Juma Bakary Hassan, aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kinazini, Unguja kuwa gari hilo ilingizwa na mfanyabishara huyo kupitia kampuni yake ya Mifuko Turky ya Zanzibar.
Juma alisema, kiwango hicho cha kodi kinatakiwa kulipwa baada ya maombi ya masamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum.
View attachment 2353084
“Baada ya maombi ya msamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na kutakiwa alipe, waliomba kufanyike tathmini upya baada ya kutia shaka kiwango walichokuwa wanatakiwa kulipa kwamba ni kikubwa lakini hesabu ilikuja ile ile ya mwanzo kulingana na thamani ya gari,” alisema Juma.
Alisema, baada ya kutakiwa alipe, aliomba wapewe muda wa kulipa kidogo kidogo kwa madai hali ya kifedha si nzuri na kulazimika kupewa miezi mitatu kuanzia Mei hadi Agosti, mwaka huu.
“Mpaka muda unamalizika Agosti, amelipa Sh. milioni 138 na bado wanadaiwa Sh. milioni 170 kati ya Sh. milioni 308 .5 alizopaswa kulipa. Tunajiandaa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa kupitia bodi ya dhamana aliyokuwa ameweka kwa kutumia taasisi moja ya fedha,” alisema.
Barua mbili za maombi ya msamaha wa kodi zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sheriff Ali Sharif, ziliweka wazi kwamba, mdaiwa anapaswa kunufaika na msamaha wa kodi kupitia Kampuni ya Mifuko Turky kama mwekezaji.
Hata hivyo, maombi hayo yalikataliwa na Waziri Mkuya kwa sababu muda wa kunufaika kisheria ulikuwa umemalizika baada ya ujenzi wa kiwanda cha mifuko kuwa umekamilika na uzalishaji kuanza muda mrefu.
“Unaweza kunufaika na msamaha wa kodi kama mwekezaji wakati wa ujenzi wa mradi na si baada ya ujenzi kukamilika na uzalishaji unaendelea kufanyika,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa ZIPA.
Wakati hayo yakiendelea, Bodi ya Mapato Zanzibar ilishasajili gari hilo la kifahari na kutoa namba Z-1 kwa malipo ya Sh. milioni 15, na kuonekana likitembea barabarani kabla ya kukamilisha malipo ya kodi.
“Sisi tumesajili na kutoa namba kwa masharti gari lisitembee mpaka wakamilishe taratibu za kodi tukazo kutoa kibali cha umiliki wa gari,” alisema Meneja Uhusiano na Huduma kwa Walipakodi ZRB, Makame Mohammed Khamis.
Gari hilo lenye thamani ya Dola za Marekani 214,668.71, liliingizwa kupitia bandari ya Malindi na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Kimataifa HT Motors Group LTD (UK) kwa kushirikiana na kampuni ya uwakala wa mizigo ya ZARA Freight Forwaders ya Malindi, Zanzibar.
Jeuli ya pesa na alipe tuView attachment 2353083