TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

Kuna gari moja Zimbabwe jumla kodi waliikata kama one milioni of TZS ila huku bongo gari ile kodi kwa wakati huo walikuwa wanachukua kama milioni 10 hivi.
Nenda hizi c center za be forward Japan au SBT kafanye utafiti juu ya hili
Huendi jela kwa kutoza kodi, unaenda huko kwa kukiuka haki za binadamu, na kumshinda mgombea wa upinzani siyo kukiuka haki za binadamu.
 
Namhurumia staff mwenzangu kaagiza BMW X6

Watakachomfanya TRA hataamini, mi niko kwenye kikokotoo chao hapa namzooom[emoji134][emoji134]
hamna tatizo inategemeana na mwaka wa gari
 
''Tilioni'' = Trilion. Matamshi ya hii namba yanawapiga chenga sana wabongo wengi hasa waliosoma shule za sasa. Kuna neno jingine tena i.e. formation. Utasikia mashabiki wa mpira wakisema ''Kocha inabidi abadili ''information'' badala ya formation.
Kumbe ni Trilioni...
Tatizo ni kwamba, hadi nakufa sitazishika hizo chapaa
 
Kuna rafk angu majuzi kidogo afe
We subiria siku apewe assessment ya hio kodi kwenda kulipia uone
We acha tu, ndo naikokotoo kwenye website ya TRA hapa, nimeishiwa nguvu!

Niwe mkweli sijui kama ataweza jamaa, sijui[emoji134][emoji134][emoji1751]...yaaan ni balaa

Ngoja nikuletee screenshot ya hiyo kodi now....


Update..

Hiyo hapo chini nilibargain na wajapa wakatushushia hadi 16000 USD ( mwanzo walikomaa na 19000)

Sasa basi mpaka hili ndinga litue hapa total amount ilikuwa tsh 52m, kodi sasa imeongezeka hapo 11m 52+ 11= 63m

Pa kuipata hiyo 11m ndo komesha

Na hujahesabu wharfage hapo ili abananishe angalau ka mkopo huku na kule, sijui kwa kweli sijui[emoji1751][emoji1751][emoji134]View attachment 1673419View attachment 1673420
 
Nachojua kuna 'CIF value' waliyonayo kwny mfumo wa TRA kwa kila gari

Na kuna 'actual CIF'/invoice price unayonunulia gari

on average CIF za TRA zilikua juu...ss sijui saivi wanakokotoa kwa actual invoice price ama ni wamerevise tu CIF values za mfumo wao
Wamerevise CIF mkuu
 
Heeeee heheeh
Piga picha una gari iko kwny meli inakuja na ulikua na kadirio lako ushajiandaa
Mara paaap ongezeko la 19Million
***** ni nini hiki!!
hata kama jmn dahh
[emoji26][emoji26][emoji26]

It's not fair at all
 
Bei ya dizel zambia lita ni tsh 1200 japo yanapitia Bandari kwetu plus distance ya kuyasafirisha,nguo uganda bei rahisi Hali zinapitia dar
Sidhani kama ni sahihi....nimepita December nadhani ilikuwa kama Kwacha 15 na points....halafu wao wanalipia ada za magari sio kama sisi ishawekwa kwa mafuta.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.
Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.

Taarifa ya TRA iliyotolewa katika gazeti la Mwananchi leo Ijumaa Januari 8 imekuongezeka kwa ushuru wa baadhi ya magari kuanzia Januari mwaka huu kutokana na uthaminishaji uliozingatia bei halisi za magari hayo, huku pia magari mengine yakishuka bei.

“Kimsingi ongezeko hilo limetokana na bei halisi ya magari husika na hivyo haimaaishi kwamba TRA imeongeza ushuru wa magari,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

TRA imesema kuwa magari yaliyotumika hutozwa ushuru wa bidhaa kutokana na umri wa gari ambapo umri wa gari huhesabiwa kwa kufuata mwaka wakalenda.
Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa maika minane hadi tisa pamoja na kodi nyingine hutozwa ushuru huo wa bidhaa kwa asilimia 15 na gari yeye umri zaidi ya huo hutozwa kwa asilimia 30.

“Hivyo ikiwa mwagizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa ikiwa gari yake ingewasili kabla ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waigizaji wa magari yenye umri huo waliagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezaka hivyo wakasema hakuna kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye magari.

TRA imesema katika taarifa hiyo kuwa uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la sheria hiyo.
Mbona taarifa inachanganya sana mara hakuna ongezeko mara kuna ongezeko kidogo..

Swala ni gari imeingia mwaka gani au wanatakiwa waangalie gari imeagizwa lini [emoji23][emoji23][emoji23] aisehh
 
Hujaelewa nini mkuu tukueleweshe?
Sio hajaelewa nini hata wewe nina uhakika hujaelewa, sasa kwanini waangalie gari imeingia kini wasiangalie gari imeagizwa lini???

Pia kwahiyo hilo ongezeke nmtokana na hiyo chat hapo ni ya december 2020 na January 2021 aisehh bado kuna mkanganyiko
 
Kisichoeleweka hapo ni nini, amesema kuwa ushuru unatozwa kulingana na umri wa gari, kwa walioagiza magari mwishoni mwa mwaka jana yakafika mwaka huu, ni dhahiri kuwa mwaka umeongezeka na ushuru inabidi upande kwa kuwa kama gari ilikua na miaka 8 mwishoni mwa mwaka jana kwa sasa sio nane tena ni 9 .. kwa hapa Uganda kama ilikua na miaka 14 isingewezekana tena kuingiza nchini kwakuwa kwakuwa nchi hairuhusu magari chakavu yaliyozidi miaka 15 .. Mi5 tena [emoji109][emoji109] ..
Kutoka Desemba 2020 hadi Januari 2021 ndio kupelekee ongezeko la kodi kutoka 11m to 31m kwa Vanguard ya 2013?
 
Mbona taarifa inachanganya sana mara hakuna ongezeko mara kuna ongezeko kidogo..

Swala ni gari imeingia mwaka gani au wanatakiwa waangalie gari imeagizwa lini [emoji23][emoji23][emoji23] aisehh
Wanaangalia gari imeingia lini ili waumize wananchi vizuri.
 
Back
Top Bottom