TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Watendaji wa vijiji vyipi unaongelea mkuu? Au ni huko kijijiji kwenu mkuu.. mimi niko tandahimba uko katikati mtendaji wa kijiji hajui chochote kuhusu efd machine halafu anatokea mtu kama wewe unasema nikachukue risiti kwa mtendaji wa kijiji, sasa nashindwa nikuelewe vip maana watendaji unaowaongelea wewe hawana elimu kuhusu iyo efd machine.

Kama mimi dreva nipo newala, katavi uko ndani ndani napataje iyo risiti?
 
Kwanza Jifunze Kujibu hoja kwa upole coz hapa hatujadili Chelsea.
Majibu ya swali lako.
Kama watendaji wa vijiji kwa huko kwenu hawana EFD machine Fanya hivi.
Hapo uliponunua mzigo wako Muulize ntawezaje kukatia risiti huu mzigo. Huwa wanajua ni wapi.
Pili ikitokea hajui Basi Fanya hivi Nenda kwenye Yale mageti (ushuru wa mazao) yako barabarani waambie wakukatie risiti
 
Sawa, ila haya yafanyike
Kwa kuangalia aina ya bidhaa, jamani, hadi chakula?, mtaua watu njaa
 
Sawa, ila haya yafanyike
Kwa kuangalia aina ya bidhaa, jamani, hadi chakula?, mtaua watu njaa
Francis
Hizi mambo mwenyewe naandika ila naumia maana yameshanitesa sana. Ndio maana nahitahidi kufunguka sana ili wenzangu wasikutwe na haya mambo. Lakini watu baadhi wanafanya kama utani hivi. Ila nawaambia usiombe hawa TRA wakukute na hiyo ishu halafu afisa awe ni chalii tu utajuta. Siku moja Mimi nimekatia mzigo risirt vizuri tu na picha niliipiga lakini ile risiti ilipotea nimefika pale makuyuni naambiwa risiti siioni nikawambia Hii hapa kwenye simu, ilikuwa balaa maana tuliongea takribani masaa matatu hapo
 
Jangwani pale wapo wanatega kuna wakati fulani nilipakia sub woofer box kadhaa nmetoa kwenye godown napeleka jangwani kuzituma mkoaa pale jangwani walitupiga tanchi
Sema tuliimba nao sana tukaelewana tukaachna

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kwa wasioelewa Ni hivi kama we ni mnunuzi wa mazao vijijini au mazao ya mbogamboga Kama nyanya,karoti n.k unachotakiwa kua nacho Ni tax clearance kutoka TRA ambayo ndio unaitumia kukatiwa ushuru wa zao ulilobeba na unapopakia kwenye gari mmiliki wa gari au dereva anatakiwa kukupa risiti ya EFD. Kwa hiyo unapokutana na watu wa TRA watachodai kwako ww mfanyabiashara wa mazao Ni tax clearance na risiti ya ushuru na dereva atatakiwa kuonyesha risiti ya EFD.
 
Mkuu hiyo kodi hatozwi mwenye nyanya, hiyo kodi anaitwa msafirishaji yaani mwenye gari.
Inakatwa kwa transportor kutoka katika gharama alizo mtoza mwenye mzigo.
Kama vile 18% ya VAT.

Kama kila tenga alimtoza mwenye nyanya 10,000/= basi yeye atalipa kodi TRA ambayo ni 1,800/= kila tenga.
Hiyo haimhusu kabisa mkulima.
 
Ikiwa kodi hii ni ya ushauri wa mazao, iweje kasha chache za nyanya zisizo zaidi tank moja adaiwe ushuru/kodi?

Zingatia agizo la Mh.Raisi Magufuli kuhusu ushuru wa mazao chini ya tano moja.
 
Hiyo pesa ndio inayonunua shangingi mpya kila wanapopata kiongozi mpya kule mjengoni!
 
Ujinga
 
Zimeshaenea kila kona
 
Haina shida maana mama Na baba Wa wafanyakazi Wa Tra ndo watakaoumia. Baadhi ya wafanyabiashara watafunga bishara ila mnunuzi wa mwisho atakoma. Busara itumike. Narudia tena tumieni BUSARA!
 
Ikiwa kodi hii ni ya ushauri wa mazao, iweje kasha chache za nyanya zisizo zaidi tank moja adaiwe ushuru/kodi?

Zingatia agizo la Mh.Raisi Magufuli kuhusu ushuru wa mazao chini ya tano moja.
Hilo unalosema ni agizo la raisi ni maneno tu. Ila mambo kwa ground ni tofauti.
Hata uwe na Gunia tano Utalipa ushuru tu
 
Hilo unalosema ni agizo la raisi ni maneno tu. Ila mambo kwa ground ni tofauti.
Hata uwe na Gunia tano Utalipa ushuru tu
Mkuu si kweli kuna siku nimepanda gari dogo limebeba boksi 27 za nyanya toka shamba la jirani hadi hapa Dar jamaa hawakutozwa ushuru wa mazao.

Acheni uzushi. Saa nyingine ikitokea umetozwa ni uhuni wa watendaji wa chini siyo agizo la Waziri au raisi au TRA makao makuu.

Kwa vile wewe mwenye mzigo unaogopa utaharibika inabidi ulipe tu badala ya kukomaa kudai haki yako kea kuchoma kulipa huo ushuru.
 
Tax administration act s86(1)(b), failure to issue fiscal receipt
Sheria zipo je nani yupo kuzifafanua hizo sheria katika lugha nyepesi, sio kila mtu anajua lugha ya kigeni au anajua lugha za kisheria,watu waelimishwe kuliko kupewa adhabu sana
 
Nadhani Benki zitakosa fedha toka kwa wafanyabiashara.kwa sababu sheria inawapa TRA kufunga na kukomba hela za watu.hiz ni nguvu za kupita kiasi kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…