Hili ni Kati ya masuala tata sana.
Kodi muhimu na kodi hii ipo kisheria.
Lakini upande wa pili wa shilingi kodi hizi kwenye usafiri wa mazao ya chakula utaongeza ugumu wa maisha na kushusha kipato cha wakulima wa mazao ya chakula, matunda na mboga mboga, maana madereva sasa hawatathubutu kubeba mizigo midogo kama hiyo njiani. Mazao yata waharibikia na masokoni kutakuwa na upungufu wa bidhaa kisha bei zitapanda kama ilivyo uzwa 1kg ya vitunguu kwa 10,000/- wakati wa Corona.
Lakini tujiulize, kama mwenye mgahawa anatakiwa atoe risiti ya EFD akiuza kitu cha chini ya 30,000 mfano kahawa cupuccino au juice au kuku nusu au Samosa(sambusa) kwanini mwenye kusafirisha mzigo na kutoza 70,000/- au 100,000/- asitoe risiti ya EFD?
Hapa madereva waongee na matajiri wao watembee na EFD na hii pesa ya mizigo ya juu kwa juu wapawe commission kubwa nje ya mishahara yao ili kuwaongezea kipato na kupunguza ugumu wa maisha.
Au
Njia ya pili ambayo mmiliki wa gari si lazima ahusishwe au ajue gari yake ilibeba mzigo wa juu kwa juu.
Kuwe na maafisa wa TRA ambao si wala rushwa wakikutana na mzigo kama huo wanakata kodi halali (yenye uwiano sahihi) kwa huo mzigo, wanatoa risiti ya EFD na gari inaendelea safari.
Kurahisisha zoezi hili na kuepuka udanganyifu wa madereva kuhusu bei walitoza kusafirisha mizigo inabidi TRA waweke vituo vidogo kama check-points au mfano wa vile vya maliasili barabarani kila Kijiji au umbali flani ambapo hapo wenye mizigo na madereva watapakilia hii mizigo na mbele ya hao afisa wa forodha.
TRA inaweza kuweka hata mawakala kwenye vituo hivi kupunguza gharama za kuajiri watu wengi.
Hakuna haja ya ku- centralize kila kitu.
Hivi vituo pia vinaweza kuwa kama vile masoko ya madini Kika wilaya.
Mkulima kazi yako kutoa mzigo wa mazao shamba na gari ndogo kisha kufikisha kwenye vituo hivi. Iwepo na miundombinu ya kusaidia baadhi ya mazao haya yasiharibike yakirubiria usafiri.
Serikali isihusike kabisa kupanga bei ya usafiri wa hii mizigo, hiyo iwe mapatano ya mwenye mzigo na dereva.
Nafikiri haya ndiyo mawazo yangu ambayo si lazima niwe sahihi.