TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Hili jambo naona watu wengi hawalifaham, mmiliki wa gari ya mizigo eg semi ni lazima awe na mashine ya EFD hii mashine hutumika kutoa risiti kwa wateja wake anaowabebea mizigo. Ikitokea unauza gari hata kama ni scrap lazima utoe risiti.
Kwa mizigo ya local huwa na VAT ndani yake. Kuhusu risiti madereva wenyewe wanafaham na wanaelekezwa kila siku wasipakie mizigo kiholela bila idhini ya ofisi.
 
Anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji au mnunuzi?

Huyo wa kwenda kwa mtendaji wa kijiji labda yule ambaye kununua labda hiyo kazi ya kununua bidhaa na kwenda kuuza ni ndiyo kazi yake mahususi lakini kwa mtu ambaye ni dereva wa Malori ya masafa marefu inakuwa si sawa.

Halafu ni kwambie kitu kwa mikoani huduma za serikali za mitaa ziko scattered kwa sana, Yani ukiwa eneo moja tena mashambani kuambiwa umtafute mtendaji ni mtihani mkubwa sana!

Usichukulie ni rahisi kumfikia mtendaji wa serikali ya kijiji kwa maeneo ya mikoani.
Mkuu haya maelezo yako hapa Wewe unachanganya hisia na sheria.
Cha msingi Wewe ukinunua mzigo wako tafuta sehem kata risiti ya huo mzigo, maana usipofanya hivyo niamin utalia kwa yatakayokukuta. Na utajikuta unalipa hela nyingi kuliko ungekata risiti.
Pale utakaponunulia mzigo jitahidi uwaulize wapi naweza kukata risiti na watakuonesha
 
Sheria ya EFD iko wazi anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji, wajibu wa mnunuzi ni kuidai hiyo fiscal receipt toka kwa muuzaji.

Tuanzie hapo halafu lete hoja yako maana sijakusoma vizuri.
Kwahiyo ukikodi GARI nani anapaswa kutoa risiti mwenye gari au anayesafirisha mzigo? Ww ukipanda basi TIKETI unatoa ww au MWENYE BASI NDIO ANAKUPA RISITI?
 
Hapo muuzaji ni mmiliki wa gari/dereva ambae inatakiwa atoe risiti ya kusafirisha mzigo ampe mkulima
Sheria ya EFD iko wazi anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji, wajibu wa mnunuzi ni kuidai hiyo fiscal receipt toka kwa muuzaji.

Tuanzie hapo halafu lete hoja yako maana sijakusoma vizuri.
 
Elimu imetolewa sana na madereva wanajua hawatakiwi kupakia mzigo wowote ila wanaleta mazoea
Ni chanzo cha rushwa, sidhani kama kila mtu anachajiwa, asipofika bei yao wana mchaji, just common sensr, nenda kariakoo usikie madudu ya TRA walivyokwamisha biashara. Tukubali TZ bado tuna operate kwenye informal economy, ndiyo maana rais wetu mwenye IQ kubwa aliliona jinsi chinga na mama ntilie wanavyochukuliwa vitu vyao na migambo akaleta vitambulisho,
 
Kwahiyo ukikodi GARI nani anapaswa kutoa risiti mwenye gari au anayesafirisha mzigo? Ww ukipanda basi TIKETI unatoa ww au MWENYE BASI NDIO ANAKUPA RISITI?
Watu wengi humu wanaleta hisia sana badala ya kufata sheria. Wanamuonea Huruma kisa kabeba tenga 27 lakini wanasahau Dereva anajua ni Kosa kufanya hivyo.

Wacha walete hisia halafu siku moja wakutane nacho
 
Mimi naona kama kuna wachangiaji huenda kuna jambo hatujalielewa vizuri.

1. Kuna tofauti ya dereva ambaye kazi zake ni kubeba hayo mazao ya kilimo toka mashambani na,
Mfano madereva wa Canters na mafuso ya makabichi toka Lushoto, viazi toka mbeya nyanya toka Moshi au Iringa , matunda toka Mheza n.k

2. Kisha kuna madereva wa masafa marefu waendesha semi trailers ambao wengine huenda kuvuka boda na kwenda nchi jirani .
Hawa mara nyingi husafirisha bidhaa za viwandani nyingine toka ng’ambo (durable goods kwa kiasi fulani) sababu Safari yao huwachukua muda mrefu sometimes.

Sasa aina ya dereva anaeongelewa ni wa aina ya kundi la 2. Hapo juu.

Huyo mara nyingi anapita barabara kuu tu hata watendaji wa vijijini huko ndani hawajui.

Amekutana na wachuuzi wadogowadogo jioni wamemwangukia anunue nyanya zao akawahurumia akanunua, alipowadai risiti wakamwambia hatuijui unaongelea kitu gani huku wakimwangukia anunue bidhaa zao , hapo ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Hili ni Kati ya masuala tata sana.
Kodi muhimu na kodi hii ipo kisheria.

Lakini upande wa pili wa shilingi kodi hizi kwenye usafiri wa mazao ya chakula utaongeza ugumu wa maisha na kushusha kipato cha wakulima wa mazao ya chakula, matunda na mboga mboga, maana madereva sasa hawatathubutu kubeba mizigo midogo kama hiyo njiani. Mazao yata waharibikia na masokoni kutakuwa na upungufu wa bidhaa kisha bei zitapanda kama ilivyo uzwa 1kg ya vitunguu kwa 10,000/- wakati wa Corona.

Lakini tujiulize, kama mwenye mgahawa anatakiwa atoe risiti ya EFD akiuza kitu cha chini ya 30,000 mfano kahawa cupuccino au juice au kuku nusu au Samosa(sambusa) kwanini mwenye kusafirisha mzigo na kutoza 70,000/- au 100,000/- asitoe risiti ya EFD?

Hapa madereva waongee na matajiri wao watembee na EFD na hii pesa ya mizigo ya juu kwa juu wapawe commission kubwa nje ya mishahara yao ili kuwaongezea kipato na kupunguza ugumu wa maisha.

Au
Njia ya pili ambayo mmiliki wa gari si lazima ahusishwe au ajue gari yake ilibeba mzigo wa juu kwa juu.

Kuwe na maafisa wa TRA ambao si wala rushwa wakikutana na mzigo kama huo wanakata kodi halali (yenye uwiano sahihi) kwa huo mzigo, wanatoa risiti ya EFD na gari inaendelea safari.
Kurahisisha zoezi hili na kuepuka udanganyifu wa madereva kuhusu bei walitoza kusafirisha mizigo inabidi TRA waweke vituo vidogo kama check-points au mfano wa vile vya maliasili barabarani kila Kijiji au umbali flani ambapo hapo wenye mizigo na madereva watapakilia hii mizigo na mbele ya hao afisa wa forodha.

TRA inaweza kuweka hata mawakala kwenye vituo hivi kupunguza gharama za kuajiri watu wengi.
Hakuna haja ya ku- centralize kila kitu.

Hivi vituo pia vinaweza kuwa kama vile masoko ya madini Kika wilaya.
Mkulima kazi yako kutoa mzigo wa mazao shamba na gari ndogo kisha kufikisha kwenye vituo hivi. Iwepo na miundombinu ya kusaidia baadhi ya mazao haya yasiharibike yakirubiria usafiri.

Serikali isihusike kabisa kupanga bei ya usafiri wa hii mizigo, hiyo iwe mapatano ya mwenye mzigo na dereva.

Nafikiri haya ndiyo mawazo yangu ambayo si lazima niwe sahihi.
Mkuu ukifanya hivyo magari yatapukutika barabarani. Madereva hawahusiki kwa lolote linalohusiana na matengenezo/tozo au malipo mbalimbali ya gari bali yanamhusu Mmiliki wake.

Sasa unapowaruhusu madereva kupakia mizigo mbali mbali bila idhini ya mmiliki wa gari hilo litawapelekea baadhi ya madereva kuwa waongo. Mf kuna aina mbili za usafirishaji kwa magari ya mizigo
1. Transit Goods
2. Local Goods
Nizungumzie hiyo ya kwanza dereva anaweza kupakia mzigo toka Bandarini Dar kwenda Rwanda. Wakati wa kurudi atarudi tupu. Sasa basi dereva anaweza kupata mzigo kutoka mpakani kuja Njia Panda ya Nyakanazi lkn mzigo huo utamaliza taratibu za malipo baada ya siku mbili. Dereva anaweza kumdanganya mmiliki wa gari kuwa gari lile limepata hitilafu mpakani wakati wa kurudi kumbe ni uongo.
Dereva yule atapoteza siku kadhaa njiani kwakuwa ameshapata chochote bila kujali kuwa gari lile lilitakiwa lifike mapema na kufanyiwa service kisha kupakia mzigo mwingine wa kwenda DRC.

Hapa mmiliki atalazimika kukodi gari lingine la kubeba ule mzigo ili asipoteze tender yake ile. Sasa basi kwanini TRA wambane dereva anapopakia mzigo wa njiani?? TRA ndiyo wanaokuwa walinzi na wasimamizi wa gari lile linapokuwa mbali na mmiliki. Hivyo basi dereva mara apatapo mzigo wa njiani anapaswa kumtaarifu mmiliki kisha mmiliki akamtengenezea hati ya malipo kisha akamfowardia control no na dereva kufanya malipo halali ya Serikali.

Hapo wote wawili Dereva na Mmiliki watakuwa salama.

Kwa hizi Local Goods ni rahisi kuzi monitor kwani hayana tofauti na mabasi. Kuna mawakala sehemu mbali mbali ndani ya Nchi kulingana na routes zako.
 
Mfano wa risiti halali ya EFD
IMG_7489.jpg

Mfano wa risiti halali ya EFD
 
Mimi naona kama kuna wachangiaji huenda kuna jambo hatujalielewa vizuri.

1. Kuna tofauti ya dereva ambaye kazi zake ni kubeba hayo mazao ya kilimo toka mashambani na,
Mfano madereva wa Canters na mafuso ya makabichi toka Lushoto, viazi toka mbeya nyanya toka Moshi au Iringa , matunda toka Mheza n.k

2. Kisha kuna madereva wa masafa marefu waendesha semi trailers ambao wengine huenda kuvuka boda na kwenda nchi jirani .
Hawa mara nyingi husafirisha bidhaa za viwandani nyingine toka ng’ambo (durable goods kwa kiasi fulani) sababu Safari yao huwachukua muda mrefu sometimes.

Sasa aina ya dereva anaeongelewa ni wa aina ya kundi la 2. Hapo juu.

Huyo mara nyingi anapita barabara kuu tu hata watendaji wa vijijini huko ndani hawajui.

Amekutana na wachuuzi wadogowadogo jioni wamemwangukia anunue nyanya zao akawahurumia akanunua, alipowadai risiti wakamwambia hatuijui unaongelea kitu gani huku wakimwangukia anunue bidhaa zao , hapo ungekuwa wewe ungefanyaje?
Mkuu ndo mana nilisema Wewe unachanganya hisia na sheria . Chunga sana Hili jambo litakukost siku moja
Sasa TRA wakikumata huna risiti utawaambia niliwaonea Huruma wale wa kulima?????? Seriously Kabisa??????? Mkuu step up achana na hisia.
 
Hapa tunazungumzia sheria inavotaka, rushwa hyo ni kesi nyingine sasa. Mmiliki wa gari ametoa gar kwenda lubumbashi na irudi empty, dereva anaanza kupakia nyanya na viazi uyole hii si sawa
 
Mzee hata bidhaa ya buku1 kama hujatoa risit unaadhibiwa alieiba simu na nguo wote si wezi tu?? Sheria haiangalii hvo[emoji28][emoji28]

Hiyo ni kwa ambaye tayari ana vigezo vya kuwa na mashine ya EFD na tayari anayo.

Kumbuka sheria ya EFD inahusu wale wenye mauzo ya kuanzia milioni 10-14 unless uniambia sheria imebadilishwa kwamba kila muuzaji wa thamani yoyote kwa Mwaka hata 1000,000 anatakiwa kuwa na EFD mashine.

Tuwe makini ktk kujadili ili tusipotoshe watu.
 
Hapa sisi hatumuongelei mkulima anayekuuzia tenga mia za nyanya ndo akupe risiti , no Sio jukumu lake hilo
Wewe unaponunua hizo tenga 100 za nyanya kuna watendaji huko vijijini ndo wanakuktaia risiti ya EFD au kuna mageti huko ya kukata risiti.

Kwa hiyo elewa Sio mkulima anayekuuzia tenga mia ndo anatakiwa akupe risiti.
 
Mkuu ndo mana nilisema Wewe unachanganya hisia na sheria . Chunga sana Hili jambo litakukost siku moja
Sasa TRA wakikumata huna risiti utawaambia niliwaonea Huruma wale wa kulima?????? Seriously Kabisa??????? Mkuu step up achana na hisia.

Hapana haitatokea kamwe!

Kwanza nikwambie sheria huwa haiamui moja kwa moja , hakimu au mwamuzi huwa anangalia pia facts around the case!

Dereva ametoka masafa marefu amepigika halali mchana wala usiku, milima na mabonde ni yake, huku kaacha nyumbani hakuna hela wala chakula, Boss wake kamwambia hela nitakumia au utakuta utakaporudi, ikitokea ana akiba amekuta nyanya njiani au mkaa amepakia mnamwambia awape EFD receipt?
 
Back
Top Bottom