TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Huyo dereva aache kazi atafute namna nyingine tu ya kuishi, pia serikali itumie busara, jamani, sasa nyanya zinakuwa bei nafuu sababu ya kujiongeza katika usafirishaji, vinginevyo vyakula vitakuwa bei juu sana na wananchi watateseka, busara itumike
Zitaozea shambani.
Bongo michosho sana
 
Mashine ni ya ofisi, sio ya dereva na dereva kajiongeza na huku kujiongeza ndio hufanya vyakula viwe bei nafuu hata wanyonge wanaweza kumudu kula, sasa tukikaza kila kona hadi kwenye vyakula tutaumiza wanyonge, busara iwe inatumika.
 
Imefika hatua waanze Kukata risiti. Ukipakia tenga moja kata risiti. Ujanja ujanja haupo tena. Hii ilipelekea wenye magari kuibiwa
 
Mkuu iwe Tandam, singo au canter Dereva unapopakia mzigo ni Lazima umkatie risiti mteja wako na hayo magari ni lazima yawe na EFD mashine. Kwa mfano ukiwa unatoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora, Singida na Manyara kuja Arusha na Moshi utakutana na TRA pale Makuyuni. Bila hiyo risiti hampiti hapo.

Na wewe kama mwenye mzigo pia unakaguliwa kama una risiti ya ushuru yenye jina lako pamoja na leseni ya biashara unayofanya. Bila hivyo vitu hupiti hapo.
 
Hao madereva wanajua kila kitu. Hapo huwa wana- gamble kama aliyebeba pembe za ndovu.
 
Rais alisema kama mzigo wako haijavuka tani moja usilipe kodi.
Na karudia rudia mara kibao.

Kwa hio sijaelewa.
Au yale yalikuwa maneno ya majukwaani???
Alisema kama una mzigo chini ya tani moja usilipe ushuru
 
Hili ni Kati ya masuala tata sana.
Kodi muhimu na kodi hii ipo kisheria.

Lakini upande wa pili wa shilingi kodi hizi kwenye usafiri wa mazao ya chakula utaongeza ugumu wa maisha na kushusha kipato cha wakulima wa mazao ya chakula, matunda na mboga mboga, maana madereva sasa hawatathubutu kubeba mizigo midogo kama hiyo njiani. Mazao yatawaharibikia na masokoni kutakuwa na upungufu wa bidhaa kisha bei zitapanda kama ilivyouzwa 1kg ya vitunguu kwa 10,000/- wakati wa Corona.

Lakini tujiulize, kama mwenye mgahawa anatakiwa atoe risiti ya EFD akiuza kitu cha chini ya 30,000 mfano kahawa cupuccino au juice au kuku nusu au Samosa(sambusa) kwanini mwenye kusafirisha mzigo na kutoza 70,000/- au 100,000/- asitoe risiti ya EFD?

Hapa madereva waongee na matajiri wao watembee na EFD na hii pesa ya mizigo ya juu kwa juu wapewe commission kubwa nje ya mishahara yao ili kuwaongezea kipato na kupunguza ugumu wa maisha.

Au
Njia ya pili ambayo mmiliki wa gari si lazima ahusishwe au ajue gari yake ilibeba mzigo wa juu kwa juu.

Kuwe na maafisa wa TRA ambao si wala rushwa wakikutana na mzigo kama huo wanakata kodi halali (yenye uwiano sahihi) kwa huo mzigo, wanatoa risiti ya EFD na gari inaendelea safari.

Kurahisisha zoezi hili na kuepuka udanganyifu wa madereva kuhusu bei walitoza kusafirisha mizigo inabidi TRA waweke vituo vidogo kama check-points au mfano wa vile vya maliasili barabarani kila Kijiji au umbali flani ambapo hapo wenye mizigo na madereva watapakilia hii mizigo na mbele ya hao afisa wa forodha.

TRA inaweza kuweka hata mawakala kwenye vituo hivi kupunguza gharama za kuajiri watu wengi.
Hakuna haja ya ku- centralize kila kitu.

Hivi vituo pia vinaweza kuwa kama vile masoko ya madini Kila wilaya.
Mkulima kazi yako kutoa mzigo wa mazao shamba na gari ndogo kisha kufikisha kwenye vituo hivi. Iwepo na miundombinu ya kusaidia baadhi ya mazao haya yasiharibike yakisubiria usafiri.

Serikali isihusike kabisa kupanga bei ya usafiri wa hii mizigo, hiyo iwe mapatano ya mwenye mzigo na dereva.

Nafikiri haya ndiyo mawazo yangu ambayo si lazima niwe sahihi.
 
Rais alisema kama mzigo wako haijavuka tani moja usilipe kodi.
Na karudia rudia mara kibao.

Kwa hio sijaelewa.
Au yale yalikuwa maneno ya majukwaani???
Lile ni tamko tu, ila halibadilishi nguvu ya sheria waliyonayo hao jamaa
 
Uchumi wa Kati. Hamsomi washamba mnapiga makofi bila kujuwa mnapigia nini.
 
Mashine ni ya ofisi, sio ya dereva, na dereva kajiongeza, na huku kujiongeza ndio hufanya vyakula viwe bei nafuu hata wanyonge wanaweza kumudu kula, sasa tukikaza kila kona hadi kwenye vyakula tutaumiza wanyonge, busara iwe inatumika
Ni kweli Dereva kajiongeza sahihi kabisa ila ndio kakutana na sheria sasa
 
Wakulima nao Wana EFD?.
Mzigo unatoka shamba efd inatoka wapi?
 
Side effects ya hili jambo wafanyabiashara kutokuweka pesa benki, hatimaye benki kuyumba kiuchumi!

Ndio maana wahindi na Wachina hawaweki pesa benki, pindi akipata pesa ananunua dola anaficha ndani.
Hata Mimi siweki pesa benki.
Unaweka laki benki yaani sehemu ya usalama. Ukienda kuicheki baada ya miezi kadhaa unakuta imekatwa umebakiziwa 78,000.
Sasa hiyo benki Ni sehemu salama ya kuhifadhi pesa au utopolo??
 
Naungana nawe, watoe elimu, watoe matangazo, watu waelewe!
Siyo watumie mianya ya wao kujielemisha bila kuelimisha walipa kodi, kuwakomesha walipa kodi!

Everyday is Saturday................................😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…