TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

Pata picha sasa gari yako ndio iko kwny meli kuja Bongo unakutana na hio kodi ya Tsh. 31m,gari itaishia kupigwa mnada tu.
Kuna unyanyasaji sana ni kama hizo hela zipo , hivi hapa alaumiwe nani waziri wa fedha au hizi mamlaka, watuambie wametumia kigezo gani
 
Umesahau mkuu alishasema magari yamekua mengi anatafuta namna kulidhibiti hilo,
 
Yeah, wanaoumia ni walioagiza gari ambazo zipo kwenye meli kwa sasa. Ni mwendo wa maumivu tu no way. Either utafute hela u top up au gari ipigwe mnada, hasara kubwa hii. Tofauti ya 2-5mil tu inaweza kukufanya uliache gari bandarini hakyanani.
Hilo ongezeko ni pesa ya kununulia hata gari moja tena [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Sio hajaelewa nini hata wewe nina uhakika hujaelewa, sasa kwanini waangalie gari imeingia kini wasiangalie gari imeagizwa lini???

Pia kwahiyo hilo ongezeke nmtokana na hiyo chat hapo ni ya december 2020 na January 2021 aisehh bado kuna mkanganyiko
Kinachoangaliwa hapo ni gari imeingia lini sio umeagiza lini!

Halafu kutokana na corona kutamalaki huko Asia, japan mizigo ilikuwa michache kuja huku, so wakawa wanajikusanya ili wajaze meli kwahiyo unakuta gari umeagiza toka October last year linaingia January hii[emoji848][emoji848]
 
Yaani nikisikia Hawa wahusika,wanahalalisha ongezeko la Kodi kwa kunukuu vifungu vya Sheria,Kana kwamba hizo Sheria ni vifungu vya bible au msahafu,huwa nashangaa sana,
 
Kuna mshikaji wangu kaagiza rav 4 kako kwenye meli huko aliko kama amepata taarifa hii, sijui itakuwaje.
Mjuze ajiandae kisakolojia kabla ya mzigo wake kufika, ajue anafanyaje
 
Na vile mi ndio nilimshawishi ye alitaka kwenda yadi, nitawaambia nini watu, ngoja niangalie kokokotoo tena

Hukujua nae hakujua ni mambo ya risk factor, cha msingi sangi wangewafanyia uwepesi wale walioagiza gari kabla ya mabadiliko maana ni uonezi
 
Kuna gari moja Zimbabwe jumla kodi waliikata kama one milion of TZS ila huku bongo gari ile kodi kwa wakati huo walikuwa wanachukua kama milioni 10 hivi.
Nenda hizi c center za be forward Japan au SBT kafanye utafiti juu ya hili
Nini kinatokea kwamba taifa linategemea kodi hii sana kuliko vyanzo vingine vya mapato
 
Mabadiliko yanapokuja iweje iwaathiri wale walioagiza magari kabla ya muda
 
Wabunge hakuna awamu hii ni mkutano wa ccm .
 
Point yangu kubwa ni kwa haya mabadiliko yani ni vyema haya mabadiliko waangalie mtu alieagiza gari kabla ya haya mabadiliko waendelee tu na utaratibu wa awali, ili mabadiliko yaanze kwa watakao agiza gari kipindi hichi
 
Huko CCM kumesheheni wezi, walaghai, matapeli na wehu tupu.
 
Namhurumia staff mwenzangu kaagiza BMW X6

Watakachomfanya TRA hataamini, mi niko kwenye kikokotoo chao hapa namzooom[emoji134][emoji134]
... Itabidi aka-top up mkopo kupata fedha za kuwalipa TRA. Of course inategemea kama take-home yake bado inaruhusu otherwise kilio cha samaki.
 
Point yangu kubwa ni kwa haya mabadiliko yani ni vyema haya mabadiliko waangalie mtu alieagiza gari kabla ya haya mabadiliko waendelee tu na utaratibu mwingine, ili mabadiliko yaanze kwa watakao agiza gari kipindi hichi
... Mkuu style ya ufanyaji kazi ya TRA ni kuviziana; kushindwa kwa mlipa kodi ndio fahari yao. Na usikute wamelia timing makusudi kipindi hiki ili wanase wengi kwani kule Japan Novemba na Desemba ni kipindi wanaita BIG SALE.

Wana clear stock zao wanauza kwa bei chee so wabongo wengi wanavizia pia msimu huo. Kumbe monster mfilisi wananchi anawacheki tu kwa jicho baya la husda. Na atanasa wengi.
 
Wabunge wa chama gani wafanye hiyo kazi, wakati Upinzani wote umefutiliwa mbali huko bungeni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…