TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

Kodi karibu na bei uliyonunulia, yaani upumbavu wetu umetufanya tuwe watumwa kwa misheria ya kijinga tuliyojiwekea wenyewe, kila kona ni hivyo hivyo tuu na mitozo isiyo na akili ndio maana hakuna siku tutaendelea
Kama taifa hii ni kasoro kubwa, tumerithi mfumo wa kodi kandamizi kutoka mfumo wa kijamaa, mpaka leo kumiliki gari inatafsiriwa (Sheria ya kodi)kuwa ni anasa.

Gari ni vyombo muhimu katika kuharakisha shughuli za kiuchumi.

Wizara ya fedha ione UMUHIMU wa kutafsiri gari kuwa sio anasa Bali ni muhimu hata mwananchi wa kawaida kumiliki.

Tujifunze kwenye boda boda, zimesaidia ajira, mafuta kununuliwa na hivyo kuchangia kodi kwa wingi.

Makusanyo ya Kodi kutokana na uagizaji magari haijawahi kuzidi makusanyo ya kodi ya bia na sigara bado TRA hamjifunzi kuwa tupunguze kodi magari yaagizwe kwa wingi ili tupate kodi mara 2(kodi kwenye uagizaji na kodi ya mafuta wakati matumizi ya gari).

Tulivyokubali kuruhusu boda boda uchumi wa vijana na ajira uliongezeka.Umeme na maji tunapeleka vijijini kinachofuata ni kuendelea kumletea mwananchi unafuu wa kumiliki vyombo vya moto(punguzo la kodi iwe kwa magari chini ya cc 3000).

Wizara ya fedha rekebisheni viwango vya tozo(import duty),ili tufikie uchumi wa kati mapema zaidi.

Fanyeni tathimini idadi ya wamiliki wa magari ikiongezeka na matumizi ya mafuta ya kiongezeka,pato litaongezeka!
1.Angalau kwenye kila kijiji chenye kaya 200 ,kaya 30 zimiliki gari, kwanini hatuangalii namna ya kuleta unafuu wa maisha hadi kijijini lengo ni kupata mchango wa kiuchumi utokee kijijini kwa kumiliki na kutumia vyombo vya moto.
2.Hizi nchi za kiafrika zinazotuzidi kiuchumi,wao kodi ya uagizaji magari ipo vipi?
3.Kwa nini kodi na tozo zilingane na gharama ya kununua gari?hii ni aibu kwa zama hizi za sasa,hii ifanyiwe kazi tuondoe aibu hii,tunaonekana kama hatuna ubunifu na mbinu sahihi za kutoza kodi.
 
View attachment 2353083
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfanyabishara maarufu wa Zanzibar, Toufiq Salum Turky, bado hajalipa Sh. milioni 308.5 za kodi kutokana na kuingiza gari la kifahari aina ya Benzi, Januari, mwaka huu.

Naibu Kamishina wa TRA Zanzibar, Juma Bakary Hassan, aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kinazini, Unguja kuwa gari hilo ilingizwa na mfanyabishara huyo kupitia kampuni yake ya Mifuko Turky ya Zanzibar.

Juma alisema, kiwango hicho cha kodi kinatakiwa kulipwa baada ya maombi ya masamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum.
View attachment 2353084
“Baada ya maombi ya msamaha wa kodi kukataliwa mara mbili na kutakiwa alipe, waliomba kufanyike tathmini upya baada ya kutia shaka kiwango walichokuwa wanatakiwa kulipa kwamba ni kikubwa lakini hesabu ilikuja ile ile ya mwanzo kulingana na thamani ya gari,” alisema Juma.

Alisema, baada ya kutakiwa alipe, aliomba wapewe muda wa kulipa kidogo kidogo kwa madai hali ya kifedha si nzuri na kulazimika kupewa miezi mitatu kuanzia Mei hadi Agosti, mwaka huu.

“Mpaka muda unamalizika Agosti, amelipa Sh. milioni 138 na bado wanadaiwa Sh. milioni 170 kati ya Sh. milioni 308 .5 alizopaswa kulipa. Tunajiandaa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa kupitia bodi ya dhamana aliyokuwa ameweka kwa kutumia taasisi moja ya fedha,” alisema.

Barua mbili za maombi ya msamaha wa kodi zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sheriff Ali Sharif, ziliweka wazi kwamba, mdaiwa anapaswa kunufaika na msamaha wa kodi kupitia Kampuni ya Mifuko Turky kama mwekezaji.

Hata hivyo, maombi hayo yalikataliwa na Waziri Mkuya kwa sababu muda wa kunufaika kisheria ulikuwa umemalizika baada ya ujenzi wa kiwanda cha mifuko kuwa umekamilika na uzalishaji kuanza muda mrefu.

“Unaweza kunufaika na msamaha wa kodi kama mwekezaji wakati wa ujenzi wa mradi na si baada ya ujenzi kukamilika na uzalishaji unaendelea kufanyika,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa ZIPA.

Wakati hayo yakiendelea, Bodi ya Mapato Zanzibar ilishasajili gari hilo la kifahari na kutoa namba Z-1 kwa malipo ya Sh. milioni 15, na kuonekana likitembea barabarani kabla ya kukamilisha malipo ya kodi.

“Sisi tumesajili na kutoa namba kwa masharti gari lisitembee mpaka wakamilishe taratibu za kodi tukazo kutoa kibali cha umiliki wa gari,” alisema Meneja Uhusiano na Huduma kwa Walipakodi ZRB, Makame Mohammed Khamis.

Gari hilo lenye thamani ya Dola za Marekani 214,668.71, liliingizwa kupitia bandari ya Malindi na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Kimataifa HT Motors Group LTD (UK) kwa kushirikiana na kampuni ya uwakala wa mizigo ya ZARA Freight Forwaders ya Malindi, Zanzibar.
Unaagizaje G Guard Brabus wakati una pesa ya kulia katanga? Kama gari limemshinda kutoa bandarini aseme tumrudishie gharama zake zote, pamoja na riba na hela ya usumbufu na ya kifuta machozi wanaume tuchukue hiyo ndinga, alisikika kaka Mshana Jr akihojiwa na vyombo vya habari vya nje
 
Kama taifa hii ni kasoro kubwa,tumerithi mfumo wa kodi kandamizi kutoka mfumo wa kijamaa,mpaka leo kumiliki gari inatafsiriwa (Sheria ya kodi)kuwa ni anasa

Lakini cha ajabu viongozi wa serikali wanalilia 'wapewe' magari wa thamani ya Tshs. 400,000,000 na hawaoni kuwa ni anasa kubwa kutumia kiasi hicho za fedha kwa kila gari ya kigogo kiongozi.

Huu ni undumakuwili mkubwa kabisa kwa viongozi wanaodai kukusanya kodi kubwa upande mmoja lakini uppande mwingine wanajipendelea kila mmoja wa viongozi kununuliwa gari la thamani kubwa.
 
Unaagizaje G Guard Brabus wakati una pesa ya kulia katanga? Kama gari limemshinda kutoa bandarini aseme tumrudishie gharama zake zote, pamoja na riba na hela ya usumbufu na ya kifuta machozi wanaume tuchukue hiyo ndinga, alisikika kaka Mshana Jr akihojiwa na vyombo vya habari vya nje
Hahaha[emoji23] Buji umeuwaaa
 
Huyo ni mbunge,mtoto wa marehemu Turky aka Mr White alirithi ubunge wa baba yake,baada ya baba yake kufa ,yeye na wabunge wenzake wanatakiwa walitazame hilo suala la kodi.Kodi haitakiwi iwe sawa au ikaribiane na thamani ya bidhaa.Wakati wa kutunga sheria wao wanapiga makofi tu na kupongeza matokeo yake ndiyo hayo.
Plivate jet yao ndo iliyompeleke Tundu Lisu Nairobi alipopigwa Risasi na Wasiojulikana
 
Unaweza kukuta kodi ya ku import Plivate jet ni ndogo kuliko kodi ya ku import hiyo Brabus
Inawezekana lakini Bado TRA kwenye kodi ya Gari hawapo sawa! Burundi japo awana uchumi kama sisi Kodi za Gari ni chini mno- kama vipi akalisajili Burundi kisha hapa analipia kibali cha mwaka mwaka ainjoy
 
Inawezekana lakini Bado TRA kwenye kodi ya Gari awapo sawa! Burundi japo awana uchumi kama sisi Kodi za Gari ni chini mno- kama vipi akalisajiri Burundi kisha hapa analipia kibali cha mwaka mwaka ainjoy
Halafu mwaka ukiisha anarudi Burundi tena halafu analiingiza tena nchini na kuliombea kibali
 
Back
Top Bottom